Thursday, 6 February 2014

Re: [wanabidii] WAKULIMA WAFUNGA BARABARA HUKO MVOMELO


 
Inabidi katiba iseme kila mtu akae kwake na kutunza ardhi yake kiendelevu. Juzi tu gazeti la Raia TZ limeeleza mfugaji kumpiga mkuki mkulimamKilwa na kumuua na mwenzake alipokwenda kumgombea wakamfunga mikono nyuma na kumtumbukiza mtoni. Bahati walipomtumbukiza kina kilikuwa kifupi akaweza kutoka na kujifungua kamba. Ukienda Monduli, Loliondo etc na Mwanza, Maswa, Magu, Bunda -wanalima mpunga, mahindi, mihogo etc hawalishii mashambani mwao. Wanaweka na miti ya miba mifugo haiingii. Lakini wakifika nje ya maeneo yao ni kulishia maekari mamia kwa usiku na mchnana na kuwachapa fimbo wakulima. Wamefikia kubaka mpaka wanawake tena wazee eti anafukuza ng'ombe zisile kisha anahonga na kutoroka rumande. Kumbaka kizee mikumi mume akafa kwa shock. Mkoa wa |Morogoro ni bread basket ya nchi sasa ni njaa tupu. Mito ya mkoa na ya iringa imetengeneza wetland nzuri kwa kilimo. Mifugo imejaa mapaka ktk miradi ya irrigation schemes japaneese financed. Wetland za za Ulaya, Zombo etc watu hawalimi wafugaji wamehama vijiji walivyopangiwa wameingia maeneo ya makazi ya wakulima. Njaa inaua na rural prostitution na ujambazi unakua. Misitu ya Mkulazi, Kidunda, Mgeta inayotegemewa na dawasa haina outgrowth ardhi ni sakafu nyeupe. Mifugo inakatiza Mikumi town kama ndege kware au kuku. Bado wanatetewa na wanasiasa walafi na wasomi wabinafsi badala ya idara za mifugo na wasomi hao na wanasiasa kuhakikisha kuwa wafugaji wanabadili ufugaji wa kizamani wa kulimbikiza kwa sifa badala yake wanafuga kisasa sustainably. Mifugo ya kuishi ktk mazingira haya yetu imefanyiwa utafiti na taasisi na vyuo vya mifugo. Madawa yapo, insurance ya mifugo ipo, wakichanga pale walipo wanaweza kuomba msaada Tasaf wakapata bwana na kuchangia. Pia tajiri wa mifugo anaweza kuchimba borehole yake akanyweshea mifugo yake na kuwauzia wenzake maji. Tumelogwa. Lakini mbona hatusikii wafugaji mfano kutoka Monduli, Batabi etc huko north kupigana na Wachaga ambao ni jirani zao. Unapita unaona mahindi yamesimama yanaiva  na mmasai au mmang'ati anapita mbali sana na mifugo. lakini akifika Ruvu, Chalize, Ngerengere, Mvomero, Mbeya, Kilwa, kisarawe, Rufiji, huko Bakora zinaanza kuwaonea wasiojiweza. Kwa Mchaga na mpare anapita kwa adabu!! Morogoro imechoka uonevu huu unaolelewa na wanasiasa. Maana unafika mahala mifugo inakula, bwana kilimo haruhusiwi kufanya assessment eti inawanywa na hakimu mwenewe. Aibu kuwa kulea uzembe wa namba hii. Hata Bwawa la maji ya kunywa lililohifadhiwa na Tasaf likawekewa mabomba ya matoleo ya maji, wao wanaingia kuoga ndani, kuingiza mifugo bila ya kuzingatia sheria ndogongogo za watumia mahi (Water user association) na za kijiji. Isipoangaliwa na kuweza kupima ardhi na kutoa hati miliki8 vijijini, kuachia land iwe public land kila mtu afanye atakavyo-tutauana kila leo. Watu wa ardhi pia waache kupima mabonde ya kilimo kuyafanya maeneo ya kujenga nyumba. Watu wa uwezo wanajaza mchanga, mawe na kujenga nyumba kuzuia kilimo vizee vinakufa njaa. inawezekana kabisa kuwa na cities with farms. Tuache ushamba kuifanya kibaha yote ni majumba kila shamba ni house plot, Bunju, Ruvu, Kitopeni Bagamoyo, Mkuranga etc ni house plots. Pumba tupu watu wa rural and urban planning. Wamesomea wapi? hata study tour za ulaya haziwasaidii? Wanajali tumboni street yao tu!! Shame on you peolpe na wajengao majengo hayo si watu wenye njaa, mnakula nao. Inakera kujitia umasikini penye raslimali za kutosha na kutesana kwa rushwa ya kuruhusu mapigano ya watu wa livelihood tofauti. Kila mtu akae kwao alikozaliwa au kwa kabila lake basi kama hatuwezi kuacha kuonea wengine kwa kwenda ktk mazingira yao na kuwatesa wewe yako kwenu unatumia upendavyo.


On Thursday, 6 February 2014, 15:30, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
Yaelekea hawa wananchi wamekwishachoka na sasa wanasema come what may. Hii ni hatari kubwa


On Thu, Feb 6, 2014 at 1:44 PM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
Wakulima wamefunga barabara huko mvomelo na kusababisha vurugu kubwa , chanzo bado hakijajulikana 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment