Monday, 23 July 2012

Re: [wanabidii] Final Update - Beatrice Massawe na Mtoto Mgonjwa Precious Maduhu - July 19, 2012

Nimesikitika sana sana kwa hiki kitendo alichokifanya huyu mama asie na shukrani kweli anafikiri kwa kitendo alichokifanya Mungu anaweza kukubali apate huo ukombizi?? atalaaniwa kwani si baraka ukandanganya ni mkimbiza wakati kwenu hakuna vita. na amewaharibia wengine ambao ni innocent kwa ajili ya kupata msaada. Pole sana mabula lakini Mungu amejua nia yako.

2012/7/19 Mabula Sabula <mabsab@hotmail.com>

Ndugu Watanzania,

 

Za leo popote mlipo? Sisi salama. Sahamani sana kwa kuchelewesha kutoa "final update" kuhusu mgeni wetu Mama Precious na "mjukuu wangu Precious" hapo juu, ambaye alikuwa aondoke jana!

 

Kwanza kabisa napenda kumushukuru Mwenyezi Mungu na Watanzania wote hapa Toronto kwa ushirikiano wenu mzuri ambao umefanikisha  zoezi la Mtoto Precious Maduhu, mtoto wa  Jumanne Maduhu, Mtangazaji wa Morning Star Radio, FM 105.3, Dar es Salaam.

 

Kama mnavyojua, Mtoto Precious na Mama yake Beatrice wamekuwa hapa kwa matibabu ya mtoto tangu kama miezi mitatu sasa. Kwa ushirikiano mkubwa, wa Watanzania wote, matibabu yamekwisha na yamefanikiwa vizuri na kupata "dischrage " ya hospitali kurudi Tanzania. Walikuwa waondoke Toronto kurudi Dar es Salaam July 28, 2012. Lakini safari ilibadilishwa ili waondoke jana, July 18, 2012 na KLM kushukia KIA, ili Mama Precious ahudhurie msiba wa Mama yake mzazi uliotokea Dar es Salaam Ijumaa iliyopita na mazishi Moshi.

 

Ndugu zangu, naandika na majonzi makubwa , Mama Precious na Mtoto hawakuondoka jana. Siku ya Jumanne, July 17, 2012, kati saa sita na saa saba mchana, Mama Precious alimtaarifu mke wangu anaenda kufua. Toka muda huo hakurudi nyumbani pamoja na jitihada za kumupigia simu na meseji nyingi kwamba kuna wageni wanamsubiri hapa nyumbani  kumupa pole lakini hakujibu simu wala meseji. Na huo ndio ukawa mwisho wa kuonekana hapa nyumbani kwetu.

 

Ndugu zangu Watanzania, baada ya kujaribu kuwapigia wote ambao nilijua wako karibu naye na ambao humchukua mara kwa mara kumutembeza, nao wakasema hawajui na kwa siku hiyo hawakuwa naye. Mpaka  saa tatu usiku simu alikuwa hapokei simu wala hajibu meseji, ndiyo nikaanza kuhangaika kumutafuta.

 

Jana Mungu akajalia tukapata taarifa kamili baada ya kuhangaika huko na kule. Mama Precious kashawishiwa na watu (majina tunayo) na mume wake na familia yake abaki hapa kinyume cha sheria kwa kuomba hifadhi ya ukimbizi (Refugee Claim), July 5, 2012 kutoka Serikali ya Canada. Swali hili litaanzwa kusikilizwa baada ya siku 30 huko Etobicoke, Ontario. Hiyo ndiyo taarifa fupi ya hatma ya ya Mama Precious na Mtoto. Kwa kifupi niliumia na kuhuzunika  kwamba kwa muda wote huo nimekaa na Mama Precious kama Mtoto wangu , halafu ananizunguka. Nimesumbuka sana kubadilsha tiketi na mambo mengine hospitali yakamilike ili aondoke jana kujumuika na familia  kwa  msiba uliowapata, kumbe mwenzangu ananiona mimi mjinga; kwani Mumewe Jumamme Madudu na familia yake yote Tanzania ilikuwa inajua. Hili liliniumiza.

 

Kuna mizigo yake aliyoiacha nyumbani. Jana baada ya kupata uhakika na kujaribu mara nyingi simu  yake bila mafanikio, tukaamue kwamba hataki mawasiliano na sisi ya aina yoyote na kwamba alivyoviacha siyo vya muhimu kwake. Pia nilimuambia mume wake kwamba Mama Precious kaacha mizigo na naomba anijulishe maamuzi yake nifanye nini , naye kimya. Kwa hiyo maamuzi niliyoyafanya  leo asubuhi kabla ya kwenda kazini nilipeleka kwenye masanduku mbali mbali ya sadaka.

Kwa kifupi mimi nimemaliza. Namtakia kila la heri.

 

N.B. Hospitali watapeleka mawasiliano ya kufunga jalada kwa Baba Precious kwa sababu hawana contact za Mama Precious. Kwa Watanzania ambao  maombi yao yalikuwa kwenye "pipeline" nitawaandikia barua binafsi ya kuwaeleza kwamba, huduma hii nimesimamisha mpaka uchunguzi na "hearing" zote zimekamilika kuhusu Mama Precious. Ubalozi wa Canada Nairobi umejulishwa. Nategemea ushikiano mzuri kati ya serikali ya Tanzania, Kenya na Canada kulimaliza swali hili haraka ikizingatia sheria na haki za wote na kila wakati, maslahi ya Mtoto wetu Precious yatakuwa mbele.

 

Nawatakia siku njema na ahsanteni tena.

 

Mungu atubariki sote.

 

 

Mabula Sabula

 



 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

No comments:

Post a Comment