Monday, 23 July 2012

[wanabidii] Re: WAFANYAKAZI SECTOR BINAFSI

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, July 23, 2012 6:40:28 AM GMT-0700
Subject: [wanabidii] Re: WAFANYAKAZI SECTOR BINAFSI

Na hivyo vitambulisho vya taifa utaforge vipi umri wako ? vipi kuhusu
taarifa zako nyingine ulizojaza wakati wa kusajili SIMCARD yako ,
akaunti za benki na sehemu nyingine hizi zote utaweza kuforge ?

On Jul 23, 4:27 pm, Dismas Anthony <mba20...@gmail.com> wrote:
> Hivi Karibuni tumeshuudua wimbi la vijana kufanya forgery ya kupunguza
> umri, sasa kwa hili la kusubiri 55-60 nadhani wupepo utageuka watu
> wataforge kuongeza umri ili 55 ifike haraka na kupata kiinua mgongo.
>
> 2012/7/23 Wanabidii Mabadiliko <wanabidiimabadil...@yahoo.com>
>
>
>
>
>
>
>
> > Kweli wameamua tuwe wezi
>
> > Ona hiyo CPI
>
> > NSSF yaelekea kufilisika
> > Wanajamvi heshima mbele,
> > NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa
> > [waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida
> > waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa mwezi
> > tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF inawataka
> > waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi] kupeleka
> > michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita ili
> > kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la
> > wafanyakazi nchini.
> > Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali
> > imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wake
> > baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha za
> > kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli
> > nyingine muhimu.
> > Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama
> > wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao yao
> > hadi wafikishe umri wa kustaafu.Mkakati utasaidia kukabilia na upungufu
> > mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa na serekali
> > hazitarajiwi kurejeshwa.
>
> > *Cag: Nssf hatarini kufilisika
> > Ofisi ya CAG ilisha toa report juu ya ili swala... na tahadhari juu ya
> > kufilisika kwa NSSF.*
>
> > *Na Reginald Miruko - Imechapwa 18 April 2012*
> > *MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na
> > kupoteza fedha za wanachama wake.*
> > *Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu,
> > mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali.*
> > *Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
> > (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya
> > jamii, ziko hatarini kupotea.*
> > *Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni
> > Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa
> > Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na
> > Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).*
> > *Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo
> > hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu
> > cha Dodoma (UDOM).*
> > *Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko
> > iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.*
> > *Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9
> > bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na
> > riba yake hazijarejeshwa.*
> > *Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo,
> > iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya
> > udhamini ya mwaka 1974.*
> > *"Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko
> > hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha
> > uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi," anasema na kuongeza:*
> > *"Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata
> > udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji
> > ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo."*
> > *Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa
> > alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya
> > .
> > Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa
> > serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi
> > ya kibiashara.*
> > *"Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni
> > pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa
> > wala kupoteza fedha za wateja," amesema Chiume.*
> > *Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, "Ukubwa wa
> > kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa
> > serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko
> > hii."*
> > *Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa
> > mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni
> > hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.*
> > *Akifafanua suala la fedha kwenye mkataba kutofautiana na fedha
> > zilizotolewa, Chiume alisema mkataba ulitakiwa kuwa mmoja ambao ulisainiwa
> > wakati wa awamu ya kwanza.*
> > *Chiume alisema kwa awamu ya pili, kilichotakiwa ni kusaini addendum
> > (makubaliano ya nyongeza), ambayo "yako mbioni kukamilika."*
> > *Utouh anaripoti, "Majengo kwa ajili ya awamu ya kwanza yalikamilika na
> > kuwekwa katika matumizi mwezi Septemba 2008. Mpaka wakati wa ukaguzi
> > 2010/2011, mfuko ulikuwa haujafanikiwa kukusanya malipo ya pango kutoka
> > serikalini.*
> > *Kwa msingi huo, hadi sasa limbikizo la riba limefika thamani ya Sh. 14
> > bilioni," anasema Utouh.*
> > *Mkopo huo ulitolewa kwa utaratibu wa kubuni, kujenga, kumiliki na
> > kuhamisha ambapo mfuko ungepokea kodi iliyokokotolewa kwa riba ya asilimia
> > 15 kwa kipindi cha miaka kumi.*
> > *Vilevile CAG amebaini kuwa majengo yaliyojengwa kwa mkopo huo, hayako
> > kwenye vitabu vya UDOM wala katika vitabu vya NSSF, kutokana na uelewa
> > tofauti uliopo kati ya pande mbili zinazohusika.*
> > *Kuna mikanganyiko katika uelewa kwa serikali na mifuko ya hifadhi,
> > ameeleza CAG. Wakati mifuko inasema fedha zilizotumika kujenga majengo hayo
> > zilikuwa mikopo kwa serikali, yenyewe serikali inadai fedha hizo ni
> > uwekezaji wa kawaida wa mifuko hiyo.*
> > *Mbali na UDOM, serikali pia haijalipa jumla ya Sh. 19.77 bilioni
> > zilizotumika katika ujenzi wa ukumbi wa bunge, ambazo hazilipwi kulingana
> > na makubaliano. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa inadai Sh. 8.96
> > bilioni, PPF (Sh. 7.9 na LAPF Sh. 2.91.*
> > *Pia upo mkopo mwingine wa NSSF wa Sh. 5.33 bilioni na riba ya asilimia
> > 15 kwa miaka kumi, uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa "taasisi ya serikali
> > ya kiusalama" mwaka 2007.*
> > *Mfuko mwingine uliowekeza katika mradi huo ni PSPF uliotoa Sh. 6.4
> > bilioni.*
> > *Kwa mujibu wa ripoti hiyo, NSSF kwa udhamini wa serikali ilikopesha
> > taasisi kwa shughuli mbalimbali.*
> > *Kwa mfano, ujenzi wa nyumba za polisi kwa Sh. 20 bilioni na Sh. 12. 9
> > bilioni kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya
> > ujenzi wa Machinga Complex, Ilala.*
> > *"Hadi sasa hakuna malipo ya riba wala sehemu ya mkopo hiyo yaliyofanywa.
> > Hii ni kinyume cha mkataba," inasema sehemu ya ripoti ya CAG.*
> > *Kwa upande wa Machinga Complex, hadi tarehe 30 Juni 2011, mkopo na riba
> > yake ulikuwa umefikia Sh. 15.3 bilioni.*
> > *Ripoti ya CAG imeainisha pia mikopo mingine ambayo hailipwi kulingana na
> > mikataba ya mifuko hiyo, bila ya kutaja viwango vyake.*
> > *Mikopo hiyo ni iliyotolewa kwa Continental Venture (T) Limited, Meditech
> > Industrial Co. Ltd, General Tyre (GT), Kiwanda cha Sukari Kagera, Bodi ya
> > Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani
> > Mbeya.*
> > *Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio amesema hajaona
> > ripoti ya CAG na yuko safarini Tanga.*
> > *Hata hivyo amedokeza kuwa hivi karibuni walikaa na CAG kujadili suala
> > hilo na kubaini makosa ya kifundi katika uhasibu baina ya mifuko na
> > serikali katika ujenzi wa UDOM; hivyo CAG kuahidi kuyashughulikia kwa
> > upande wa serikali.*
> > *Alipoulizwa ni makosa yapi hayo, Erio alimtaka mwandishi awasiliane na
> > kaimu wake, Stephen Alfred ambaye ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano. Hadi
> > tunakwenda mitamboni, Alfred hakupatikana. Last edited by Straight; Today
> > at 13:06. *
> > **
> > **
> > Date: 2012/7/23
> > Subject: CHADEMA, CUF, NCCR, TLP tujue msimamo wenu kwenye hili!
> > To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, wanabidii <
> > wanabidii@googlegroups.com>
> > Wapendwa,
>
> > Jahazi la wafanyakazi wa sekta binafsi linapitia katika machafuko makubwa
> > kabisa ya bahari yaliyotokana na mabadiliko ya "kanuni" zilizokuwa
> > zinawezesha wafanyakazi kuchukua mafo yao baada ya kuachishwa au kuacha
> > kazi kw hiari. Neno kanuni kama nilivyolitumia linaweza lisiwe limebeba
> > maana yake halisi kwa kuwa tangu mwanzo utoaji huu wa mafao kwa wafanyakazi
> > mara tu wanapoacha kazi haukuwa ni wa kisheria! Yes, haukuwa wa kisheria
> > kwa maana ya kupingana na sheria ya uanzishwaji wa mifuko  ya jamii!
>
> > Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa utaratibu huo wa kuchukua mafao yao mara tu
> > baada ya kuacha au kuachishwa kazi ulitokana na maelekezo au busara za rais
> > wa awamu ya 3 mzee Mkapa kutokana na hali halisi ya nchi yetu ilivyokuwa
> > kwa wakati huo na ninamini imeendelea kuwa hivyo ever since. Yeyote mwenye
> > taarifa zinazopingana na hizi na aziweke hapa sasa au akae na ukimya wake
> > milele!
>
> > Siku chache zilizopita mamlaka ya kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii (
> > MAKUMIHIJA) au kwa ufupisho wake wa kiingereza SSRA, ilitoa tamko la
> > kuharamisha muendelezo wa utaratibu wa wafanyakazi kujitwalia mafao yao
> > hayo kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa kutambua madhara ya uharamishaji huo
> > kwa wafanyakazi na familia zao na kwa kutambua kuwa asilimia kubwa ya
> > wafanyakazi hapa Tanzania ni wale walio kwenye sekta binafsi na ile isiyo
> > rasmi ningependa kufahamu misimamo ya vyama vyetu vikubwa vya kisiasa na
> > hata vile vya kutetea haki za binadamu kwenye sakata hili.
>
> > Sasa ndio wakati wa sisi kuwafahamu nyinyi vyama vya siasa na vya kijamii
> > kwa rangi zenu halisi. Kutumia maneno ya lile tawala dhalimu George W.
> > Bush; kwenye hili choreni mstari ardhini, U are either with us, or against
> > us!!!!!
>
> > Wafanyakazi tunasubiri.
>
> > Note: neno MAKUMIHIJA  si kifupisho rasmi cha kiswahili cha SSRA!!!!! Neno
> > hilo lina asili ya Mlan
>
> > --
>
> ...
>
> read more »

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

No comments:

Post a Comment