Ndugu zangu
Imetokea tabia na utamaduni wa watanzania kushiriki kuuza ardhi za watanzania wenzao hovyo na kiholela bila kufuata taratibu maalumu hata pale wanapofuata taratibu basi wanatumia hongo ili kuhakikisha maslahi yao yanatekelezwa yale ya kuuza ardhi hovyo kwa kiwango kikubwa .
Nimetembelea maeneo ya bagamoyo na msata siku chache zilizopita nimeona halikubadilika sana kwa maeneo mengi kuuzwa kwa watu wasioeleweka baada ya barabara hiyo kuanza kukamilika kwa kiwango kikubwa , sio bagamoyo tu , sehemu nyingi zinazojengwa barabara na miundombinu mengine ardhi inauzwa kwa kiwango kikubwa bila ofisi za vijiji kuwa na taarifa za uuzwaji wa ardhi hizo .
Huko tunapoenda watoto wetu wanaweza kukosa viwanjya vya kuchezea , kukosa viwanja vya kujenga shule na zahanati au hata sehemu za kufanya huduma nyingine za kijamii kama tutaendelea kuuzwaji huu wa ardhi kiholela .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment