Saturday, 21 June 2014

Re: [wanabidii] Re: AJALI YAUA 7 LUGALO , DAR ES SALAAM

Twawapa pole. Ila ajali nyingi zitatokea GVT isipotenga njia au barabara kufanya kama wenzetu ulaya na marekani kuwa na barabara tofauti kwa magari ya aina za shughili tofauti unapoingia miji mikuu na nje ya miji kuelekea bandari na nchi jirani. Njia ya lori za mizigo tofauti na ile ya kupita bus za mji, tofauti na za bus za abiria za kwenda nje ya mji tofauti na ya taxi, gari binafsi, pikipiki; njia ya waenda kwa miguu mwiko chombo au kikwazo chochote. Hapa bongo tu vichwa sugu tusiosikia, utii mdogo wa sheria. Pamoja na speeding kuogopana kutokana na wanga wa kisasi kufikia abiria kumuogopa koda na dreva kumwambia asikimbie hovyo aufyate au watamfyatua. Lori za trela full mzigo mbio sana na kusotea matakoni nyuma ya bus, taxi, bajaji. Kwa nini lori za kwenda wazo zisipite mbezi makabe-wazo barabara pekee; kimara-mlonganzila-pugu-kilwa road-bandari zisiingie mjini wawe na njia yao pekee. Ipite gari si lori-piga, firisi gari kuweka nidhamu na utii wa sheria kuondoa ajali za kijinga.toza kodi kubwa ya parkin


---Original message---
From: 'lesian mollel' via Wanabidii
Sent: Sat, 21 Jun 2014 17:06:54 -0700
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: AJALI YAUA 7 LUGALO , DAR ES SALAAM


Nilikuwepo maeneo haya
Nawapongeza sana wanajeshi wetu wa kambi ya chi brigade na Lugalo wamesaidia sana kuokoa majeruhi
Kwa kweli tatizo ni speed kali ya dereva wa dala dala lililokua likienda Ubungo likitokea mtongani, nadhani gari lilikata labda break na kupoteza mwelekeo na kuhamia upande wa magar yaliokua yakielekea Tegeta na kulifyeka hiyo coaster....kiukweli maafa ni makubwa na yalikua ya kutisha hata sikuweza kutoa simu kupoga picha nilijikuta nabubujikwa na machozi......Madereva  wasioa na busara au wavuta bangi wasipewe kuendesha abiria jamani
Kwa haraka niliona maiti zaidi ya kumi though nasikia imetangaza 6 mmmmmh
Hali ilikua inatisha jamaniiiiii, acheni


On Saturday, June 21, 2014 4:22 PM, Oksana Spice <worldngojobs@gmail.com> wrote:






On Saturday, June 21, 2014 4:19:08 PM UTC+3, Oksana Spice wrote:
Ajali mbaya ya gari imetokea mchana huu, katika maeneo ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Katika ajali hiyo, inakadiriwa zaidi ya watu saba wamefarik

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment