Tuesday, 24 July 2012

[wanabidii] URASIMU UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA URAIA

 
Uandikishaji Kwa ajili ya vitambulisho vya taifa vimegeuka kuwa mradi kwa wanaohusika katika serikali za mitaa.
Mfano serikali ya mtaa ya Mlalakuwa Mwenge wanaurasimu sana mpaka mtu kujiandikisha wanzungusha sana mara kalete barua ya Mjumbe wa shina, ukifika kwa mjumbe naye anataka kitu kidogo ili akugongee barua mhuri.
Ukirudi na barua na Kivuli cha utambulisho mara ooh subiri tuna mkutano, watu kibao wanajazana pale .
kinachouzi zaidi kuna bwana moja anachukua fedha za watu na kuwajazia form huyo bwana Mrefu Mweusi Mnene.
Nimeshuhudia watu waliokuja bila hizo barua na wakutoka mbali na sio wakazi wa Mlalakuwa anapokea fedha na kuwajazia form.
Naomba wahusika wachunguze jambo hili wanasababisha usumbufu wa raia wakati tuliambiwa zoezi hili ni bure.

0 comments:

Post a Comment