Wednesday, 27 July 2016

[wanabidii] VODACOM NI MAJIZI WA KUTUPWA!

Hizi kampuni za simu baada ya kubanwa na Dr Makufuri walipe kodi, hasira zao wamezihamishia kwa wateja wasiokuwa na hatia. Tazama jinsi hizi kampuni zinavyowaibia wateja waziwazi:

Nimetumiwa meseji hii kutoka Vodacom nikiwa online lakini nikiwa si-upload chochote kile kwenye laptop yangu:

*******************
MB za kifurushi cha Intaneti cha TSH 1000 zimekaribia kuisha. Salio ni MB 37.3. Kuongeza kifurushi bofya: http://vda.cm/JazaIntaneti au piga *149*01#
Time: 7/27/2016 9:54:57 PM
*******************************************************************************
Nikiwa bado naendelea kusoma meseji hiyo na nikiwa sija-upload kitu chochote, nikatumiwa meseji nyingine hii:

*******************
Name:
Number: VodaTaarifa
Content:
MB za kifurushi cha Intaneti cha TSH 1000 zimekaribia kuisha. Salio ni MB 18.2. Kuongeza kifurushi bofya: http://vda.cm/JazaIntaneti au piga *149*01#
Time: 7/27/2016 9:56:33 PM
*****************************************************************************
Mwisho nimetumiwa hii hapa ndani ya muda huo mfupi:
*************************
Name:
Number: VodaTaarifa
Content:
Umefika mwisho wa matumizi. Endelea kutumia intaneti kwa Tsh.0.2 kwa KB. Kununua tena, bonyeza http://vda.cm/JazaIntaneti
Time: 7/27/2016 9:59:03 PM
************************
Hii mana yake ni nini? Ina maana ndani ya dakika 4 (9:54:57 PM hadi 9:59:03 PM) nimetumia MB 37.3. Hii inawezekanaje? Hakuna uwezekano kama huo zaidi ya wizi wa mchana kweupe. Hata kama nilikuwa naplay youtube isingewezekana kumaliza 37.3 MB ndani ya dakika 5! Moja kwa moja huu ni wizi wa KIJINGA. Inawezekana hizi meseji zimetegwa tu kwenye system kwamba baada ya muda fulani wa matumizi ya internet zirushwe kwa mteja hata kama bundle yake haijaisha inafyekwa juu kwa juu. Hii ni biashara KICHAA, na hakuna mteja yeyote anayeweza kuvumilia WIZI huu wa KIBWEGE! Sikutegemea UJINGA huu kutoka kwenye kampuni kubwa kama Vodacom. When you grow horns, you also need to grow up! I didn't expect such a foolish theft from Vodacom.

N.B
Huu WIZI unanitokea mara kwa mara ila leo uvumilivu  umefika tamati. Nina hakika wateja wengine wa Vodacom mliomo humu mmeishashuhudia huu wizi UCHWARA. Siwezi kuwa adui kwa usema ukweli.



0 comments:

Post a Comment