Saturday, 2 February 2013

Re: [wanabidii] Re: Hamisi Kigwangalla: Hoja Binafsi ya Kuongeza Ajira kwa Vijana na Kukuza Uchumi



 

Duh, Dr Kigwa!

What a lost opportunity!

Nimesoma habari hii nikiwa nimechelewa. Ningeiona mapema, mimi ningeshauri, na nadhani bado ushauri huu unaweza kufaa, kwa sababu ambazo nitazieleza.

Tunapozungumzia ukombozi wa vijana, haraka utasikia kuwa "wawezeshwe" kwa maana ya kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshwa!

Vijana hawahitaji mikopo. Mikopo(soma: madeni) ni utumwa! Wote tunafahamu jinsi vijana wanavyochakarika mara kuchoma mkaa mara kufanya shughuli za seremala. Nimesafiri miji na vijiji vingi nchi hii. Nimeona hizi ndizo shughuli kubwa zinazofanywa na vijana. Mi nafikiri hivi:

1.Halmashauri zote ziache kuagiza samani (fenicha) kutoka nje, au kutoa tenda za kuleta madawati kwa vibopa wa wilayani. Sehemu ambako vijana hawa wapewe tenda hizi, wasiombwe rushwa, walete mzigo walipwe kwa wakati.Hii hasa ni kwa zile Halmashauri zenye misitu mingi. Ni aibuje nchi hii shule kukosa madawati? Kwanini halmashauri kama Mafinga na Njombe(kwa kutaja chache), zisiwatafutie vijana vitalu(hata kwa kuwakopesha halafu kuwakata kwenye mauzo), ili wapate mbao tu kwa ajili ya kutengeneza madawati tu? Hivi sehemu kama Mafinga, au mkoa wa Iringa mzima kusema eti shule hazina madawati, ni akili kweli? Mimi sijui "intricacies" za kutawala, lakini kwa kutumia akili ya kawaida, sioni kama hapa nazungumza abrakadabra yoyote!

2.Tuache kuwatumia vijana kwa maslahi yetu ya kisiasa na kuwashawishi(kwa uongo) kwamba kwa kutubebea mikoba, na pengine, kuingia front na kuwa na uwezekano wa kujeruhiwa au kufa, ndio ukombozi wao. Tuwafikirishe kuwa ukombozi wao ni wao wenyewe.

3.Halmashauri zinaweza kuwapa vijana kandarasi ndogo ndogo  kama kuchimba barabara, kuziba mashimo, kuzibua mitaro na kusafisha mito na au maziwa kuondoa magugu maji. Hili nalo mpaka apewe mkandarasi" Utakuta mfanyabiashara anamiliki biashara inaitwa "A & B Company. Dealers in General Supplies" Hii general supplies maana yake ni biashara inayoanzia duka, steshenari, kupeleka chakula na kuni hospitalini, magereza na mashuleni, ujenzi, useremala nk. Dhamira ikiwepo, baadhi ya hizi kazi zinaweza kufanywa na vikundi vya vijana.

4. Kwa wale waliomaliza elimu ya vyuo wasio na ajira, hapa nadhani tuangalie sheria za ustaafu, ili watu waondoke na wengine waingie. Aidha utaratibu wa ajira ubadilike. Kila ajira ya umma iombwe watu wasailishwe. Nchini Afrika Kusini, idara zote za Serikali zinaitwa "Business Departments". Kazi inawekewa malengo na inakuwa ya mkataba. Usipoyimiza malengo, basi unaondoka. Ajira tuiondoe kuwa ni reserve ya vigogo na washirika wao. Ni kwa kuajiri vijana weledi "competent" ndipo hata uchumi wetu utakapo kua kwa maana halisi, kuliko hii tunayoaminishwa nayo!

MJL

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment