Nakuhakikishia kuna watu wa idara wataifuatilia skandali kwa ukaribu na utasikia conclusion.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Hebu umwage hapa nani kanunua, na ni kwa shs ngapi na pia utaratibu gani ulifuatwa na muuzaji ni nani? Tuanzie na skandali hii. Hapa hataweza kujificha popote!
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Kabulo ni tofautoti. Hapa kuna kesi nyingine ambayo sehemu kubwa ya mlima wa pale Kiwira uliuzwa kinyemela. Huo ndo wenye makaa ya mawe, ukimuuliza Dk Kafumu anajua jambo hili vizuri sana.
Mbona ufisadi wa kiwira fedha zilirudi na leo ipo chini ya serikali tena! Ulifanya vizuri na ulikuwa na ushahidi. Mkiwa magazeti matano tu ya namna hii ya kuandika na ushahidi ukazaa matunda ufisadi utamalizika. Tatizo nyie mnajiita mhimili wa nne, wakati pia mnashabikia vyama vya siasa ambavyo ni mhimili tofauti. Independent media na waandishi wake ndipo mtaisaidia nchi hii.
Kwa maandishi na mifano yako, nafurahi ni kama umekubali kuwa ushahidi ukiwekwa hata hadharani, sio mtandaoni tu, kama ulivyofanya marekebisho hufanyika. Kosa ni kama ufisadi huo ulikuwa na jinai ndani yake ili wahusika pia wakapelekwa mahakamani!
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Kazi ya vyombo vya habari huwa ni kweka facts. Ngoja nikupe mfano hai, niliandika series za story kama tatu kuhusu ufisadi wa Kiwira.
Jinsi Yona alivyojimilikisha mgodi wa Kabulo na kusaini kibali cha kumiliki mgodi huo siku moja kabla ya JK kuapishwa kuingia Ikulu. Kila kitu kiko wazi na documents zote.
A well balanced story ambayo hata watyhumiwa walipata nafasi ya kujieleza vizuri, ninapozungumza leo ni miezi minne imepita, ulitakaje? Niwapelekee gazeti wahusika ili waone kuwa ni kosa?
Kaka kwa suala la rushwa CCM hawako tayari kushughulikia mtu. Suala rada mpaka leo Takukuru wanasema uchunguzi umekamilika, DPP anasema bado, wanatuchezea tu wanadhani hatujui mchezo wao?
Kuwa na taasisi imara ni uamuzi tu, kama CCM ingekuwa kweli inatawala basi hilo lisingekuwa mjadala leo. Linhwkuwa limefanyika siku nyingi badala ya JK kusimama kulalamika wakati yeye ni Mkuu wa nchi na kiongozi mkuu wa CCM.
Waliovuliwa gamba si kwasababu walishindwa kazi, wameponzwa na kiherehere cha kusema ovyo kuhusu rushwa. Kusema ukweli kumewaponza, CCM hawataki ukweli hasa kuhusu rushwa.
Kwani Tony wewe hili hulifahamu? Jana ulisema EL ana wafuasi 32 tu NEC but siyo kweli kwani kura walizopata wafuasi wake kwenye uchaguzi wa wajumbe 10 wa NEC ni za kishindo. Ile orodha ya washindi ilitoka siku 3 kabla ya uchaguzi.
Serukamba alitaja majina ya watu 10 ya washindi wa nafasi hizo na kwa taarifa yako wote waliotajwa walipita isipokuwa mmoja tu, Asumpta Mshama. Jina ambalo Serukamba halikuwa kwenye orodha yake ni la B. Membe.
Sasa hao ndio wenye chama, kama wana uwezo wa kutabiri matokeo kwa asilimia 90 na yakawa hivyo huwezi kuwadharau. Anyway, mimi nasubiri miujiza ya akina Mangula, ila kwa jinsi CCM kilivyo sioni kikifanikiwa.
Mbona unaji-contradict? Kumbe kuvuana gamba kumeanza, na wamewavua hao baada ya kushindwa kuwavua gamba wahalifu?
Haya huyo Chadema atatumia njia ipi kuwaadabisha wahalifu bila ushahidi? Atawapiga risasi kutokana na tuhuma za mitaani?
Mfano wako wa Kenya sio kweli bila kueleza sababu kamili! Serikali zinazoundwa kutokana na vyama zaidi ya kimoja zina uwajibikaji mkubwa zaidi. Tuhuma Kenya huanzia bungeni kwa sababu kuna checks and balances ndani ya bunge. Uchunguzi unafanywa na vyombo vilivyo huru (havijateuliwa na serikali), vinawajibika kwa bunge na sio serikali.
Hapa tutafaulu ikiwa katiba utabadilika na kuleta mfumo wenye tija zaidi. Swali ni kama hili litatokea, maana juzi umeona bungeni tuhuma dhidi yao walivyoteteana.
Uliona wapi waliohojiwa na tume ya bunge ni watuhumiwa peke yake na katibu mkuu wa nishati tu. Utapata jibu sahihi kihivyo kweli? Judicial or quasi-judicial probe teams ndizo pekee zinakuwa na uwezo wa kuchunguza na ndizo Kenya wanazitumia sana siku hizi.
Neville, sawa kuwaandika jamaa mafisadi kwenye magazeti au redio au kuwatuhumu waziwazi ni kazi ngumu kwavile hauna ushahidi. Mtandaoni ni rahisi zaidi lakini napo uwe basi na ushahidi wa kuwezesha kuridhisha na hivyo kufanya vyombo husika vione aibu na kufufuatilia.
Sasa waTz tumebakia na maneno ya vijiweni tu na hakuna hata gazeti lenye uwezo wa kuja na uchunguzi wenye mashiko ya ushahidi. Kama mnaogopa nanyi mnabakia na uzushi tu mnataka nchi isaidikaje?
Uzushi na malalamiko peke yake hayasaidii. Tafuteni ushahidi, mwaga hapa mtandaoni hata kwa kutumia psudo-names, lakini ushahidi wa maana. Usalama na vyombo vingi wanasoma mitandao yote kila saa na hivyo itasaidia (authentic whistle-blowing!)
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Kamwe hatutaupata. Hatutaupata kwa sababu katika nchi yetu tuko chini viwango vya Kiafrika.
Jirani zetu Kenya wanaweza kusikia jambo kuhusu rushwa wakachukua hatua kesho yake, wakachunguza hata kama ni Waziri na wakatoa taarifa kwa umma.
Hapa kwetu ukiandika kuhusu tuhuma jamaa wanasimama kwamba eti kama una ushahidi tuletee. Hata ile level ya taasisi kuwajibisha watuhumiwa kwa sababu za kimaadili haipo.
Ndo maana Mukama, Chiligati na Msekwa wamevuliwa gamba kwa sababu tu walijaribu kuwagusa watuhumiwa wasiogusika. Ukisema rushwa waziwazi ndani ya CCM unageuka kuwa adui wa wengi.
Jana nilisema kwamba kwamba sijui akina Mangula wataanzia wapi, maana utulivu unaodaiwa kuwa upo ndani ya CCM ni kutokana na watuhumiwa wa ufisadi kuachiwa watambe katika uchaguzi wa ndani ya chama.
Siku wakiguswa tu, mtaniambia. Katika mazingira kama hayo, hatuwezi kusonga mbele. Rushwa na ufisadi ndani ya CCM vimetaasisiwa (instituted corruption) na ndiyo maana maadui wa chama ni wale wanaopinga rushwa.
Wachapa kazi ndani ya CCM hawatakiwi, ndo maana watu kama Dk Magufuli, Dk Mwakyembe na wengine wenye kasi kama yao, hawapendwi na wengine utendaji wao umewagharimu afya zao. Tony Diallo akiwa Maliasili na Utalii alimgusa Severe akang'olewa.
Kumbe CS Luhanjo aliyekuwa akimlinda Jairo na madudu yake, aliacha mizizi maliasili wakati akiwa KM chini ya Zakia Meghji. Katika mazingira haya, tunawaaminije hawa wapya katika sekretarieti ya CCM?
Unadandia treni jamani! Ngoja tuone mwelekeo. Kwani trafiki hao wataacha chadema wakitawala? Mwenye kosa ni chama ama serikali chini ya JK? Je, akija mtu kama Slaa lakini upande wa ccm utaacha ubishi au wewe kosa ni rangi tu?
Kimbuka serikali za kiafrica institutional governance hakuna, ipo individual head of state effort na jinsi atakavyo washughulikia wakosaji chini ya serikali yake. Kwahiyo, vyama ni vyombo vya kupitia tu, inategemea ujasiri wa mkuu wa kaya, period!
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Hicho kigezo cha kusema "lete ushahidi" ndicho kilichoifikisha CCM hapo ilipo na kuitwa kichaka cha wanyang`anyi. ikimanisha kwamba , ujambazi wote unaosemwa juu ya kiongozi wa CCM anaeusema ataulizwa lete ushahidi. sasa ingekua kuna uzalendo kwamab ukiletwa ushahidi utafanyiwa kazi , labada ungeletwa . lakini tofauti ni kwamba atakaeleta ushahidi , atasakamwa gizani ( tumeshuhudia hayo). Mfano mdogo ni ushahidi uliotolewa katika sakata la Richmond. lakini hao takukuru unaodai wapelekewe walisafisha wakasema hakukua na kosa.
hivi ndugu tony sema tu kama mtanzania halisi unaepita mtaani au hat unaendesha gari, hujawahi ona rushwa ya wazi kabisa inayofaanywa na baadhi ya askari wa usalam Traffic??
hivi TAKUKURU hawaoni kabisa hayo tunayoona sisi?? kweli kabisa toka moyoni mwako??
Au wataka kutuambiwa hayaa yote yasemwayo kuhusu Ufisadi wa Baadhi ya viongozi ni uongoo?? tuache unafiki na sio eti kwakua amechaguliwa kinana kua Katibu Mkuu. basii kabala hata hajafanya chochote CCM imeshakua Safi ?? du kwe;li mmeona watanzania ni wajinga na hawatfakari..... endeleeni
Ernest
Hiv
Subject: Re: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
From: tony_uk45@yahoo.co.uk
Date: Sun, 25 Nov 2012 07:02:20 +0000
Langai Mlima wa moto!
Hilo nalo neno, na kweli wananchi wanaudhika sana. Lakini pia kwanini msiwe mnawasema hapa: mfano badala ya kuhisia tu ana magari 600, kwanini usilete orodha ya hayo malori (Reg number) na jina la usajiri na kujua jina hilo ni la mtoto au ndugu yake?
Pia mafisadi, vizuri mfano hapo arusha majengo plot nr na hati kama unaifahamu itasaidia. Takukuru nayo sasa inajipanga kupokea taarifa kama hizi maana hisia tu hazitasaidia. Kuna watu siku moja watasema Mbowe ana dola milioni 50 kaweka Uswiss bila kuwa na details haisaidii sana.
Watanzania ni woga wa kutoa taarifa sahihi lakini wepesi kudakia maneno. Sasa kwanini hata ushupavu huu wa udaku tusiutumie kutaja mali za mafisadi hapa ukiwa na ushahidi? Mitandao inaweza kutumika productively ikasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza ufisadi nchini; iwe kwa ccm au chadema au Cuf.
Umbeya na malalamiko tu yasiyo na takwimu sahihi haitasaidia hata tone na tatizo litaendelea hata kwa serikali zisizo za ccm. Watu ni walewale; watakuwa wamebadili rangi, matendo hayohayo.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
| Katika mambo ambayo Katibu Mkuu wa chama tawala CCM ndugu Abdulrahaman Kinana anajidanganya nayo ni kutegemea kuwa ataweza kuleta mabadiliko Tanzania bila kuwatoa mhanga Mafisadi na watu waliojilimbikizia mali wakiwa madarakani. Kinachofanya watu waichukie CCM sio kitu kingine zaidi ya Viongozi walioko madarakani kuibia Watanbzania na kujilimbikizia mali.
Serekali ya CCM haitaweza kabisa kuleta imani kwa Watanzania bila kurudisha mali walizoiba na kufuta mikataba mibovu yote ya wawekezaji inayolifilisi Taifa. CHADEMA itaendelea kupeta na wakizubaa watajikuta wako nje ya utawala na mali zao zote kutaifishwa. CCM wakati ni huu wa kurudisha kila mlichokwapua. Sasa hivi tusiwadanganye Watanzania kwa kuwa kila linalofanyika Watanzania wanaliona. Mtoto wa Rais anamiliki biashara za kuchimba madini, kusafirisha mafuta, kusafirisha mizigo huku akiwa na malori zaidi ya 600 fedha hizo amezipata wapi?.
Mawaziri mbali mbali na viongozi wa ngazi za juu wa CCM na Serekali yake wanajihusisha na biashara. Chama kinaua viwanda kikidai hakitaki kujihusisha na biashara lakini viongozi wake wote ni Wafanya biashara. Kama Serekali imeviua viwanda vyote na kunyima Watanzania ajira kwa kisingizio cha kutokutaka kufanya biashara wao kama viongozi wanafanya biashara za kazi gani?.
CHADEMA tunaomba muikomboe Tanzania kabla ya kufilisika, na pingeni majeshi ya Tanzania kupelekwa Congo. Wale waasi wanapinga matumizi mabaya ya rasilimali hivyo hawana tofauti na nyie CHADEMA. Hakuna kumsaidia kabila anachezea mali za Wakongo kama CCM. Tanzania tuna matatizo makubwa ya rushwa, umasikini, uongozi mbobu, kupanda kwa maisha kwa nini tumsaidie mtu anayechezea rasilimali za nchi kama Kabila. CCM inataka kutoletee mambomu Tanzania.
CHEDEMA piteni kila mahali kuhakikisha mnashinda uchaguzi Mwaka 2015. CCM ni usanii tu hakuna jipya. Mwisho kila Mtanzania anayeitakia mema Tanzania ajiulize ni kwa nini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hajawahi katika maisha yake kuvaa mavazi ya CCM. Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anaona mbali. Alijua CCM itamsaliti kwa kuzika juhudi zake zote za kumkomboa Mtanzania. CHADEMA kazi kwenu kuikomboa nchi, Kinana akitaka Watanzania tumuamini kuwa sio Kondoo aliyevaa ngozi ya chui awafunge kwanza wezi wa mali za umma. Mkereketwa Lengai Ole Letipipi |
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment