Monday, 23 July 2012

[wanabidii] CHADEMA, CUF, NCCR, TLP tujue msimamo wenu kwenye hili!

Wapendwa,
 
Jahazi la wafanyakazi wa sekta binafsi linapitia katika machafuko makubwa kabisa ya bahari yaliyotokana na mabadiliko ya "kanuni" zilizokuwa zinawezesha wafanyakazi kuchukua mafo yao baada ya kuachishwa au kuacha kazi kw hiari. Neno kanuni kama nilivyolitumia linaweza lisiwe limebeba maana yake halisi kwa kuwa tangu mwanzo utoaji huu wa mafao kwa wafanyakazi mara tu wanapoacha kazi haukuwa ni wa kisheria! Yes, haukuwa wa kisheria kwa maana ya kupingana na sheria ya uanzishwaji wa mifuko  ya jamii!
 
Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa utaratibu huo wa kuchukua mafao yao mara tu baada ya kuacha au kuachishwa kazi ulitokana na maelekezo au busara za rais wa awamu ya 3 mzee Mkapa kutokana na hali halisi ya nchi yetu ilivyokuwa kwa wakati huo na ninamini imeendelea kuwa hivyo ever since. Yeyote mwenye taarifa zinazopingana na hizi na aziweke hapa sasa au akae na ukimya wake milele!
 
Siku chache zilizopita mamlaka ya kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii ( MAKUMIHIJA) au kwa ufupisho wake wa kiingereza SSRA, ilitoa tamko la kuharamisha muendelezo wa utaratibu wa wafanyakazi kujitwalia mafao yao hayo kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa kutambua madhara ya uharamishaji huo kwa wafanyakazi na familia zao na kwa kutambua kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi hapa Tanzania ni wale walio kwenye sekta binafsi na ile isiyo rasmi ningependa kufahamu misimamo ya vyama vyetu vikubwa vya kisiasa na hata vile vya kutetea haki za binadamu kwenye sakata hili.
 
Sasa ndio wakati wa sisi kuwafahamu nyinyi vyama vya siasa na vya kijamii kwa rangi zenu halisi. Kutumia maneno ya lile tawala dhalimu George W. Bush; kwenye hili choreni mstari ardhini, U are either with us, or against us!!!!!
 
Wafanyakazi tunasubiri.
 
Note: neno MAKUMIHIJA  si kifupisho rasmi cha kiswahili cha SSRA!!!!! Neno hilo lina asili ya Mlandizi.

--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment