Mama Kiwasila
Asante kwa taarifa. Umetupa uwanja wa kujua mema na mabaya
On Jul 20, 2013 3:21 AM, "Hildegarda Kiwasila" <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:
-- --
Waliotolewa Ramsar site Kilombero wetlands wamehamia maeneo mbali mbali. Wanaolima makwao na kupeleka mifugo kwingine nao wanazidi kuzagaa. Pia wakipewa pa kuhamia, hawakai huko wanazagaa kusiko stahili. Kujichangisha kuweka huduma mfano maji ya mifugo wanaouwezo ila hawataki. Kila mmoja kuuza mbuzi mmoja na kuchangia shallow well au borehole au rain harvesting charco dam.
Ukifika Mikumi mjini mifugo imezagaa, mashamba yanalishiwa na wameingia Mikumi National Park, Mweda irrigation system na mabonde ya kilimo ya Mhenda, Ulaya, Zombo. Baadhi ya vijiji walikowekwa nao wanalima extensively na kupeleka mifugo kula maeneo ambayo ni bread basket kwa kilimo-Ihombwe, Madizini, Lumango, Kidogobasi etc- Wanapanda sasa Migomberama mountains kwenda udunghu na Chomwe kupitia Msimba village.
Wameingia Ruvu Basin maeneo ya Kiwangwa, maeneo ya kilimo chwa umwagiliaji cha Ruvu Makurunge (Japanese financed irrigated rice scheme) ugomvi ni huo mpunga umekuwa malisho ya mifugo. Bado hizo vita za Rufiji sio tu Handeni, etc. Handeni wanahama maeneo wanayotakiwa kukaa wanakuja kwa wakulima na kuingiza mifugo ktk bwawa la maji ya kunywa lililogharimiwa na TASAF kwa mamilioni na hakuna maji maeneo hayo ya Magambazi. Huko kuna artisanal mining ya gold na utaona mifugo inakunywa maji yenye mercury ktk vibwawa vya amalgamation of gold.
Wakikaa maeneo ya wachungi waliyopewa na kuchangia kuchimba bwawa la kunywesha kama wakazi wanavyochangia la kunywa kunyengewa na TASAF funds utata usingekuwepo. Huwezi kuchanganya mifuko mingi na makazi ya watu na mashamba. Ukifanya tracer studies per kaya utagundua walikotoka wana ardhi, mifugo na familia. Utagundua pia kuwa baadhi yao ni wachungi under traditional system paid in kind as per livestorck keeping norms.
Ukienda eneo la Morogoro Rural-Ngerengere ukitoka ubena Zomozi kama unataka kuelekea Selous Game Reserve kupitia Maturi, Kwaba, Mkulazi, Makanga to Kidunda kituo cha reli ya Tazara kabla ya kuingia Selous-wamejaa kutoka kilombero.
Maeneo hayo ni ya ukame wanavijiji wanategemea mabonde ya mto, Mkulazi, Mgeta na Ruvu kwa Kilimo cha ufuta, mpunga na mtama, mahindi yanapomea vizuri. Sio ardhi yote inalimika.
Wamejaa pia wasukuma Ngerengere Division wanachaanga miti Mkulazi Forest Reserve kukata. Mbao zakatwa, kuchoma mkaa na kuuza. Maisha yanakuwa rahisi maana huuzi mifugo yako unapata hela unakula. Wasukuma hulima intensively na extensively pia.wakifa kufagia mahala, huhamia kusagia kwingine. Carrying capacity ya Ngerengere imezidiwa sana sana na mifugo iliyoingia. Soon vita itapiganwa na watauana kama ilivyotokea Kilosa. Inapofika kulishia mashamba ya watu walala hoi usiku asubuhi unakuta kweupe kumefagiliwa ni hatari ambapo kwa mfano-msukuma analima kila chembe ya ardhi yake lake zone na kuuza mchele TZ bara, ZNZ, Mombasa-Nairobi lakini mpunga hauwi majani ya kulishia mifugo. Anapoitoa Lake zone ili alime vizuri na kuipeleka makazi vijiji na wilaya nyingine kuongeza wingi awe tajiri (wealth ranking socio-economic criteria) na kulishia mashamba ya wenye shida kama yeye kisha kuwachapa fimbo si utu hata kidogo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Vianzi kijiji cha Chanyumbu, Kata ya Mkulazi, Tarafa ya Ngerengere amepigwa bakora hivi karibuni na mamang'ati. Mtoto wa mfugaji huyo alikutwa na mwenye shamba kitongoji hicho akipurura ufuta shambani ili akauze apate visenti. Mwenyeshamba akamkuta na kumkamata kijana huyo na kumpeleka kwa mwenyekiti wa kitongoji. Mwenyekiti na aliyeibiwa wakampeleka kwa mzazi wake. Kufika kule mzazi alipoambiwa tukio alichofanya kijana wake mdogo huyo ni akawasarandia na kuwakung'uta wote wawili bakora za harakaharaka-mzee aliyeibiwa ufuta na mwanae na m/kiti wa kitongoji cha Vianzi wakala kipigo.
Kesi hizi zinakuwa ngumu maana wafugaji wana hela wanahonga polisi na wahusika wa kusaidia haki kupatikana. Waathirika hukosa pa kukimbilia kupata haki. Na wanawaambia na hao wafugaji kuwa-hamtuwezi hao viongozi wote na polisi ni watu wetu. Ukitaka ukweli zaidi wa kipigo nhiki piga simu kwa Diwani Mh Magari Mpapalika 0785116394 na aliyechapwa bakora ni Mr Ajyae Majimoto na mwanakijiji wa eneo lake la kitongoji cha Vianzi.
Tatizo lingine ni kuwa, wanaweza wakahamia wafugaje wachache hawafiki hata 10, baada ya muda-wakajazana wengine kupitia migongo ya walioanza kuhamia ikawa kama ni watoto/ndugu zao kumbe sivyo. Wengine kuhamia usiku msituni kukaa miezi na baadae kutoka kusogea vitongojini na mjini na kujenga. Inapotokea ugomvi baadhi ya maeneo hawana kituo cha polisi cha karibu budi mtu achukuo bodaboda aende mbali na ni gharama ya 20,000-30,000/= njia mbaya sana sana. Wakiitwa ktk mashauri hawaendi hao maa groups na wasukuma wao kwani wana power ya silaha, ubabe na uwezo wa kuvurumisha bakora kwa mkutu, mluguru na vikabila vigine vya asilia ya eneo ambapo kupigana kibabe kwao haimo ktk mila na desturi.
Kama nchi hii itaendelea na kuwa na vijiji ardhi haipimwi na kumilikisha wananchi kwa hati na kuendelea kuacha watu kuhamahama kuvamia vyanzo vya maji, misitu, kulima na kufuga unsustainably-hatutafika mbali katika kulinda mazingira, kuepuka majanga ya njaa, mapigano na kuchomeana nyumba, kutiana vilema. Magonjwa ya figo, moyo, vilema vya maumbile pia vitakuwa vingi kutokana na kunywa maji ya mabwawa yenye mercury, dip ya mifugo, kinyesi, madawa ya kuua wadudu wa mimea.
Nilitoa taarifa huko nyuma kuwa-Mikumi mama Mzee aliona mifugo inaingia shambani akaenda kuifukuza-akachapwa na kijana wa kimasai (aache ile) kisha akambaka na kumuibia simu. Mama mtu mzima huyo alijitahidi naye akamvuta nonino ambapo ilibidi baada ya siku 3 akatafute matibabu St Kizito Health Centre ambapo mama alilazwa na kutoa taarifa. Daktari akamuona mgonjwa huyo na kumuita mama kumtambua-akakutwa na simu pia akawekwa lupango kusubiri kesi lakini akitoroka (alihonga mipesa). Mume kupata taarifa za mama/mkewe alipata shock akaanguka na kufariki. Loss kubwa hii, vijukuu yatima vinateseka na hakuna fidia na msaada serikalini. Mama hajapata haki hadi leo, ni kilema anashindwa kulima kama zamani maana alilemazwa mikono.imeathirika. Shamba langu la Mikumi-limefagiwa kabisa kipara, ndio njia wanayopitisha mifugo.Proper land use planning, mafunzo ya sheria ya ardhi na kuunda kamati husika za ardhi na mabaraza yake, sheria ndogo ndogo na kuziheshimu ni muhimu. Bongoland-mijini sheria za ujenzi na usafi hazizingatiwi; vijijini sheria za matumizi ardhi hazizingatiwi; utunzaji vyanzo vya maji na misitu maji-NIL; kudhuriana ndio inaonekana utatuzi wa matatizo kumbe sio. Uhuru wa kwenda popote pale na kufanya lolote utakalo uwe mgeni au mwenyeji (Mtangania) lazima upunguzwe ama sivyo TZ itakuwa DRC na Sudan ya pili.
From: Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 19 July 2013, 20:20
Subject: [wanabidii] Wafugaji Kuchomewa Nyumba zao na Serikali ni sawa?
Kwa mujibu wa ITV wafugaji wanaodaiwa kuvamia maeneo mkoani Tanga wamefukuzwa na Kuchomewa nyuma zao. Hapa mimi sielewi kabisaaa. Inakuaje wanachi walioishi kwa miaka mitano na baadaye waambiwe waliingia kinyume cha taratibu? Mbona serikali haikuwakatalia mapema? Sasa watoto wanahangaika na baridi inayoweza kuwasababishia magonjwa.--
Vin
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment