Tuesday, 24 July 2012

[wanabidii] URAIS 2015 : JOSHUA NASSARI AMKANA ZITTO KABWE

Katika barua yake kwenda kwa mhariri mtendaji mkuu wa Mwananchi. Hii
ni sehemu ya waraka huo wa Nassari.

Nukuu hiyo si ya kweli. Nimesikitishwa sana na upotoshaji mkubwa wa
kunilisha maneno mdomoni uliofanyika katika sehemu kubwa ya habari
hiyo (mbali na nukuu hiyo) kwa maslahi ambayo sijui ni ya nani.

Wakati ukijiandaa kuchukua hatua kutokana na sababu ya pili ya
kukuandikia barua hii ambayo nitaieleza punde hapa chini, naomba
utafakari masuala kadhaa, ikiwemo; kwa nini ilichukua siku zaidi ya
tano kwa habari hiyo kuandikwa?

Pili, kutokana na usumbufu mkubwa ambao nimeupata kutoka kwa
Watanzania wa maeneo mbalimbali wanaotarajia kuniona mwakilishi wao
nikizungumzia masuala yanayowahusu wao, ambayo ni muhimu zaidi kuliko
jambo jingine lolote kwa sasa.

Lakini pia nikiwa Mtanzania anayetambua umuhimu na unyeti wa nafasi ya
urais katika nchi hii na kwamba inaamuliwa kwa maslahi mapana ya umma
wa Watanzania wala si uchu wa watu wachache, hivyo nisingeweza kutamka
maneno hayo ambayo gazeti lako limeandika, naomba kukuandikia rasmi
kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo
ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.

Lakini pia nikiwa Mtanzania ambaye ni mwanachama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kinaamini kuwa kwa sasa
suala la urais si kipaumbele, bali muhimu kwa wakati huu ni
kushughulika kujua mizizi au vyanzo vya matatizo makubwa
yanayowakabili Watanzania ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi
na utawala mbovu wa CCM, kwani serikali imekuwa ikishughulikia
matokeo.

Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe,
naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama taifa ni kutafuta
mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya
Watanzania.

Kwa chama changu na mimi mwenyewe pia kama mwakilishi makini wa
Watanzania, naamini kuwa siku zote suala la urais linategemea mahitaji
ya Watanzania na kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa na utashi
au uchu wa watu binafsi.

Lakini pia suala la nikiwa kama mwanachama mwaminifu wa CHADEMA na
ninayeipenda nchi yangu kwanza, naamini kuwa suala la urais linafuata
katiba, kanuni na taratibu za chama, hatua ambayo haijafikiwa kwa
sasa.

Naomba kusisitiza kuwa sijawahi kutamka, siwezi kutamka na sitarajii
kutamka maneno hayo uliyoyaandika kwenye gazeti tena kwa kuninukuu na
kuniwekea maneno mdomoni. Naomba kurudia tena kukutaka ukanushe habari
hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika
toleo tajwa.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment