Kwa ndege tunaenda mbali sana .
Wewe kaa pale Ubungo mataa uone SU , STK , zote zinazoingia jioni zina mkaa juu , nyingine nyama , mbogamboga NK
Tumeona meno ya tembo yakikamatwa kwenye magari ya serikali , jeshi la polisi na vyombo vingine hii ni hatari .
Vyombo vya serikali vipigwe marufuku kujihusisha na biashara wale kubeba vitu au mambo binafsi na kama ikitokea vyombo hivyo vikamatwe wanaoendesha au kuongoza washtakiwe .
2013/8/27 Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com>
Naanza kuona umuhimu wa kukagua mizigo ya hawa viongozi wetu!2013/8/26 Sisty Basil <stiba7@yahoo.com>Wabunge wa CCM Zanzibar wameibua zengwe jipya dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba anatumia ndege ya Rais kubebea mkaa, mihogo na ndizi kutoka Pemba kwenda Unguja.Habari zilizopatikana kutoka ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaeleza kuwa, tuhuma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita.Kitendo hicho kinachodaiwa kufanyika mwezi uliopita kimeonekena kuwakera baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo wabunge wa CCM Zanzibar, ambao wakati wa kikao hicho na Rais Dk Shein mwezi uliopita mjini Zanzibar, walilizungumza kwa uchungu na kuomba Rais amuonye Maalim Seif kwa kuigeuza ndege ya Rais kuwa ya mizigo.Anayedaiwa kuibua hoja hiyo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis, ambaye alisema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege hiyo kubebea mkaa, mihogo na mikungu ya ndizi kinadhalilisha Ofisi ya Rais.Katibu wa Wabunge wa CCM Zanzibar, Mbunge wa Magomeni, Mohammed Chombo alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo alikiri wabunge hao kulifikisha suala hilo kwa Rais Shein."Tulimweleza Rais matatizo mengi likiwamo na hilo la Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege ya Serikali kubebea mihogo na mkaa," alisema.Alisema kuwa Rais aliwaambia kuwa ameyapokea malalamiko hayo na kwamba atayafanyia kazi.Chombo alisema kuwa kwa sasa wanamsubiri Rais Shein awaite kuwapa majibu ya matatizo yao.Baadhi ya wabunge wa CCM Zanzibar ambao walizungumza na gazeti hili, walisema kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya mali za umma kwa sababu kuna vyombo vingi vya usafiri vinavyoweza kutumika kusafirishia mizigo hiyo.Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutoka Mamlaka ya Ndege za Serikali, akizungumzia utaratibu wa viongozi wa Serikali kutumia ndege hizo, alisema viongozi wa juu wa Serikali ya Muungano na Zanzibar hukodi ndege zao.Alisema hajawahi kuona ndege kubebea mkaa, hata ndege ya jeshi hajawahi kuona ikibeba mkaa.Hata hivyo, Katibu wa Wabunge wa CUF, Mohammed Habibu Mnyaa, alisema madai hayo ya wabunge wa CCM ni siasa chafu dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kwamba wao wanaamini hawezi kufanya jambo hilo.http://mazingirachanya.blogspot.com/
Africa Holds two fifths (2/5) of the world's Uranium and Gold, three quarters (3/4) of the world's platinum and 90% of the world's diamonds.....the world'd richest continent, Makes you Wonder WHY:-?__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (2) .![]()
__,_._,___
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
No comments:
Post a Comment