Thursday, 11 July 2013

Re: [wanabidii] Taarifa hii inamlenga nani?

Taarifa hii inatulenga wote maana sheria si za Polisi pekee ila watanzania wote.
Ninatumaini Polisi wataanzia taarifa nyingine ya Chadema kuwa CCM inawapa vijana wa Green Guard mafunzo ya ukakamavu. Hapo watakapowashughulikia wote bila kujali wadhifa wa mtu au taasisi ndipo na sababu za kuviimarisha VIKUNDI HIVYO zitakuwa hazip[o. Polisi onyesha nutrality angalau kuanzia hapa

From: Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, July 11, 2013 9:35 AM
Subject: [wanabidii] Taarifa hii inamlenga nani?

KAULI YA POLISI KUHUSU CHADEMA KUANZISHA KIKUNDI
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
10 Julai, 2013


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.

Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kufuatia kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Jamani nashindwa kulielewa hili jeshi la Polisi. Mbona jamaa zao wana kikundi cha kuwalinda hawaoni? Mbona hawajawachukulia hatua za kisheria? Eti jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote bila kujali wadhifa wake. Subutuuuu!!!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment