Hildagarda
Nadhani mchango wako ni hai hapa. Lakini kuna mambo mawili ambayo huenda hayajafanyiwa kazi sana. Moja ni hili ulilosema la kwamba waandishi wa habari wanatakiwa kuwa na elimu ya fani mbalimbali. Kimsingi ni kuwa katika kila aina ya elimu kuwe na uwezekano wa kuwa na uelimishaji wa jinsi ya kutoa taarifa ya taaluma yake kwa wengine - Uandishi wa habari.
Lakini la pili wengi wa waandishi wetu wamelipigia kelele wakisema hakuna haja ya kuwa na elimu kubwa kama ya Chuo Kikuu. Kwangu mimi naona ni muhimu kuwa na elimu hiyo kama ulivyosema ili kupanua uwezo wa uelewa na upambanuzi ambao katika ngazi za chini za elimu huwezi kuupata. Hili naamiini linapingwa kwa kuwa wengi wa waandishi wetu wa Habari wana kiwango kidogo cha elimu. Kupinga mabadiliko ni kawaida hasa mabadiliko yenyewe yanapokuwa hayakuhakikishii uwepo wako.
Nadhani mchango wako ni hai hapa. Lakini kuna mambo mawili ambayo huenda hayajafanyiwa kazi sana. Moja ni hili ulilosema la kwamba waandishi wa habari wanatakiwa kuwa na elimu ya fani mbalimbali. Kimsingi ni kuwa katika kila aina ya elimu kuwe na uwezekano wa kuwa na uelimishaji wa jinsi ya kutoa taarifa ya taaluma yake kwa wengine - Uandishi wa habari.
Lakini la pili wengi wa waandishi wetu wamelipigia kelele wakisema hakuna haja ya kuwa na elimu kubwa kama ya Chuo Kikuu. Kwangu mimi naona ni muhimu kuwa na elimu hiyo kama ulivyosema ili kupanua uwezo wa uelewa na upambanuzi ambao katika ngazi za chini za elimu huwezi kuupata. Hili naamiini linapingwa kwa kuwa wengi wa waandishi wetu wa Habari wana kiwango kidogo cha elimu. Kupinga mabadiliko ni kawaida hasa mabadiliko yenyewe yanapokuwa hayakuhakikishii uwepo wako.
K.E.M.S.
From: Laurean Rugambwa B. <rugambwa@hotmail.com>
To: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>; Wanabidii Group <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, 23 July 2012, 22:35
Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African Journalist Awards 2012
Dada Hildergarda,
Nakubaliana na wewe, niunge mkono suala la elimu ya uandishi wa habari.
Hapa sisi ni kutanganza warsha, mikutano, nani anafungua nini na kukata utepe wapi.
Wiki hii kuna mkutano mkubwa wa kimataifa unaendelea Washington,DC, watu kama 25,000, lakini hakuna chombo cha habari kinaonyesha picha za watu kwenye matukio, zaidi ya kuonyesha clip ya Hillary Clinton akizungumza kwenye plenary msimamo wa serikali ya marekani.
CNN au Aljazeera hawaonyeshi warsha, hawaandiki press statement verbatim!
Hata ndugu zetu hao wakenya hapo, their standard is high, ndo maana wanaingia kwenye category, nanai atakataa yule Tom Mboya wa Citizen hakusitahili hiyo tuzo?
Kila la heri,
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Date: Tue, 24 Jul 2012 03:52:07
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African
Journalist Awards 2012
Tatizo sio curriculum pekee au shule kufundisha vibaya tu, kusoma na kuwa na ufahamu mzuri na kuwa na uwezo kiakili ni kujituma binafsi pia. Unaweza kuona shule inafaulisha kumbe wanakariri tu. Ukimuweka na wengineo wa kujieleza anashindwa kujieleza kimantiki kuwianisha vitu. Uvivu wa kusoma vitabu vya sekta unayosomea, kuangalia mitandao ya kudesa vitu tu ni tatizo. Masomo ya kumfanya mtu afikiri kwa makini kimantiki ni muhimu. Mwandishi wa habari asiwe form four tu. Awe amemaliza Chuo Kikuu au angalau form six halafu amekwenda chuo/vyuo vya specialization kuhusu jambo analotaka kuwa analiandikia. Huko Chuo Kikuu asome sekta husika mfano Misitu, Ustawi wa Jamii, Vita, Uhamiaji, ukimbizi, Politics, Governance, Watoto yatima, Oldage and care and other social issues; Wildlife, Marine science, environmental sanitation and diseases, health, Usafiri majini n.k. Wa usafiri majini lazima ajue kuogelea, kuzama chini kwenye miamba kuonyesha watu viumbe vya huko. Aende serengeti kama ni wa wildlife anatuonyeshe wanyama pori mbali mbali na kutujuza mfano jinsi gani tembo ni mnyama muhimu kuliko viumbe nyote mbugani na jinsi anavyofanya modification ya ecosytem wote tuelewe ili tuwalinde. Au mtu wa Climate atujuze mambo ya mabadiliko ya tabia nchi au jinsi gani tabia za uchafu za binadamu ktk miji zinavyoweza kuhatarisha maisha ya kizazi cha sasa na cha baadae.
Mtu ajitume mwenyewe, akeshe na ashinde akisoma vitabu vinavyotakiwa asikeshe ktk pool table, TV nyumbani au bar. Hata mwalimu awe mzuri nawe unatakiwa-Ujitume binafsi.
Ingekuwa wanafanya hivi na watu kusoma ktk magazeti mengi, kuona ktk TV na sio kusikiliza upande mmoja bali kumuhoji mtu kwa mantiki mawazo atoayo, tungebadilika. Kuna tabia ya waandishi kukimbilia pale pa kupata taarifa rahisi rahisi bila specialization, pili kuweka habari kwa priority ya kuuzika. Utaona daima ni serikali au polisi wabaya. Mwananchi anasema-serikali ije ifunge hizi bar za gongo (ambazo ziko mafichoni, wanaozijua kwa siri ni wao, wapikao wake na watoto wao, wanaokufa na kupofuka ni wao!!). Serikali ije ituondolee hizi takataka n.k. wakati uzoaji taja na mikataba ipo chini ya Mtaa, kuchanga hela ya gari ya kuondoa kulingana na uzalishaji takataka wa kaya au biashara wanaepuka kutoia 500-2000/= kwa wiki badala kutia takataka mitaroni na hapo hapo kwenye mtaro mchafu anauza chakula, mainzi yamejaa ktk kabati la kioo ambalo halifungi ingawaje lina milango na kibanio na watu wanaona mainzi ndani lakini wananunua wanakula. Mwandishi wa habari anatakiwa awahoji kiasi ambacho wataona kibanzi katika macho yao pia.
Uandishi wa makala za kushinda unatokana na uandishi wa kuonyesha realism ya mantiki kisayansi inayokubalika sio one sided views. Kulikuza jambo kwa kichwa cha habari cha kutisha ndani humo hayahusiani; kubadili ukweli ulioongelewa na kuweka udaku unaoleta vurugu badala ya mabadiliko positive katika jamii. Nani atapokea stori zisizo na muono unaotegemewa ktk sayansi ya uandishi? Ukiangalia wana media wa CNN wanavyohoji na kuandika-bado kuna haja ya sisi watu wa story, copy and paste, remba and sale fast kubadilika. Wana habari wangapi kwetu TZ huingia uwanja wa vita Burundi au Congo? Kutembea na meli baharini kuonyesha hali ya kuzidisha abiria na huduma za meli zilivyo?
Sio wengi watafika hivyo unavyotegemea kwa CNN hadi hapo tutakapokuwa na mwandishi wa habari Civil engineer, public health specialist, architect ambaye atatuelimisha na matatizo hata haya ya ujenzi wa majumba mazito ktk Wetland areas, over-extraction ya maji kwa kuchimba boreholes Dar kote ndani ya majuma hayo mazito; kutupa taka kwenye oxidation ponds za mabibo na vingunguti kisha kukesha hapo kutwa na usiku kucha kunywa pombe. Watu wa habati wana majukumu makubwa katika jamii. Tuanze kuwafanya wawe na specialization ili walikwamue taifa kwa kuhoji na kuandika kisayansi.
Ifike wakati pia waitishe makongamano kupitia chama chao, kuonyesha video za taarifa walizokusanya sekta mbali mbali, matukio halisi ili kuboresha good governance.Media ni shule!!
From: RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 24 July 2012, 5:58
Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African Journalist Awards 2012
Kila mwaka wanshiriki zaidi ya mia tatu, lakini kwa miaka minne sasa hatujabahatika kutoa siyo tu mshindi hata mtu wa kuingia fainali. Nilitaraji kwa jinsi tuzo za Media Council zinavyopamba moto then anagalau kutakuwa na watu wawili watakaoingia mwaka huu, lakini ikawa kinyume.
Ukisoma makala mbali mbali zilizoshinda mwaka huu kwenye CNN, utagundua ni kwa nini watu wetu bado wanapwaya lakini nina imani kuna siku wataibuka tu, tuwape muda.--- On Mon, 7/23/12, Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com> wrote:
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African Journalist Awards 2012
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, July 23, 2012, 7:02 AM
LareanWanafunzi wafanyeje wakati wakijaribu kuandika walivyoelewa ni kosa kubwa. Lakini pia kwa mfano wakati wenzetu wa nchi za Ulaya ukipewa assignment wanashauri usijaze full scape zaidi ya mbili lakini Maprof wetu bila kuandika kurasa 15 wanaona hujafanya kazi yoyote. Ni kama unatengeneza kitu kipya duniani.Bila ya kuwa na mfumo wa elimu wenye kueleweka hakika tutakwama tu
2012/7/23 Laurean Rugambwa B. <rugambwa@hotmail.com <> > Tony,
Unajua shida sio mfumo wa uandishi wa habari pekee. Ni kila sekta, kuna shida kubwa.
Wewe jiulize inakuwaje wewe mtu binafsi unaanzisha shule leo unatoa elimu bora kuliko shule za serikali?
Mimi naunga mkono kuwe na shule binafsi lakini je mbona curriculum ni tofauti?
Tukisha fix suala la mfumo wa elimu tutapambana na majirani wetu kwenye sekta zote ikiwemo uandishi wa habari.
Nakubaliana na wewe kuwa wengi wetu tunasoma kujibu mitihani, unakuta mwanafunzi wa chuo kikuu anasoma notes za kwenye daftari kama mwanafunzi wa darasa la tatu. Na akimaliza shule anasoma gazeti tena kule ukurasa wa nyuma maana wengi wana mapenzi na habari za michezo. Hajiendelezi kwenye fani yake ajue kuna nini kipya!
Hilo mimi naona ni tatizo! Tuwekeze kwenye elimu, tuwe na vitabu vya kutosha zaidi ya kushabikia A+ na A, Bs za mtu asiyeelimika.
Kila la heri,
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk <> >Date: Mon, 23 Jul 2012 14:32:00To: <wanabidii@googlegroups.com <> >Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African Journalist Awards 2012Mr Kaaya,Uvivu wa kusoma, kuandika na kufikiri ndiyo common feature ya waTz siku hizi! Unaposikia elimu kushuka unadhani mchezo! Tunataka kila kitu tufanyiwe na serikali na tuendako hata ukitaka kuoa unaomba mchango serikalini. Kujituma kumekwisha na ndio mwanzo wa kuisha kwa utaifa na taifa letu!Mungu Ibariki Tz.Tusione ajabu sana!Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.From: "Elishilia D. Kaaya" <kaayashilia@hotmail.com <> >Sender: wanabidii@googlegroups.com <> Date: Mon, 23 Jul 2012 17:25:14 +0300To: wanabidii@googlegroups.com <> <wanabidii@googlegroups.com <> >ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com <> Cc: AfriCanID@yahoogroups.com <> <AfriCanID@yahoogroups.com <> >; naijaintellects<naijaintellects@googlegroups.com <> >; NigeriansnCanada<NigeriansnCanada@yahoogroups.com <> >; USAAfricaDialogue<USAAfricaDialogue@googlegroups.com <> >; wanabidii<wanabidii@googlegroups.com <> >; wanakenya@googlegroups.com <> <wanakenya@googlegroups.com <> >; Wanazuoni<wanazuoni@yahoogroups.com <> >; youngprofessionals_ke@googlegroups.com <> <youngprofessionals_ke@googlegroups.com <> >Subject: Re: [wanabidii] Final List Of The CNN-MultiChoice African Journalist Awards 2012What a pity that not a single name from Tanzania has featured in this long list. Tanzania indeed boats of high calibre professionals in this particulars field but may be daring remains a serious limitation.Sent from my iPadOn Jul 23, 2012, at 3:52 PM, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com <> <mailto:oldmoshi@gmail.com <> > > wrote: <https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5LYh4wDDmWbKGRrnItd6IYH132GDuONkQ16Icmfrt-QQYBOhrlBeHFJ2UcKAo2hEHXYOy-S1J17Iqva7oGq9nTbAuMnNQDEZZm1R8aEASQYleFmshMsIkbfaWTGYjTjb3Vj8pLhCbF5Bq/s1600/cnn.jpg>(1)Manar Attiya(Egypt)(2)Idris Akinbajo(Nigeria)(3)Tunde Akingbade( Nigeria) (4)Joshua Anny(Ghana)(5)Adriaan Basson(South Africa) (6)Najlae Benmbarek(Morocco)(7)Demelza Bush(South Africa) (8)Edward Echwalu(Uganda)(9)Teresa Sofia Fortes(Cape Verde) (10)Ramusel Graça(São Tome e Príncipe)(11)Arsénio Henriques(Mozambique) (12)Isabel João(Angola)(13)Ahaoma Kanu(Nigeria) (14)Charles Kinyua Kariuki(Kenya)(15)Tom Mboya(Kenya) (16)Craig McKune(South Africa)(17)Musikilu Mojeed(Nigeria) (18)Clive Mtshali( South Africa)(19)Andrew Mulenga(Zambia) (20)Nimrod Taabu Mwagamoyo(Kenya)(21)Jephitha Mwai Mwangi(Kenya) (22)Waihiga Mwaura(Kenya)(23)John Muchangi Njiru(Kenya) (24)Peter Nkanga(Nigeria)(25)Elor Nkereuwem(Nigeria) (26)Evanson Nyaga(Kenya)(27)Verashni Pillay( South Africa) (28)Piet Rampedi(South Africa)(29)Antoine de Ras(South Africa) (30)Megan Small(South Africa)(31)Stephen Ssenkaaba(Uganda) (32)Joy Summers(South Africa)(33)Gerald Tenywa(Uganda) (34)Nelson Wesonga(Uganda) -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ <http://www.mwanabidii.com/> Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ <http://www.kazibongo.blogspot.com/> Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ <http://www.patahabari.blogspot.com/> Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <> <mailto:wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <> > Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/Kujiondoa Tuma Email kwendawanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.-- Bariki G. Mwasaga,P.O. Box 3021,Dar es Salaam, Tanzania+255 754 812 387-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
No comments:
Post a Comment