Wednesday, 25 July 2012

Re: [wanabidii] Ufafanuzi wa Mhe Zitto Kabwe Kuhusu kusafishiwa Njia ya Urais 2015

Mh. Zitto,

Umeeleza vizuri sana. Ila akiba ya maneno katika hili haipo. Labda kama kuna jambo limejificha.

Lwega

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Boniface Magessa <magessabm@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, July 25, 2012 10:10:59 AM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] Ufafanuzi wa Mhe Zitto Kabwe Kuhusu kusafishiwa Njia ya Urais 2015

kwa kutafakari kidogo tu haya yalioandikwa na zitto..ni kwamba wabunge wale
waliyatamka waliyonukuliwa kuyatamka ktk tamasha lile, pengine
walilazimishwa kuyakanusha!

2012/7/25 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>

> na Zitto Kabwe
>
> Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari
> yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari
> hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa
> zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari
> kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala
> yafuatayo.
>
> Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola,
> Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David
> Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa
> kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.
>
> Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph
> Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba.
> Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao
> yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au
> hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
>
> Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza.
> Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee,
> Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
>
> Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na
> video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya
> documentary ya tamasha lile la kihistoria.
>
> Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii
> iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana
> katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe
> tukio la Kigoma tu.
>
> Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi
> itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi
> zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema
> Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao,
> habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli
> ndio utasimama.
>
> Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya
> kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya
> urais yanapotajwa zinashangaza sana.
>
> Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea
> Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato
> utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha
> bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii
> na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa
> hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
>
> Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema
> 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba
> ya maneno. Tusimalize yote.
>
> Zitto Kabwe
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>


--

Sent from Samsung Galaxy Ace GT-S 5830 --The future of Android Technology

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment