Saturday, 21 June 2014

Re: [wanabidii] Tanzania kuwekewa vikwazo ikiwa itakataa ushoga

Anayetaka kuamini ujinga huo na aamini. Watanzania wengi hatuamini na hatupo tayari kukubaliana na suala hilo. Waafrika tumesumbuliwa  na kunyanyaswa sana. Kukubaliana na ujinga wa ushoga hakutobadili maisha yetu, bali ni kuzidi tu kudidimia kiakili na kimawazi. Wataendelea tu kutuangamiza kwani umasikini wetu ndio chanzo kikubwa cha kudharaulwa na kunyanyaswa. Ni lazima tuwe imara katka maamuzi yetu. Uganda ni mfano mzuri
Mtanganyika

Od: "Jd ChingaOne" <chingaone@gmail.com>
Do: wanabidii@googlegroups.com;
Wysłane: 10:37 Sobota 2014-06-21
Temat: Re: [wanabidii] Tanzania kuwekewa vikwazo ikiwa itakataa ushoga

Tuache kuishi kwa hisia ila tuishi kwa uhalisia... toa source ya habari yako na sio kumwaga sumu kwenye jambo lenye uharibifu kama hili... sio wote wenye upeo wa uelewa na uchambuzi kwenye habari za kusoma na kusikia..... kwa nini tuishi kwa historia zilizopita na kuhisi ujinga huu utakubalika kwetu? Kuna dalili gani zinazokufanya uamini hivyo?

On Jun 20, 2014 11:09 PM, "'Gikaro Ryoba' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Baada ya Uganda kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani kwa kukataa ushoga, kuna taarifa za chini chini kwamba Marekani ina mpango wa kuzitaka nchi za Kenya na Tanzania kutunga sheria zinazounga mkono mambo ya ushoga, kama ilivyozilazimisha nchi hizo kutunga sheria zinazopinga vitendo vya ugaidi.
 
Msemaji wa wa serikali ya Marekani ameilaani Uganda kwa kutunga sheria inayokataza vitendo vya kishoga na pia kuwanyanyasa wapenzi wa jinsia moja. Ikulu ya White house imelaani sheria hiyo ikisema kuwa inakwenda kinyume na uhusiano kati ya nchi hizo ikitoa wito wa sheria hiyo kufutiliwa mbali. Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amefananisha sheria hiyo na sheria za utawala wa zamani wa kinazi nchini Ujerumani.
 
Ndugu zangu, hivi kweli ikiwa Marekani itavalia njuga suala hili kuna uwezekano Tanzania kugoma kufanya hivyo? Nina wasiwasi kama kweli Tanzania itakubali kukosa fedha za maendeleo kwa sababu tu ya kugoma kuunga mkono vitendo vya kishoga, hasa ukizingatia uhaba wa kifedha unaoikabili nchi. Ngoja tusubiri tuone lakini sina uhakika kama Tanzania ina ubavu wa kukataa ushenzi huo kwa kuwa nakumbuka ilikuwa nchi ya kwanza kutunga mswada wa ugaidi kabla ya nchi nyingine za afrika mashariki kukubali kufanya hivyo.
 
Nina imani kwamba serikali ya Kenya inawezea kukataa ushoga kama ilivyofanya Uganda lakini ni vigumu sana kwa Tanzania kukataa kwa kuhofia kuharibu uhusiano na wafadhili wake na kukosa fedha za misaada ya maendeleo ya wananchi. Mungu epushia mbali ushenzy huo usifike Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment