Yona Pendekezo lako ni zuri sana na lingeweza kuutatua mgogoro huu. Lakini sijaelewa (labda) mimi na naona tofauti kubwa kati ya mgogoro huu na mifano uliyotoa. Ziwa Victoria na Tanganyika nchi majirani wanakubaliana juu ya mipaka ya nchi zao kwanza na huu ni mtaji mkubwa ndipo wanaunda hizo mamlaka. mfano inajulikana Tanzania inamiliki eneo kubwa la ziwa Victoria. Kwa mto Nile vile vile. Unaanzia Rwanda unapita Tanzania Uganda Sudani etc. Kwa upande wa Ziwa Nyasa: Malawi wanadai ni lao lote. Wana haja gani kuunda Mamlaka ya kuendeleza ziwa hilo na Tanzania wakati Tanzania haina umiliki wowote wa ziwa hilo? Tanzania inadai nusu ni mali yake. Ili kuunda mamlaka ya kuendeleza ziwa hilo lazima kwanza ubishi huu uishe ama kwa mazungumzo ama kwa kuchapana kidogo au kikubwa ndipo kuheshimiana kuje na tuweze kuamua ustawi wa ziwa hilo. Mimi ningependa mgogoro huu ukaisha sasa kwa kutumia njia yoyote. Na yoyote ni kati ya hizi mbili zilizo mbele yetu. Nakumbuka wakati tuko vitani na Uganda Afrika ya Kusini iliwahi kuisaidia Malawi kutaka kumaliza mgogoro huu kijeshi. Ni kama jeshi letu la ulinzi wa anga lilijibu bila 'adabu' wakanywea. Africa ya Kusini walidhani Tanzania kuwa na vita sehemu mbili Uganda na Malawi tusingemudu (nilisikia hivyo). Na tanzania ikadhibitisha kuwa kuwa na vita uganda hakujadhoofisha ulinzi mipaka mingine. Kama wakati wa Nyerere na Mkapa diplomasia ilishindwa tunahitaji kuamua kiume kwamba miaka ijayo diplomasia itashinda au tuwawekee watoto wetu mgogoro. Vinginevyo ni vinginevyo. Binafisi sipendi vita. Na vita ni njia mojawapo ya kuzuia vita. Eneo hili la africa hakukuwa na bwege lolote ambalo lingeweza kuichokoza Tanzania baada ya vita ya Amini. Sasa yapo. Moja ni hilo. Lisaidieni na majirani watakumbuka. --- On Sun, 8/5/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
No comments:
Post a Comment