Unadandia treni jamani! Ngoja tuone mwelekeo. Kwani trafiki hao wataacha chadema wakitawala? Mwenye kosa ni chama ama serikali chini ya JK? Je, akija mtu kama Slaa lakini upande wa ccm utaacha ubishi au wewe kosa ni rangi tu?
Kimbuka serikali za kiafrica institutional governance hakuna, ipo individual head of state effort na jinsi atakavyo washughulikia wakosaji chini ya serikali yake. Kwahiyo, vyama ni vyombo vya kupitia tu, inategemea ujasiri wa mkuu wa kaya, period!
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Hicho kigezo cha kusema "lete ushahidi" ndicho kilichoifikisha CCM hapo ilipo na kuitwa kichaka cha wanyang`anyi. ikimanisha kwamba , ujambazi wote unaosemwa juu ya kiongozi wa CCM anaeusema ataulizwa lete ushahidi. sasa ingekua kuna uzalendo kwamab ukiletwa ushahidi utafanyiwa kazi , labada ungeletwa . lakini tofauti ni kwamba atakaeleta ushahidi , atasakamwa gizani ( tumeshuhudia hayo). Mfano mdogo ni ushahidi uliotolewa katika sakata la Richmond. lakini hao takukuru unaodai wapelekewe walisafisha wakasema hakukua na kosa.
hivi ndugu tony sema tu kama mtanzania halisi unaepita mtaani au hat unaendesha gari, hujawahi ona rushwa ya wazi kabisa inayofaanywa na baadhi ya askari wa usalam Traffic??
hivi TAKUKURU hawaoni kabisa hayo tunayoona sisi?? kweli kabisa toka moyoni mwako??
Au wataka kutuambiwa hayaa yote yasemwayo kuhusu Ufisadi wa Baadhi ya viongozi ni uongoo?? tuache unafiki na sio eti kwakua amechaguliwa kinana kua Katibu Mkuu. basii kabala hata hajafanya chochote CCM imeshakua Safi ?? du kwe;li mmeona watanzania ni wajinga na hawatfakari..... endeleeni
Ernest
Hiv
Subject: Re: [wanabidii] RE: KINANA ANAJIDANGANYA KUWAKOMBOA WATANZANIA
To: wanabidii@googlegroups.com
From: tony_uk45@yahoo.co.uk
Date: Sun, 25 Nov 2012 07:02:20 +0000
Langai Mlima wa moto!
Hilo nalo neno, na kweli wananchi wanaudhika sana. Lakini pia kwanini msiwe mnawasema hapa: mfano badala ya kuhisia tu ana magari 600, kwanini usilete orodha ya hayo malori (Reg number) na jina la usajiri na kujua jina hilo ni la mtoto au ndugu yake?
Pia mafisadi, vizuri mfano hapo arusha majengo plot nr na hati kama unaifahamu itasaidia. Takukuru nayo sasa inajipanga kupokea taarifa kama hizi maana hisia tu hazitasaidia. Kuna watu siku moja watasema Mbowe ana dola milioni 50 kaweka Uswiss bila kuwa na details haisaidii sana.
Watanzania ni woga wa kutoa taarifa sahihi lakini wepesi kudakia maneno. Sasa kwanini hata ushupavu huu wa udaku tusiutumie kutaja mali za mafisadi hapa ukiwa na ushahidi? Mitandao inaweza kutumika productively ikasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza ufisadi nchini; iwe kwa ccm au chadema au Cuf.
Umbeya na malalamiko tu yasiyo na takwimu sahihi haitasaidia hata tone na tatizo litaendelea hata kwa serikali zisizo za ccm. Watu ni walewale; watakuwa wamebadili rangi, matendo hayohayo.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
| Katika mambo ambayo Katibu Mkuu wa chama tawala CCM ndugu Abdulrahaman Kinana anajidanganya nayo ni kutegemea kuwa ataweza kuleta mabadiliko Tanzania bila kuwatoa mhanga Mafisadi na watu waliojilimbikizia mali wakiwa madarakani. Kinachofanya watu waichukie CCM sio kitu kingine zaidi ya Viongozi walioko madarakani kuibia Watanbzania na kujilimbikizia mali.
Serekali ya CCM haitaweza kabisa kuleta imani kwa Watanzania bila kurudisha mali walizoiba na kufuta mikataba mibovu yote ya wawekezaji inayolifilisi Taifa. CHADEMA itaendelea kupeta na wakizubaa watajikuta wako nje ya utawala na mali zao zote kutaifishwa. CCM wakati ni huu wa kurudisha kila mlichokwapua. Sasa hivi tusiwadanganye Watanzania kwa kuwa kila linalofanyika Watanzania wanaliona. Mtoto wa Rais anamiliki biashara za kuchimba madini, kusafirisha mafuta, kusafirisha mizigo huku akiwa na malori zaidi ya 600 fedha hizo amezipata wapi?.
Mawaziri mbali mbali na viongozi wa ngazi za juu wa CCM na Serekali yake wanajihusisha na biashara. Chama kinaua viwanda kikidai hakitaki kujihusisha na biashara lakini viongozi wake wote ni Wafanya biashara. Kama Serekali imeviua viwanda vyote na kunyima Watanzania ajira kwa kisingizio cha kutokutaka kufanya biashara wao kama viongozi wanafanya biashara za kazi gani?.
CHADEMA tunaomba muikomboe Tanzania kabla ya kufilisika, na pingeni majeshi ya Tanzania kupelekwa Congo. Wale waasi wanapinga matumizi mabaya ya rasilimali hivyo hawana tofauti na nyie CHADEMA. Hakuna kumsaidia kabila anachezea mali za Wakongo kama CCM. Tanzania tuna matatizo makubwa ya rushwa, umasikini, uongozi mbobu, kupanda kwa maisha kwa nini tumsaidie mtu anayechezea rasilimali za nchi kama Kabila. CCM inataka kutoletee mambomu Tanzania.
CHEDEMA piteni kila mahali kuhakikisha mnashinda uchaguzi Mwaka 2015. CCM ni usanii tu hakuna jipya. Mwisho kila Mtanzania anayeitakia mema Tanzania ajiulize ni kwa nini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hajawahi katika maisha yake kuvaa mavazi ya CCM. Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anaona mbali. Alijua CCM itamsaliti kwa kuzika juhudi zake zote za kumkomboa Mtanzania. CHADEMA kazi kwenu kuikomboa nchi, Kinana akitaka Watanzania tumuamini kuwa sio Kondoo aliyevaa ngozi ya chui awafunge kwanza wezi wa mali za umma. Mkereketwa Lengai Ole Letipipi |
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment