Wednesday, 5 February 2014

Re: [wanabidii] Maria: Mume wangu aliongopa mahakamani ndoa yetu ikavunja

Kama katika nchi hii, kuna wanataaluma watakuwa chachu cha mauaji na ukatili, ni mahakimu. Wanapokea rushwa na kutoa hukumu za kipumbavu kabisa.
Nadhani, tunaweza kuwawezesha Tamwa na wao wakamweka mwanasheria ili kumsaidia mama na watoto.
TAMWA TUWEKEENI NO YA KUCHANGIA.
--------------------------------------------
On Wed, 2/5/14, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Maria: Mume wangu aliongopa mahakamani ndoa yetu ikavunja
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, February 5, 2014, 10:40 PM

Kitendo cha huyo bwana kuwa
na mke mwingine ndani ya ndoa nafikiri ni sababu tosha
kuvunja ndoa ila kinacholeta utata ni mlalamikiwa kujifanya
mlalamikaji na kufungua kesi ambayo imehukumiwa haraka sana
kitu kinachoashiria kaharufu ka vijihongo . Ndoa kama hii
haina sababu ya kuendelea kuwepo ila cha msingi haki
itendeke katika kugawana mali walizochuma katika kipindi
chao cha ndoa kikiwemo kiinua mgongo kwa upande wa mwanamke.
Ebu wanasheria tusaidie inakuwaje mahakama itoe uamuzi wa
kugawana watoto? Wana maana ya nani amuhudumie mtoto gani au
ina maana watoto hawa ni wa huyu na wengine ni wa yule.
Tangu lini mtoto akawa na mama bila baba au kuwa na baba
bila mama? Sheria kama hii ipo ni vyema ikaangaliawa upya,
maana inaingilia haki za watoto



2014-02-06 Joachim
Mushi <mushijoa@gmail.com>:

Maria: Mume wangu aliongopa mahakamani ndoa
yetu ikavunja 
[caption id="attachment_42717"
align="aligncenter" width="640"]<a
href="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/Maria-Tarafa-wa-kwanza-kushoto-akiwa-na-watoto-wake-wanne-aliozaa-na-Ndebile-Kazuri-akiwa-amekaa-kwenye-kifusi-cha-sehemu-ya-nyumba-anayokaa-mumewe-ameibomoa-nyumba-hiyo-ili-kumfukuza-eneo-hilo..jpg"><img
src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/Maria-Tarafa-wa-kwanza-kushoto-akiwa-na-watoto-wake-wanne-aliozaa-na-Ndebile-Kazuri-akiwa-amekaa-kwenye-kifusi-cha-sehemu-ya-nyumba-anayokaa-mumewe-ameibomoa-nyumba-hiyo-ili-kumfukuza-eneo-hilo..jpg"
alt="Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto
wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye
kifusi cha sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa
nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo."
width="640" height="424"
class="size-full wp-image-42717" /></a>
Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne
aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye kifusi cha
sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili
kumfukuza eneo hilo.[/caption]

[caption id="attachment_42718"
align="aligncenter" width="584"]<a
href="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/Bw.-Ndebile-Kazuri.jpg"><img
src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/Bw.-Ndebile-Kazuri.jpg"
alt="Bw. Ndebile Kazuri anayedaiwa na aliyekuwa mkewe
kuiongopea mahakama." width="584"
height="480" class="size-full
wp-image-42718" /></a> Bw. Ndebile Kazuri
anayedaiwa na aliyekuwa mkewe kuiongopea
mahakama.[/caption]

<strong>Nkasi,
Rukwa</strong><strong>NOVEMBA</strong>
18, 2013 Mahakama ya mwanzo, Namanyere, Wilaya ya Nkasi
iliamua kuvunja ndoa ya Ndebile Kazuri na Bi. Maria Tarafa
wote wakazi wa Kijiji cha Isale Mji mdogo wa Namanyere
wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa. Ndoa hiyo ambayo hadi mahakama
inaivunja ilikuwa na watoto wanne, yaani watoto wawili
wakiwa na miaka 9 na 7 huku wengine wawili wakiwa na miaka 3
na mwingine mwaka mmoja.

Mume ndiye aliyeenda mahakamani kufungua kesi akiomba
kutengana na mkewe akidai anatabia mbaya hivyo hawezi
kuendelea kuishi naye. Kazuri anaomba mahakama itengue ndoa
hiyo akiwa tayari na mke mwingine ambaye anaishi naye
tofauti na Bi. Tarafa.

Bi. Tarafa anasema shauri hilo lilifunguliwa Oktoba 22,
2013 na Novemba 18 mahakama baada ya kuridhika na sababu
zilizotolewa na mlalamikaji na bila kumpa nafasi ya
kujieleza mlalamikiwa iliamua kuvunja ndoa hiyo. Bi. Tarafa
katika mahojiano na mwandishi wa makala haya alipotembelea
Wilaya ya Nkasi kwa msaada wa Chama cha Wanahabari Wanawake
(TAMWA); anasema sababu zilizotolewa na mumewe mahakamani
kuomba ndoa ivunjwe si za kweli japokuwa mahakama iliridhika
na kuamua kuvunja ndoa yao na kuwagawa watoto.

Anasema chanzo cha mumewe kuamua kuvunja ndoa hiyo ni
pamoja na yeyé kudai mahitaji yake na familia yao kwa
mumewe ambaye kipindi hicho alikuwa tayari amemtelekeza bila
huduma hizo huku akiishi na mwanamke mwingine aliyezaa naye
pia.

"…Hadi anafungua kesi hiyo kuomba ndoa
itenguliwe alikuwa tayari amenitelekeza maana alikuwa hatoi
chochote kwangu licha ya kuwa naishi na watoto wake, alikuwa
hanihudumii hata nikiumwa nilikuwa nikiishi kwa kutegemea
kilimo mimi pamoja na watoto wangu…alinitelekeza
kihuduma tangu Oktoba 2012."

"…Hata mazao ambayo yalipatikana baada ya
mimi kulima na wanangu nayo alikuwa akiyasimamia yeyé na
wakati mwingine kumnufaisha zaidi mke mwenzangu na familia
yake zaidi yangu mimi ambaye ndiye niliteseka
kiuzalishaji," anasema Bi. Tarafa katika
mazungumzo.

Anasema mbali na unyanyasaji huo pia alikuwa akipigwa
sana na mumewe mara kwa mara kwa sababu zisizokuwa na
msingi. "…Kuna wakati nilikuwa mjamzito wa
miezi nane alinipiga hadi nikaenda kulazwa aliniumiza sana
kiuno pamoja na shingo, lakini mbali na kuniumiza kiasi
hicho aligoma kabisa kunipeleka hospital ili niweze
kutibiwa. Walilazimika kuja wazazi wangu ambao walinipeleka
hospitali na kulazwa. Baada ya mimi kulazwa yeyé alikamatwa
na polisi na kufunguliwa mashtaka kutokana na kitendo
alichokifanya," anasema Bi. Tarafa.

[caption id="attachment_42716"
align="aligncenter" width="480"]<a
href="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/wake-Ofisa-Ustawi-wa-Jamii-wa-Halmashauri-ya-Wilaya-ya-Nkasi-Oscar-Mdenye.jpg"><img
src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/02/wake-Ofisa-Ustawi-wa-Jamii-wa-Halmashauri-ya-Wilaya-ya-Nkasi-Oscar-Mdenye.jpg"
alt="Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi, Oscar Mdenye," width="480"
height="510" class="size-full
wp-image-42716" /></a> Ofisa Ustawi wa Jamii
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Oscar
Mdenye,[/caption]

Anabainisha kuwa baada ya kumuomba sana mke wake
aliingiwa na huruma na kufuta kesi ili waende wakayazungumze
kinyumbani na wazee wa pande zote ili kutafuta suluhu, hivyo
aliridhia na kufuta kesi hiyo. Kikao cha wazee kilimuamuru
kulipa gharama na muda kwa wazazi wangu ambao walilazimika
kusafiri kutoka kijijini kwao na kuacha shughuli zao na kuja
kuniuguza mimi zaidi ya wiki moja hadi hali ilipokuwa
nzuri.

Pamoja na hali hiyo mateso kihuduma kwangu yaliendelea
alikuwa hatoi chochote kutoka kwa mkewe mwingine anayeishi
naye kuja kwangu kwa ajili ya wanae. Wakati mwingine
aliwafukuza wanangu kukanyaga kwa mkewe huyo mwingine, licha
ya watoto hao kuwa wakimsaidia kazi nyingine. Anasema mtoto
wangu mmoja ndiye aliyekuwa akichunga ngombe ambazo ambazo
zinainufaisha zaidi familia ya mke mwenzake, lakini wao
hawapati hata maziwa ya ng'ombe wanapokamuliwa.

"Nilivumilia nikachoka siku moja nikamfuata na
kumwambia kama ataendelea kuwatenga wanangu ki-huduma hata
mifugo ambayo wao ndio wachungaji basi nitawazuia kuchunga
ng'ombe hizo maana zinawanufaisha wao pamoja na mke
mwenzangu lakini sio mimi na watoto wangu ambao ndio
wachungaji.

Hapa napo alinipiga sana na kudai kwanini ninawazuia
watoto wangu kuchunga ng'ombe za baba yao, alisema
watoto lazima wachunge maana watakapotaka kuoa ukubwani
watatumia ng'ombe hizo kama mahari hivyo siwezi
kuwazuia…mgogoro uliendelea. Ndipo nilipoamua
kumshtaki kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isale
'A', anasema.

Bi. Tarafa anasema hata siku anaenda kujifungua mtoto
wa nne ambaye ni wa mwisho kuzaa na Kazuri alilazimika
kuwafungia watoto wake ndani usiku na kwenda hospitali
mwenyewe. "…Nilipoanza kuhisi uchungu nilituma
watoto wakamjulishe kuwa hali yangu ni mbaya hivyo naitaji
msaada nipelekwe hospitali, aligoma kabisa kuja, majirani
wakamfuata tena wao akagoma ndipo walipokuja mama na kaka
yangu na kunipeleka wao hadi hospitalini nikajifungua salama
mtoto wake wa nne," anasema.

Baada ya kujifungua manyanyaso yaliendelea alifikia
hatua ya kunitaka mimi na watoto wake niondoke pale kwake na
niende kuishi kwa wazazi wangu eti akidai atakuwa
akinihudumia kulekule. Mimi nilikataa nikamwambia siwezi
kuondoka na mzigo wa watoto na kwenda nao nyumbani
kwetu. 

Anabainisha kuwa Novemba 18, 2013 baada ya mvutano na
yeye kukiri kuwa yupo tayari kuachana na mume huyo iwapo
atapata haki zake na watoto, mahakama ilivunja ndoa hiyo na
kuamuru aondoke na watoto wawili bila kueleza namna
watakavyo pata huduma toka kwa baba yao.

Alisema mahakama iliamuru watoto wa miaka 7 na 9
watabaki kwa baba yao na yeye kuondoka na wawili wenye miaka
miaka chini ya saba. Aliongeza kuwa Mahakama iliamuru apewe
magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo tulilima pamoja na
bati 7.

"…Mume wangu alidanganya kuwa hatuna mali
pale mahakamani, mimi nikaeleza ni uongo kwani tuna
ng'ombe zaidi ya 127, buzi 30, nyumba mbili pale
kijijini Isale pamoja na hekari zaidi ya 70 za
ardhi…hawakunisikiliza pale mahakamani. Ukweli ni
kwamba tunamali hizo ambazo tulichuma tukiwa wote,"
alisema Bi. Tarafa.

Mwandishi wa habari hii amebahatika kupata nakala ya
hukumu ya kesi hiyo, ambayo kweli haikuonesha namna watoto
wanaobaki kwa mama watahudumiwaje na baba yao licha ya
kuamuru kuwa watabaki na mamayao. Hata hivyo
akizungumzia mvutano huo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya
Wilaya ya Nkasi, Ramadhan Rugemalira anasema mama huyo
anahaki ya kufungua kesi nyingine ya madai kuomba mgawanyo
wa mali na matunzo kwa watoto endapo hakuridhika na hukumu
iliyotolewa kwa shauri hilo.

 "…Anachotakiwa kuomba mahakamani kwa
sasa ni mgawanyo wa mali, kwamba katika kesi yao ambayo
mahakama ilivunja kuna mali ambazo mahakama haikuzizungumzia
kabisaa lakini na mimi (mke) ninahaki na mali hizo,
unaona…ataleta ushahidi kama ng'ombe hao wapo
kama kuna ardí na nini…hivyo huyo mwanaume ataitwa
na kesi kusikilizwa," anafafanua Rugemalira.

Hata hivyo, Hakimu Rugemalira anasema huenda mtoa
hukumu wa mwanzo aliteleza kwa kitendo cha kutoainisha namna
watoto wanaobaki kwa mama watalelewa vipi na baba
(kihuduma). Anasema pamoja na hayo bado mama huyo anahaki ya
kufungua madai mengine kudai haki hizo.

Anasema Bi. Tarafa anaweza kufungua kesi ya madai kudai
matunzo ya watoto pamoja na mali ambazo mahakama
haikuzizungumzia kabisha wakati wa kesi ya msingi ya kuvunja
ndoa yao. Anaongeza kuwa au mama huyo anaweza kukata rufaa
mahakama ya wilaya kupinga hukumu ya awali kwamba
hakuridhika na kitendo cha mahakama kumpa watoto bila ya
kueleza namna ya watakavyo pata gharama za matunzo toka kwa
baba.

"…Anaweza kuleta shauri mahakamani
akilalamika kwamba katika ndoa yetu iliyovunjwa kuna mali
ambazo mahakama haikuongelea kabisa, na mali hizi katika
kuzichuma na mimi ninauhusika, basi ataleta ushahidi
mahakamani kuthibitisha uwepo wa mali hizo na walichuma wote
kisha mahakama itamwita huyo mwanaume na kesi kusikilizwa
ikiridhika basi mali hizo zitagawanywa," anasema
hakimu Rugemalira.

Mwandishi wa makala haya alizungumza na Kazuri
aliyekuwa mume wa mama huyo kujua anazungumziaje juu ya mali
ambazo mkewe anazilalamikia, yaani ng'ombe 127, nyumba
2, mbuzi  30 na ardhi hekari 70. Katika majibu yake
anasema mali hizo zinazolalamikiwa alipewa na babayake mzazi
amshikie wakati anaanza maisha hivyo bado ni mali ya
babayake ambaye alidai yupo hadi sasa. 

Pamoja na madai hayo uchunguzi uliofanywa na mwandishi
wa makala haya umebaini baba yake na Kazuri (kwa jina Kazuri
Moshi) ni marehemu na alifariki dunia tangu mwezi Machi 2004
na mali zake kugawiwa kwa watoto wake wote wenye haki ya
kupata akiwemo Kazuri mwenyewe.

Hata hivyo mtalaka wake Kazuri akifafanua zaidi juu ya
mali anazolalamikia; anasema walipewa ng'ombe 65 za
urithi toka kwa baba yake na Kazuri, lakini wamezizalisha
hadi kufikia ng'ombe zaidi ya 127. Aidha anabainisha
licha ya mifugo hiyo wanamiliki mashamba na nyumba mbili
lakini anashangaa mzazi mwenzake anamdhulumu zote.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye, akizungumzia sakata hilo
anakiri kumfikia. Anasema Bi. Tarafa alifika katika ofisi
yake akilalamika kutoridhika na uamuzi wa mahakama.
Alilazimika kutembelea familia hiyo zaidi ya mara moja
Kijijini Isale na kufanya mazungumzo ya kina na pande
zote.

Anasema kwa maoni yake baada ya kuchunguza amegundua
kuna utata juu ya sababu zilizotolewa mahakamani hadi
kuvunjwa ndoa hiyo. Anasema kwa kuzingatia sheria nyingi
kama Sheria ya Mtoto (2009), Sheria ya Ndoa (1971), Sheria
ya Kanuni za Adhabu (1937) na zinginezo; pamoja na mikataba
ya kimataifa iliyoridhiwa na kusainiwa na taifa ni vyema
kila mtu, kwa nafasi yake mzazi/mlezi, mahakama, polisi, na
maofisa Ustawi wa Jamii pamoja na vyombo vingine kuona
Ustawi na maendeleo ya mtoto ni jambo muhimu. 

Anabainisha kuwa; Sheria ya Ndoa (1971) fungu 113 (2),
inaeleza uwezo wa Mahakama kutengua/kubadili amri yake ya
kutengana iwapo itatosheka kwamba amri hiyo ilitokana na
maelezo ya kupotosha au yasiyo na ukweli.

"…Mahakama inaweza kuangalia upya taarifa
ya sababu za kuachana (wizi na kiburi) ambazo Kazuri
aliwasilisha mahakamani kwa kuwa zinaonesha hazina ukweli na
zinahitaji ushahidi na uhuru wa kujitetea. Kwa kufanya hivyo
mahakama itakuwa imempa Tarafa fulsa ya kufungua kesi ya
madai na hivyo kupata mstakabali wa ustawi wa watoto wote
wanne," anasema Mdenye.

Kiongozi huyo wa ustawi wa jamii anasema;
alivyofuatilia kwa kina mzozo huo amebaini  Kazuri
alimpa mimba mtalaka wake akiwa darasa la sita 2003/2004,
hivyo kumpotezea fulsa ya kusoma, lakini leo anamwacha
solemba (mtelekeza na watoto) kirahisi tu bila kukumbuka
makosa yake ya nyuma. 

"Kikubwa zaidi Sheria ya Ndoa (1971), kifungu 114
kinaeleza uwezo wa mahakama kutoa amri ya kugawana mali za
waliooana. Mahakama itazingatia masilahi ya watoto, na
itatazama usawa katika ugawaji. Pia kifungu 136 (1)
kinaeleza uwezo wa Mahakama kuzingatia nasaha za maofisa wa
ustawi na wengineo husika."

Anabainisha kuwa Kazuri hajafanya hivyo badala yake
amebomoa hata nyumba ya vyumba viwili aliyokuwa akiishi
mtalaka wake na watoto na alipoulizwa kwa nini anafanya
ukatili huo alijibu amebomoa ili mkewe na watoto waende
kuishi kwa bibi yao yaani mama mkwe wake.

Kimsingi nashauri sote tuache mawazo mgando kama ya
Kazuri ambaye anazungumza kwa kujiamini kana kwamba ni jambo
jema. Nina mengi ya kusema juu ya mzozo huu ambao Kazuri
anaonekana kukosa utu, lakini sina uwezo wa kupinga amri ya
mahakama. Tuiachie kwa kuwa ndio chombo cha mwisho cha
uamuzi kwa tatizo hili," anasema Mdenye.

<strong>*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa
kushirikiana na TAMWA</strong>
--
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la
Thehabari.com


Mail address:-
mushi@thehabari.com/
jomushi79@yahoo.com/
info@thehabari.com


Mobile:- 0717
030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  

          http://joemushi.blogspot.com




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment