Tusijidanganye kwamba mgomo wa madaktari umeisha kwa kuwa wamerudi kazini. Hii si kweli hata kidogo. Tukumbuke unaweza kumlazimisha Punda kwenda mtoni lakini si kunywa maji. Pili tutambue kazi ya udaktari si ya kuponda mawe ili upate kokoto, inahitaji akili na moyo wake ili mgonjwa apate tiba stahiki. Kama serikali yetu haiwezi kuona hili basi Mungu atuhurumie.
Naungana na wote wanaosema serikali ifute kesi iliyoko mahakamani pamoja na kuwarudisha waliofukuzwa kazi. Baada ya hapo sioni watajadili nini maana inaonyesha serikali hawajui "negotiation". Na ndo maana tumekuwa tunaingia MIKATABA mingi isiyo na maslahi kwa Taifa toka makampuni ya kimataifa.
Mtu ambaye anasubiri kusimuliwa hata issue nyeti kama ya madaktari ndipo anatoa maamuzi badala ya kuchambua na ikiwezekana kuwaita akae nao ili apate msimamo wao kwa masikio yake mwenyewe ni ngumu sana kufikia muafaka . Njia pekee labda ile ya kuwahusisha viongozi wa dini, madaktari na Rais, mimi sijui!!!!
Hapa tatizo kubwa ni kuchagua vipaumbele na kukosa uzarendo wa makusudi kwa watawala wetu. Wengine wanaona bora walipwe vizuri wabunge na kuongeza mikoa na wilaya mpya badala ya kuboresha sekta ya afya. Ni bora kuwa na mawaziri watatu kwenye baadhi ya wizara kuliko kuboresha miundombinu ya reli na umeme. Ni bora kuwa na ma DC na ma DAS wasiyo na kazi ya kufanya kuliko kuwekeza kwenye sekta ya kilimo.
Kuna wakati nawaza bora tupigwe na bomu kama la iloshima(Japani) kuliko kuwa na kizazi na Taifa lenye watu wanaofundishwa uizi na namna ya kudhuluma haki za wengine. Taifa ambalo professionals si watu muhimu kwao na ukitaka maslahi mazuri unaambiwa nenda kagombee uongozi wa kisiasa. Inauma sana lakini ndo taifa langu.
Mungu atusamehe, tunahitaji huruma yake ili kulinusuru taifa letu.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
From: Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 9 Jul 2012 17:45:03 +0300
To: <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Cc: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko ] Neno La Leo: Vita Hii Ya Serikali Na Madaktari Ikome Sasa
Rais aliwaita ikulu, akanzungumza nao siku iliyofuata akazungumza na wazembe wa dar es salaam akawatusi na kuwakejeli! huyu si mtu wa kuzungumza naye na hata wakati ule niliwasihii madaktari wasiende maana kikwete nimaneno matupu ya kiswahi swahili, hayupo serious kwa jambo lolote, sijui hata familia yake anaimudu vipi.
kumaliza mgomo ni kutatua matatizo yaliyosababisha mgomo, serikali inasema haina fedha, interpool wanaziona huko uswizi. hapa ni kukomaa mpaka kieleweke. mgomo wa hospitali moja hauwezi kutikisa serikali
2012/7/9 maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Ndugu zangu,NCHI yetu ingali katika huzuni ya uwepo wa mgogoro kati ya madaktari wetu na Serikali yetu. Ni huzuni iliyochanganyika na hofu na mashaka. Suluhu ya kushikana mikono haijapatikana.
Inasikitisha, maana, hii ni nchi yetu, wanaogoma ni madaktari wetu na inayogomewa ni Serikali yetu. Ni wananchi wa nchi hii wenye kutaabika na hata kupoteza maisha yao kutokana na mgomo huu.Hili ni jambo la kuhuzunisha sana. Ni jambo lenye kuitia doa nchi yetu. Huko nyuma kuna tuliosisitiza, na hapa narudia kusisitiza msimamo wangu kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, kuwa hakuna njia nyingine ya kuumaliza mgogoro huu bali ni kwa njia ya mazungumzo ya kindugu na kirafiki. Wahusika wana lazima ya kukaa kwenye meza moja kama Watanzania na kuitafuta suluhu ya mgogoro huu kwa manufaa ya nchi yetu na watu wake.
Kwa sasa kila upande unamwona mwenzake ndiye mwenye makosa. Hivyo, kila upande umejichimbia handakini na kuendeleza ' vita vya kuviziana'. Ukweli, katika vita hivi hakutakuwa na mshindi, maana, kama taifa, sote tumeshashindwa. Na tunaendelea kushindwa zaidi, maana, watu wetu wanaangamia kwa kukosa tiba ya uhakika.
Kimsingi madai ya madaktari ni ya msingi na yanazungumzika. Na hoja za Serikali ni za msingi na zinazungumzika. Hivyo, pande zote mbili zinaweza kuzungumza na kufikia muafaka. Si jambo la hekima kwa sasa kwa madaktari kuendelea na mgomo wao wakati milango ya mazungumzo haijatiwa komeo la shaba, na si hekima vile vile kwa Serikali ' kugomea' kuzungumza na madaktari kwa kisingizio kuwa suala hilo liko mahakamani. Naungana na viongozi wa kidini walioisihi Serikali kufuta shauri hilo na kuimaliza kadhia hii kwenye meza ya mazungumzo.Ni vema na ni busara sasa kwa madaktari wakatangaza, kwa manufaa ya nchi yetu, kuahirisha mgomo wao mara moja na kurudi kazini kuwahudumia Watanzania kwa moyo wote. Wafanye hivyo hata katika mazingira magumu waliyonayo, wakati juhudi za kufikia muafaka na Serikali zikiendelea.Maana, mgomo wowote ni jambo la hasara. Kila siku inayokwenda kukiwa na mgomo ina maana ya hasara kwa nchi na watu wake. Ni hasara ya fedha na uhai. Ndio maana ya pande zote mbili zinapaswa kuhakikisha zinakutana na kutafuta suluhu ya kushikana mikono.Na huko twendako, endapo kutatokea hali ya kutoelewana baina ya Serikali na madaktari, basi, Chama cha Madaktari kianze sasa kufikiria namna njema ya kuendesha migomo tofauti na hii ya sasa. Mathalan, katika kuishinikiza Serikali ingewezekana kuanza na mgomo kwa Hospitali moja na si nchi nzima.
Ingewezekana pia isiwe kwa hospitali nzima bali vitengo kadhaa huku huduma kwenye vitengo vingine zikiendelea. Hata hilo pia lingewaletea usumbufu wananchi na kufikia kuishinikiza Serikali kwenye kujadiliana na madaktari katika kuboresha maslahi yao.
Lakini hili la ' Wild Strike' kwa maana ya mgomo wa nchi nzima lina' hatari ya kiafya' kwa taifa. Tusifike mahala tukachangangia kuifanya nchi yetu wenyewe iende kwa kutambaa kutokana na migomo.Nimepata kuandika, kuwa katika nchi zetu hizi, mganga wa tiba aliyesomeshwa kwa fedha za walipa kodi na kwa miaka mingi anahitajika sana. Mganga wa tiba msaidizi anahitajika sana. Na hata kama angelikuwapo Msaidizi wa Mganga Msaidizi wa tiba , naye angehitajika sana. Vivyo hivyo kwa wakunga wakuu na wasaidizi, wauguzi wakuu na wasaidizi wao. Wote hao anahitajika sana.--Na katika nchi zetu hizi, Serikali hazipaswi kufikia hatua ya kuwatisha na hata kuwafukuza kazi madaktari. Hilo la mwisho lifanyike tu pale ambapo njia nyingine zote za kumaliza tofauti na kusuluhisha migogoro na madaktari zitakapokuwa zimeshindikana. Na kwa nini ishindikane?Naam, Watanzania tungependa kuona vita hii baina ya Serikali na madaktari ikimalizwa haraka kwa kutafutwa suluhu ya kushikana mikono. Inawezekana.Maggid Mjengwa,Sweden.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
This years motto: 'WALK THE TALK'
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment