Jesse,
Nakubaliana na wewe ndo maana mimi kwenye mambo yanayohusu dini huwa nakaa mbali. Watu na imani wanakuwa gizani, ndo maana yule jamaa kiongozi wa dini Uganda Chibwetere aliwateketeza waumini wake. Waliamini, yeye na imani yao kwa dini.
Ndugu yangu hata leo wewe ukisema unaponya, ndo kabisa watu wanafurika kwako.
At the level of analysis deep down most Tanzanians are superstitious, racists and discriminating based on colour, religion, tribe etc.
Ndo maana unasikia watu wanakaa na kuhesabu ni watu wangapi wa kabila moja wako kwenye shirika nyeti au chama cha siasa. Hizo ni dalili za ubaguzi tu.
Na ndio maana baraza la mawaziri linaangaliwa kwa jicho la udini, ukanda,ukabila sio weledi, uzoefu na ujuzi.
Maajabu!
Kwahiyo, hawa wanaotukana wenzao na kuleta maneno ya uchochezi kutumia dini, ni miongozi mwa wengi walio kimya.
Tuanze kujadiliana juu ya nini kifanyike; ukabila unarudi, udini ndo usiseme. Kama taifa hatutakuwa wazi na kujadiliana kwa uwazi bila fitina mambo haya, tutafika pabaya.
Asante,
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: Jesse Kwayu <
jessekwayu@gmail.com>
Date: Wed, 4 Jul 2012 07:30:10
To: <
wanabidii@googlegroups.com>
Subject: FW: RE: [wanabidii] RE: Mawazo ya Katiba, mtazamo wa
Waislam/MASUALA kwa WAHUSIKA!/2-3
Hoja nyingine kwenye jukwaa hili zinakera kweli kweli!
Kwa mfano tukisema Waislam wa Tanzania ni asilimia 75 ya Watanzania wote na Wakristo ni asilimia 20 na wapagani na dini nyingine ni asilimia tano, sasa hizo takwimu zinamuongezea nani sahani ya ugani nyumbani kwake. Kwani kuna mtaa wanaokaa watu wa dini moja tu, au kuna duka au aina ya dawa za dini moja tu, wenye kuhitaji chakula, dawa, umeme, maji na kila hitaji ni wananchi. Tumbo la Mkristo, mpagani au Mwislam lina tofauti gani? Njaa ni njaa tu, mahitaji ni mahitaji tu hayana imani. Tatizo la baadhi ya watu katika taifa hili ni kujitia kujua kwingi wakati hawajui chochote cha maana.
Nadhani kama kuna mwenye hasira na maendeleo hana njia mbadala isipokuwa kufanya kazi kwa bidii na kuondoa umasikini wake. Ndiyo maana hapa nchini wapo baadhi ya Waislamu mabilionea kama walivyo baadhi ya Wakristo na hata wapagani. Ukristo au Uislam au upagani hautoi umasikini kwa kukaa tu, mtu hawi tajiri au masikini kwa sababu ya dini yake. Umasikini unaondoka kwa kutoka jasho, kujituma. Kama hujitumi na badala yake ukakaa kusubiri mgawo wa vya bure utasubiri sana.
Ukiwafuatilia wanaoeneza propaganda hizi za oohh sisi akina Fulani hatutahesabiwa katika sensa utakuta hata shughuli halali ya kujipatia kipato/riziki wanayoifanya ni vigumu kuibainisha, hawa wanajitia wakereketwa wa maendeleo. Tuache kuichafua nchi bila sababu za maana. Mwisho, Waafrika kwa ujumla wetu tuache kutamba kwa sababu ya dini hizi, si Ukristo wala Uislamu, zote tuliletewa hapa tu, si asili yetu wenye dini zao wako kimpya wala huwasikii wakipiga kelele za udini. Mwenye kulibishia hili na aseme.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+
unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment