Friday, 26 June 2015

Re: [wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?


sasa ningependa kusikia kuhusu watia nia wengineo pia. Inawezekana kabisa hii ikawa kama safu ya mashambulizi ya Barcelona. Waweza kumkaba sana Messi, na kweli Messi ni hatari, lakini unawaacha akina Neymar, na wengineo kukufunga. Na kwa vile wote ni team moja, basi wameshinda wao.
 

From: 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, June 25, 2015 5:19 PM
Subject: Re: [wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?


Hii Kali sana. Sina la Kusema. Nimefungwa mdomo. Mlongaji kamaliza. Kazi kwenu wapiga KURA mpate KULA.

--------------------------------------------
On Thu, 25/6/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?
To: "Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 25 June, 2015, 14:04

Na Navaya ole Ndaskoi

PHILEMON Ndesamburo, Mbunge wa Moshi Mjini, ni miongoni mwa
wabunge walioijadili Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge
iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa
Dharura ulioipa ushindi Richmond LLC ya Houston, Marekani
2006, iliyosababisha, aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa,
kujiuzulu.

Ndesamburo aliliambia Bunge, "…nchi za wenzetu kama za
China, wahujumu wa namna hii si kwamba wanajadiliwa,
wananyongwa hadharani."Mafisadi wananyongwa China. China
ilimhukumu kunyongwa Liu Han Februari 2015. Han alikuwa na
shilingi trilioni 10. Gazeti la Telegraph la Uingereza la
Februari 9, 2015 liliripoti kuwa Han alikamatwa 2013 na
kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.
Opereshini Fox Hunt; maana yake ni operesheni Kamata Mbweha,
ni maarufu sana nchini China.

Kamata Mbweha imefanikisha kukamatwa watuhumiwa wa ufisadi
680 waliokimbilia Marekani, Canada, Australia na kwingineko.
Walirudishwa China kujibu mashitaka ya ufisadi.
Waliopatikana na hatia tayari wamekwishakunyongwa. China
haitaki porojo.

Dk. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati, aliwasilisha
taarifa ya Richmond bungeni Februari 6, 2008. Kamati
ilimtuhumu Lowassa, pamoja na mambo mengine, kuvunja sheria
kwa kushinikiza Tanesco kupokonywa jukumu la kutafuta
kampuni ya kufua umeme.Waziri wa Nishati na Madini,
alimwandikia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julai 13, 2006,
kuwa, "Nimezungumza tena na Waziri Mkuu (Lowassa) leo, juu
ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo (wa Lowassa) ni ule
ule niliokueleza awali na ameagiza…achukuliwe
Richmond."

Februari 7 2008 Spika, Samuel Sitta, alimpa Lowassa nafasi
ya kujitetea. Lowassa alikuwa na saa zaidi ya 14 kujipanga
kujibu. Badala ya kijitetea Lowassa alijiuzulu. Alifahamu
kuwa asingeweza kuwababaisha kisanii wabunge makini kama
akina Mwakyembe?

Lowassa anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond. Si
kweli. Magazeti yalianika bayana kashfa hiyo. Lowassa anadai
kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond akiwaeleza wenzake
"kuhusu habari za magazeti." Alihisi mambo yamemkalia
vibaya siyo?

Lowassa, na wapambe wake, anajitahidi kujionyesha kuwa yeye
ni mtu wa uamuzi mgumu. Anatamani umma uamini kuwa Jakaya
Kikwete ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuvunja mkataba wa
Richmond. Alipoona kuwa Kikwete havunji mkataba kwa nini
hakujiuzulu? Mtu wa "uamuzi mgumu" asingesubiri Kamati
Teule ianike uozo wa kashfa ili kujiuzulu.

Jitihada za Lowassa kujinasua katika kashfa ya Richmond
iliyotia taifa hasara ya zaidi ya shilingi milioni 152 kwa
siku kwa miaka miwili zitagonga mwamba. Anadai alionewa.
Wakuonewa Lowassa? Wajumbe wa kamati hiyo wako hai. Wabunge
waliokuwa wakali wa CCM wakati huo kama Christopher Sendeka,
Lucas Selelii, James Lembeli, Anna Malecela mpo? Dk. Slaa na
wapinzani wenzake waliokuwa bungeni Februari 6 na 7, 2008
watanyamaza?

Vita ya Richmond ina wapiganaji wengi. Hivyo acha niandike
mambo mengine muhimu. Kwanza, uadilifu wa Lowassa unatiliwa
shaka na watu wengi. Septemba 15, 2007 pale Mwembe Yanga,
Temeke, Dar es Salaam na kwa ujasiri mkubwa Dk. Slaa
alimtaja Lowassa katika orodha aliyoita ya "mafisadi."
Na kwa jinsi Lowassa anavyotamani kuwa rais, japo kwa saa
chache tu, angekimbilia mahakamani kama angekuwa msafi.
Hakudiriki!

Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari waliokutana na
Lowassa Dodoma hivi karibuni nao pia waliutilia shaka na
kuhoji utajiri wake. Lowassa aliwajibu kuwa eti ana
"ng'ombe kati ya 800 na 1,000. Kwetu Umasaini unapokuwa
kiongozi unapewa ng'ombe ili usipate taabu kwa ajili ya
kuwakarimu wageni wanapokuja." Huu ni uongo. Hakuna kitu
kama hicho Maasaini.

Lowassa anadiriki kuwakashifu wazalendo wanaopinga wizi wa
mali za umma. Alisema, "...kudanganya watu kwamba nikiwa
masikini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga." Hili ni
tusi la nguoni kwa wanaopambana na ufisadi. Utajiri usio na
maelezo ni batili. Hakuna anayewachukia matajiri waliopata
fedha zao kwa juhudi na njia halali, wanaolipa kodi na
hawajawahi kupora ofisi za umma.
Bilionea Philemon Ndesamburo, kwa mfano, ni kipenzi cha
watu. Hakuna anayeutilia shaka utajiri wake. Anamiliki hadi
chopa. Bilionea mwingine anayeheshimika ni Dk. Reginald
Mengi.

  Mengi anamiliki hadi vyombo vya habari. Haiwezekani
kuwaorodhesha hapa matajiri wasafi Tanzania. Ni wengi sana.
Nani mwenye mgogoro nao? Pili, kinyume cha majigambo yake na
wapambe wake kuwa eti ni mchapa kazi na mwenye kuchukua
uamuzi mgumu Lowassa ni adui mkubwa wa sheria na utawala
bora.

Gazeti la Mwananchi la Mei 26, 2015 lilimnukuu Lowassa
akiuelezea uviziaji wake wenye shaka, "Chini ya uongozi wa
Rais (Benjamin) Mkapa tukagundua hawa jamaa (City Water) ni
matapeli...tulifanya kikao saa tisa alasiri, tukachukua
kibali cha kumkamata yule Mzungu wa City Water na
tukamfukuza akaondoka siku hiyo hiyo kwa ndege kurudi kwao,
tulifanya saa tisa alasiri ili asiende mahakamani kupata
zuio, kwa hiyo tulivizia muda huo ili asije kwenda kupata
zuio." Huo ni uviziaji wa kimafia. Mzungu huyo hakupewa
haki ya asili ya kusikilizwa. Si ajabu walimvizia asije
akafungua mkoba wa mabaya.

Tatu, Lowassa alikuwa kinara wa mtandao wa uliomwingiza
Kikwete madarakani mwaka 2005. Kikwete aliposhinda alimteua
Lowassa kuwa Waziri Mkuu; kuthibitisha majigambo ya Lowassa
kuwa yeye na Kikwete "hawakukutana barabarani."
Waliuhadaa umma kwa maneno matamu kama vile "ari mpya,"
"nguvu mpya," "kasi mpya" na porojo nyingine kama
"maisha bora kwa kila Mtanzania." Ni wazi kuwa ahadi za
Kikwete zimebaki hivyo; ahadi. Shilingi imeporomoka. Gharama
ya maisha imepanda.

Lowassa asivyojali hayo leo anajipitisha badala ya kuomba
radhi kwa kuudanganya umma.
Nne, baadhi ya waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya
habari, wanajitahidi kumsafisha sana Lowassa, lakini
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anawaonya Watanzania
dhidi ya genge hili, "Hao wanaomtaka Lowassa ni wale
wanaojua watanufaika binafsi (Lowassa akiwa Rais)."

Mwisho, ni rahisi samaki kuishi nchi kavu kuliko Lowassa
kuhamia vyama vya upinzani hasa vile vinavyounda Ukawa.
Kwanza, hadiriki! Pili, hatakiwi kule. Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa Chadema, ameshasema Lowassa "hafai kuongoza
Tanzania." Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF, nae
amekaririwa mara kadhaa akisema kuwa "Lowassa ni
msanii."

CCM, kwa vyovyote vile, haina sababu ya kumwonea haya
achilia mbali kumwogopa Lowassa.

Raia Mwema
Toleo la 411
24 Jun 2015

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment