Mwandishi kajawa na lindi la udini moyoni, ubuongoni, damuni na mwilini.Nimeshindwa kumalizia kusoma sababu upuuzi kama huu sina ushabiki nao.
--
Sent from myMail app for Android
Saturday, 21 June 2014, 00:16AM +0300 from Magora Hassan <magorah15@gmail.com>:
Rgrds
Magora
---------- Forwarded message ----------
From: "Magora" < hmagora@yahoo.com >
Date: Jun 21, 2014 12:13 AM
Subject: Fwd: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
To: < magorah15@gmail.com >
Cc: < hmagora@yahoo.com >
-------- Original message --------
Subject: CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU Z'BAR
From: musa khamis < mizanimedia@yahoo.com >
To: Magora Hassan < hmagora@yahoo.com >
CC:
CCM IFAFANUE TAMKO LA LUKUVI DHIDI YA UISLAMU NA MADAI YA KUREJEA WAARABU
Z'BAR
Kutoka gazeti la mizani june 20, 2014
Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera Uratibu na Bunge), ndugu William Lukuvi, alitoa kauli nzito Kanisani huko
Dodoma ambayo ilikuwa na maudhui kadhaa ikiwemo kuwataka wananchi kupinga
serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na akatoa
vitisho kwamba vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya
Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.
Ndugu Lukuvi alikaririwa akisema hayo mnamo
13 Aprili mwaka huu, katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa
mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mbele ya waumini
waliofurika katika ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu wa
Kanisa hilo katika jimbo, na akatoa ombi kwa waumini wa Kanisa kuwa waendelee
kuliombea Bunge lifanye uamuzi sahihi wa Serikali mbili.
Mimi binafsi hayanishughulishi matamko
ya Ndugu Lukuvi ya kupiga kampeni ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
wenye muundo wa Serikali mbili kama ilivyo sasa. Hii ni kwa sababu hata mimi
binafsi naunga mkono muungano wa mfumo huo nikiwa na dhana kuwa kuondoa kero za
muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko kuongeza mzigo wa Serikali nyingi
ambazo hazina tija wala hatuna uwezo wa kuziendesha.
Aidha rasimu ya Katiba iliyowasilishwa
na Tume ya Jaji Warioba kwa upande wetu Waislamu tunaiona haifai hata pesa
mbili, kwa sababu imezingatia udini zaidi kutokana na kutokuwemo ndani yake maoni ya jamii ya Waislamu. Jaji Warioba na
wenzake hawakuwa na haki hata kidogo ya kupuuza maoni ya jamii kubwa kama ya
Waislamu kwa kiwango kwamba wakaona hayafai hata kujadiliwa. Huo ni udini
ulioanikwa katika jua kali la mchana wa kipwa na wala si kazi waliyoteuliwa
kuifanya.
Katika ujumbe wa Ijumaa hii, sikusudii
kuzungumzia suala la muundo wa Muungano. Nia yangu kutafakari maelezo
yaliyohusu Uislamu kama dini yangu, ndani ya hotuba ya Ndugu William Lukuvi katika
hotuba yake akiwa ndani ya Kanisa ambako ameupaka matope Uislamu na
kuudhalilisha.
Ndugu Lukuvi akiwa ni Waziri katika Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) ametushitua sana Waislamu hapa nchini pale
alipotoa matamko yanayoonyesha uadui iliyo nayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania juu ya Waislamu, kwa kiwango kwamba sababu za kutowapa Wazanzibari
haki zao ni kwa kuhofia Uislamu ambao Lukuvi anadai ni kitu hatari. Isitoshe
Lukuvi ameonyesha chuki kwa Waarabu ambao ni Waomani waliotawala Zanzibar nchi
ambayo kwa ni rafiki na ndugu wa kihistoria w Tanzania.
Kwa kuwa Lukuvi ni Waziri anayesimamia
sera za Serikali, na ukizingatia ukweli kuwa Serikali hii ni ya chama cha
Mapinduzi (CCM), utapata jibu kuwa Sera ya CCM ni kuing'anga'nia Zanzibar kwa
kuhofia kuwa, kwa kuwa asilimia 95 ya Wazanzibari ni Waislamu, basi wanaweza
kuamua kuunda Serikali ya Kiislamu ambayo Sera za Serikali inaona kuwa hilo ni
jambo hatari kwa usalama wa Tanzania Bara.
Kabla ya kuendelea mbele tafadhali
msomaji rejea sehemu ya maneno ya Waziri Lukuvi na hapa ninamnukuu:
''Tunataka tuwaache Wazanzibari
wajitawale wenyewe na Tanganyika! Wazanzibari kule waliko asilimia 95 ni
Waislamu. Tunataka wajitangazie Serikali ya Kiislamu kule? Mnajua madhara yake?
Wale waarabu watarudi. Watazalisha siasa kali kule watakuja kutusumbua, mimi
najua, kabisa...'' mwisho wa kunukuu.
Sisi kama viongozi wa Taasisi, Waalimu na
Masheikh wa dini ya Kiislamu, wajibu wetu wa kwanza mbele ya Mwenyezi Mungu na
Mtume wake (SAW) na mbele ya waumini tunaowaongoza ni kuutetea na kuunusuru
Uislamu pale unaposhambuliwa na kusingiziwa na watu kama Ndugu Lukuvi.
Kwa msingi huo haiwezekani hata kidogo, iwe
Ndugu William Lukuvi kama alivyo kiongozi mwandamizi Serikalini, awe ametumwa
na Serikali, au CCM, au hata kama iwe ni kwa chuki zake kinafsi, au fikra zake
tu, atoe tamko la kuudhalilisha na kuutangazia umma kuwa Uislamu ni imani ya
kutisha na kuogofya, na kisha sisi tunaojifanya wahubiri na watetezi wa Uislamu
tukae kimya. Tukikaa kimya tutakuwa tumeogopa na kuwasaliti Waumini
tunaowaongoza. Na kwa wajibu huo tunajibu tuhuma zake kama ifuatayo;
Kwanza ni juu ya tamko lake kuwa Tanganyika
ikiiacha Zanzibar, basi kwa kuwa asilimia 95 ya Wazanzibari ni Waislamu
wataunda Serikali ya Kiislamu. Kwa tamko lako hili ndugu Lukuvi, umekusudia
kuonyesha kuwa ninyi Wakristo mliomo ndani ya Serikali ya Muungano au serikali
yenyewe katika vikao vyenu vya siri, hamuupendi Uislamu na kwa chuki hizo
mnaishikilia Zanzibar kimabavu kwa hofu kuwa isije ikawa taifa la Kiislamu.
Aidha tamko hilo linadhihirisha ukweli ambao
kila mtu anautambua kwamba, misingi ya kuunda muungano haikufuatwa wakati wa
kuziunganisha nchi mbili hizi. Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume walikubaliana
wao wenyewe kuziunganisha nchi zao na kila mmoja kati yao alikuwa na sababu
zake binafsi. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kulaumu dhamira yao njema na
hasa kutokana na mfumo na nidhamu ya utawala enzi hizo na shakhsiya ya watu wenyewe
na imani ya wananchi juu yao kwa wakati huo.
Ndugu Lukuvi anapaswa kufahamu kuwa wakati
Sheikh Abeid Amani Karume akifanya Mapinduzi Zanzibar waislamu walikuwa ni
wengi na zaidi ya asilimia 95 anazotaja yeye. Kama leo Zanzibar kuna asilimia
95 ya Waislamu, basi hiyo asilimia 5
anayodhani kuwa ni ya Wakristo ni wahamiaji ambao wamehamishiwa Zanzibar kutoka
Bara kwa shabaha ya kupandikiza Ukristo Zanzibar na kwa lengo hilo hilo
wamekuwa wakinunua ardhi ya kuanza kujenga Makanisa ambayo hayahitajiki, jambo
ambalo limekuwa likizusha chuki na kusababisha vitendo vya uchomaji wa
Makanisa.
Lakini kubwa kuliko yote tunamuuliza Ndugu Lukuvi
kabla ya Muungano wa mwaka 1964, Zanzibar ambayo ilikuwa ikitawaliwa na Sultan
Muomani kulikuwa na Serikali ya Kiislamu? Na je Serikali hiyo ilikuwa na
madhara gani kwa amani na usalama wa Bara? Na je Mzee Karume alipopindua
Serikali ya Sultan aliunda Serikali ya Kiislamu? Je kabla ya Mapinduzi na baada
ya Mapinduzi ni jambo gani linalotokana na Uislamu wa wazanzibari limekuwa
hatarisho la usalama wa Watanganyika na hususan Wakristo? Tunataka jibu lako,
au la Serikali au CCM yenyewe.
Juu ya madai ya Ndugu Lukuvi kuwa sababu ya
Tanganyika kuing'ang'ania Zanzibar ni kuwa eti waarabu watarejea na kuzalisha
siasa kali, tunamuomba Ndugu Lukuvi afahamu kuwa maneno yake hayo hayana ukweli
wowote ule na hayakutegemewa kutamkwa na mtu mzito Serikalini ambaye amepewa
dhamana ya kusimamia Sera za Serikali.
Hadi sasa bado tunamuona Lukuvi kama mtu mwenye
nia njema ya kutaka kuhakikisha muungano unadumu, lakini mwenye kutumia njia
isiyofaa ambayo inajenga chuki baina ya Waislamu na Serikali ambayo yeye ni
kiongozi wake.
Ndugu Lukuvi unaweza kutueleza ni madhara gani
yatakayotokea kwa Watanganyika iwapo wazanzibari ambao wewe mwenyewe unasema ni
Waislamu kwa asilimia 95 wakiamua kujitawala wa mfumo wa Serikali yenye kufuata
maadili ya dini yao wenyewe ya Uislamu? Unasema maneno haya kama kiongozi wa
Serikali au Mkristo mwenye kuchukia Uislamu? Kama si yote mawili unasimamia
wapi wakati unapowatishia wananchi na kuwataka wawe na hisia mbaya juu ya
Uislamu?
Sisi hatudhani kama ni busara kwa kiongozi
mzito kama wewe kujaribu kuwatia hofu na kuwatisha wananchi kwa kutolea mfano dini
ya Kiislamu ambayo unafahamu fika ina wafuasi ambao wako tayari kuipigania dini
yao kwa hali na mali? Aidha tunakuomba ufute kabisa maneno yako unayoutuhumu
Uislamu kuwa ni ''SIASA KALI''.
Mimi nafahamu wazi kuwa wewe hujui chochote juu
ya Uislamu. Na sifa ya mwanadamu kamili ni ujinga, na dawa ya ujinga ni kusoma. Nani aliyekwambia katika Uislamu kuna mafunzo
yanaitwa imani ya siasa kali? Panua
ufahamu wako kwa kufahamu kuwa hakuna kinachoitwa siasa kali katika Uislamu.
Tamko hilo ni neno lililotungwa na viongozi wa Kikristo wa mataifa makubwa kwa
nia ya kuzishambulia na kuziangamiza nchi za kiislamu kwa chuki zao na kwa nia
kupora utajiri wao.
Kwa faida yako na napenda nikupe darsa la
maneno machache ambayo yatakuelimisha na kukuweka katika ufahamu wa nini maana
ya Uislamu kama ifuatavyo;
Dini ya
Kiislamu ni sheria, kanuni na maadili ya Kiungu ambayo ndani yake kunapatikana
mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu na
viumbe wote. Katika kanuni hizo Mwenyezi Mungu hajawahi kuufanya uhalifu
kuwa ni mfumo kamili wa maisha ya viumbe. Bali Mwenyezi Mungu ametutaka
tufahamu kuwa uadilifu ndiyo mfumo sahihi na timilifu wa maisha ya viumbe.
Ili maisha ya viumbe yawe ya amani, ni lazima
uadilifu uwe ndiyo msingi wa maisha yenyewe, na uadilifu ni utiifu wa kanuni na
sheria zilizoletwa na Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume wake. ukipatikana
Uadilifu ndipo amani pia hupatikana. Na hii ni kwa sababu amani ni zao la
uadilifu.
Uadilifu si swala linaloweza kunasibishwa na
imani fulani, bali ni swala la kimaumbile kwa kuwa ni silika ya kila mwanadamu
kupenda uadilifu na kuchukia dhulma. Na ni kwa sababu ya kutaka kusimamisha
uadilifu ndiyo maana tunaona mahakama zimewekwa hadi kwenye jamii zisizokuwa na
dini ili kila mwenye kudhulumiwa awe na pahala pa kupatia haki yake nia ikiwa
kusimamisha haki.
Ndugu Lukuvi, hiyo ndio maana ya Uislamu
tuliyojifunza sisi wenyewe Waislamu. Huo Uislamu wa siasa kali unaowatisha nao
watu umejifunza wapi? Kutoka kitabu gani cha Kiislamu? Na ni hivyo ndivyo Sera za Serikali ya Jamhuri
ya Muungano zinavyoitakidi kuhusu Uislamu? Unadhani Waislamu tungetambua kuwa
CCM na Serikali yake vinautazama Uislamu kama adui tungekuwa wapenzi na wanachama
wa adui yetu?
KUREJEAA WAARABU Z'BAR
Ndugu Lukuvi kama walivyo wanasiasa wengine
wenye chuki, akiwa Kanisani aliwatisha Waumini wa Kikristo kwa kuwaambia kuwa
endapo Tanganyika itaicha Zanzibar, basi Waarabu watarudi kuleta siasa kali za
kiislamu ambazo madhara yake amedai eti anayajua. Hili nalo si jambo la hakika.
Ni propaganda za chuki kwa waarabu lakini msingi wa chuki hii ni kuchukia
Uislamu.
Lukuvi anapozungumzia kurejea tena utawala wa
Waarabu, anazungumzia Dola ya Usultani wa Omani ambao hivi sasa inaendeshwa na
mjukuu wa Wafalme hao ambaye ni Sultan Qaboos bin Said Al Said.
Lakini kwanza nataka Ndugu Lukuvi aelewe kwamba
sisi sote tunautaka muungano. Na lazima muungano huu ujengeke katika misingi imara
ya maridhiano na sio kama anavyofanya Lukuvi kuweka vitisho vilivyojaa chuki akidhani
kufanya hivyo kutasaidia maridhiano. Labda tumsaidie Ndugu Waziri Lukuvi
kufahamu anachosema juu na hao anaodai kuwa ni Waarabu na anaohofia watarudi
Zanzibar.
Waarabu waliokuwa wakitawala Zanzibar ni wa kabila
la Al Busaidi na Al Said. Waarabu hawa walitawala Zanzibar miaka mingi kabla ya
ujio wa Ukristo. Wakati Ukristo ukiingia Zanzibar uliukuta Uislamu kwa miaka
zaidi ya 800. Ni Sultan wa Zanzibar (Muarabu) ndiye aliyewapa kiwanja Mapadre
cha kujenga Kanisa na akawapa pia saa kubwa iliyowekwa juu ya mnara wa Kanisa. Ndugu Lukuvi ukijikumbusha hayo
utafahamu vema Uislamu unavyowatazama Wakristo, si maadui ni marafiki na hata
ni ndugu.
Tunaomba Ndugu Lukuvi afahamu kuwa Waarabu
waliokuwa wakitawala Zanzibar hawawezi, hawana mpango wala nia ya kurejea
kutawala Zanzibar. Wakafuate nini Zanzibar? Ukoo uliokuwa ukitawala Zanzibar
hivi sasa unatawala Dola ya Usutani wa Oman. Kiongozi wa Dola hiyo ni Sultan
Qaboos bin Said Al Said.
Napenda nimjuze Waziri wetu kuwa historia
inatukumbusha kuwa Dola ya Oman ilikuwa Dola kubwa miongoni mwa Dola za
Kiarabu. Enzi za utawala wa Masultani wawili ndugu, Yolanda na Jolanda, Oman
ilikuwa ni pamoja na nchi zote zinazofahamika sasa kama nchi za Umoja wa Falme
za kiarabu ambazo ni pamoja na Abu Dhabi , Umm al-Quwain , Ras al-Khaimah , Sharjah, Dubai na
Ajman. Usultani wa Umani ulianza miaka ya 751 na Al Said umeanzia mwaka 1744 na
ungali ukiendelea hadi sasa.
Falme za Kiarabu
zimekuwa nchi tajiri hivi sasa kutokana na akiba kubwa za mafuta
ya petroli . Utajiri huu unapatikana kwa viwango
tofautitofauti kati ya nchi za Imarat zinazounda shirikisho hili. Abu Dhabi ikiwa
ni mwanachama mkubwa na kiongozi wa huo muungano ina pia kiasi kikubwa cha
petroli na mapato makubwa kutokana na mauzo ya mafuta.
Kama Sultan Qaboos
angekuwa na tamaa na kutaka kutawala, kwanini asigombee kurejeshewa ardhi zake
ambazo hivi sasa zimeganywa katika mataifa madogo madogo na sasa yanatajwa kuwa
tajiri, badala yake aje akagombee kurejea kutawala Zanzibar? Kwani Zanzibar
kuna nini cha kuisaidia Oman?
Aidha kwanini Waarabu
wa Oman watoke maelfu ya kilometa kuja Zanzibar badala ya kupigania nchi yao
iliyojaa utajiri wa mafuta ambayo imegawanywa vipande vipande na ambayo
hawahitaji kusafiri ili kuikomboa? Je watu hawa wana azma kweli ya kupanua
himaya yao kama anavyosema Lukuvi?
Ni vizuri kufahamu pia
Sultan Qaboos bin Said ni kiongozi ambaye anaheshimika na kusifika kwa utawala
wake wenye kuzingatia haki na uadilifu na asiyependa mapambano wala siasa za
kujitukuza na kujitanua. Sultan Qaboos amekuwa msuluhishi mkubwa sana katika
eneo la Ghuba ya Uajemi kwa matatizo na hitilifu zinazoyakumba mataifa ya
kiarabu.
Sultan Qaboos katika
utawala wake amefanikiwa kujenga nchi yake ya kuboresha kiwango cha maisha ya
wananchi wake kwa kiasi kwamba ni vigumu katika nchi ya Oman kutambua nyumba
anayoishi ndani yake masikini na tajiri.
Mfamle Qaboos ni
mtawala mwenye kujali na kusikiliza kwa nia ya kutatua matatizo ya raia wake,
na kwa nia hiyo amejiwekea ratiba ya kutembelea vijijini nchini mwake, ambako
huko hukaa katika mahema majangwani. Akiwa mikoani hukutana na wakuu wa
Makabila (machifu) na kupata fursa na kusikiliza vilio vya raia wa ngazi ya
chini kabisa uso kwa uso. Akiwa Muscat Sultan hukutana na wananchi karibu kila
siku na kusikiliza shida zao na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa hapo.
Hali hii imepelekea
Sultan Qaboos kuwa kipenzi cha Waomani kwa kiasi kwamba ukitembelea nchi hiyo
huwezi kukutana na Muoman ambaye anamlaani, kumpinga, kumlaumu au kulalamika
juu Sultan Qaboos wala kusema maneno ya fedhuli dhidi yake na kila raia
anamuombea dua njema.
Hali hiyo ni tofauti
na hapa nchini ambapo moja ya sifa yetu watanzania ni kuwatukana,
kuwadhalilisha na kutokuwa na adabu na viongozi wetu. Mimi binafsi nasoma kila
siku gazeti moja ambalo lina ukurasa maalum kwa ajili ya kumtukana na
kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete binafsi, sijakwambia Mawaziri wake.
Wakati Rais Kikwete
akigombe muhula wa pili baadhi ya ndugu zake Lukuvi wakristo walitoa mwito wa
kukesha makanisani usiku wa kuamkia kupiga kura na kulishana kiapo cha
kutomchagua JK kwa sababu ya chuki kwa nini atawale mwislamu. Ukiwa Serikalini
bila shaka unajua jambo hili na mengine mengi ambayo hapa si wakati wake.
Oman nchi ambayo ardhi
yake imetawaliwa na majabali, haina mito, maziwa wala mvua, haina taabu ya maji
kama iliyopo Tanzania ambayo ina mito, mabwawa, maziwa, maji mengi chini ya
ardhi na pia bahari. Miundo mbinu ya barabara imezunguka nchi nzima huku
zikijengwa bara bara za kisasa za juu (flyovers) ambazo Tanzania hadi
tunafikisha miaka 50 ya uhuru hakuna hata barabara moja kama hiyo. Mjini Muscat
kuna barabara kama hizo zaidi ya kumi na mwishoni mwa mwaka huu zinatazamiwa
kufikia 20 kwa mji mmoja tu.
Mfalme Qaboos katika
kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake anatoa elimu bure na kugharamia elimu
ya juu nje ya nchi kwa gharama za serikali. Kima cha chini kabisa cha Muomani
Serikalini ni Riyale za kiomani 381 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania
1,562,000/=. Aidha kima cha chini katika sekta binafsi ni Riyale 325 ambazo ni
sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania 1,330,000/=.
Muomani ambaye
anafanya kazi anaruhusiwa bila pingamizi lolote kuchukua mkopo wa gari na
nyumba, ambapo mkopo wa nyumba utadumu kwa miaka 20 ya mkopaji na endapo
mkoapaji atafariki wakati wowote baada ya kupokea mkopo wake wa nyumba, basi
Benki haina haki ya kupokea marejesho kutoka kwa warithi. Watu wanaoishi katika
hali kama hiyo Ndugu Lukuvi wanakuja kutawala Zanzibar ili wapate kitu gani?
Pamoja na kuanzishwa
mataifa mengine ndani ya ardhi ya Oman Sultan Qaboos pia amesamehe ardhi ya
nchi yake iliyoporwa kimabavu na watawala wa ukoo Al Saud wanaotawala hivi sasa
Saudi Arabia. Sultan Qaboos amesamehe ardhi hiyo huku dunia ikijua kuwa
imevamiwa na watawala wa Saudia kwa tamaa ya mafuta yaliyopo katika eneo hilo. Ikiwa
hali ya mambo ni kama hivyo tunawadanganyaje wananchi kuwa Waomani watarudi
Zanzibar wakiwa wanakuja kuanzisha siasa kali ili kuhatarisha Maisha ya akina
Lukuvi? Ama kweli chuki ya kidini humpeleka mtu mbali na ukweli!
Sasa tuangalie nchini
Oman kwenyewe ambako watu wengi wana uhusiano na Tanzania Bara na visiwani.
Kwanza lazima tukiri kuwa watu wa Oman na Tanzania wana uhusiano wa karibu sana
na wa kidugu. Wako Waomani Waarabu waliozaliwa na mama wa kiafrika na pia wapo
wale ambao baba zao ni waafrika na mama zao ni waarabu. Watu kama hawa mahala ambapo
uadilifu unatawala ni raia wa nchi zote mbili.
Ndugu mmoja alipokuwa
Marekani akisoma na mkewe walibahatika kupata mtoto huko Marekani na kisha
baada ya masomo yao walirejea nyumbani. Baada ya miaka mingi kupita binti yao
huyo alikwenda kwenye ubalozi wa Marekani kuomba visa ya masomo na akaacha hati
yake ya kusafiria ubalozini hapo. Aliporudi kuchukua visa aliambiwa kuwa
Marekani haiwezi kumpa visa raia wake anapotaka kwenda nyumbani. Na hii
ilitokana na kumbukumbu kuonyesha kuwa binti huyo alizaliwa Marekani kwa hivyo
ana haki zote za Taifa hilo.
Hivi ndivyo
ilivyostahili kuwa baina ya Waarabu wenye asili ya Omani ambao walizaliwa
Tanzania badala ya Sera mbovu za Ndugu Lukuvi za kujaribu kuwatisha wananchi
kwa kulifanya jina la mwarabu kuwa tishio kwa amani na usalama wa nchi yetu
badala ya ndugu. Hawa ni ndugu zetu na hawawezi kamwe kuisahau Tanzania na lazima
watakuja kwani hapa ni kwao na wana haki japo Serikali kwa chuki za Wakristo
wenye ushawishi Serikalini wanajaribu kupandikiza chuki na kuweka vikwazo.
Wakoloni daima huzivamia nchi zetu kwa nia ya
kutaka kupora utajiri wetu wa mailiasili. Ukoo wa Al Said na Al Busaidi hauwezi
kurejea Zanzibar kwa kuwa hakuna wanachokihitaji huko. Na ikiwa hali ya Omani
ni nzuri kiuchumi na kuna Serikali inayosimamia vema mapato ya nchi, Waomani
wanaoingia Zanzibar wanafanya hivyo kwa kuwa zanzibar ni kwao walikozaliwa na
wala si kwa ajili ya kupelekea Uislamu ambao Lukuvi anauchukia.
Ni jambo lililo wazi kuwa Wazanzibari wenye
asili ya Oman wameisaidia sana Zanzibar kwa kuingiza mitaji na kuanzisha miradi
mbai mbali ya kiuchumi ambayo kwa kiasi kikubwa imesadia kupunguza hali ya
ufakiri na umasikini baina ya wazanzibari na kuboresha hali za maisha yao.
Labda kinachomkera Lukuvi ni kuona Waislamu Zanzibar hali zao zinaimarika huko
Zanzibar na kwa kiwango fulani kufeli njama za kuuangamiza Uislamu kwa
kuanzisha kila mahala Makanisa ambayo hata hivyo hayana wa kusali ndani yake.
Nimalize ''Ujumbe wa Ijumaa'' kwa kutoa tamko
ambalo majibu yake yataleta natija ya maudhui hii kwa kusema, Nawaomba viongozi
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kama wao hawana wakati wa kujibishana na
sisi mnaotuita "SIASA KAli" basi niwaombe viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdurahmani Kinana na Ndugu Nape Nnauye watupe ufafanuzi
Waislamu ambao tumekerwa sana na Maneno ya Kada wenu Ndugu William Lukuvi.
Ndugu Lukuvi amesema kuwa Serikali ya Muungano
imeing'ang'ania Zanzibar kwa hofu kuwa Zanzibar ikiachwa ijitawale, kwa kuwa
Wazanzibari asilimia 95 ni Waislamu, itatangaza Serikali ya Kiisalamu ambayo
italeta Siasa kali ambazo zitahatarisha amani ya Tanganyika. Tunaomba kujua
hiyo ndiyo sera ya CCM au Serikali yake au chuki za kidini za Lukuvi binafsi?
Jibu la swali hilo kwa Waislamu wa Tanzania
litatusaidia Waislamu kufahamu kama CCM ni adui wa waislamu ili nasi tujue
tunashika njia gani kwa kuwa Uislamu unatufundisha kuchukua tahadhari tena
kubwa sana kwa adui yako hasa anayeichukia dini yako.
Wabillahi taufiq
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
No comments:
Post a Comment