Thursday 31 July 2014

Re: [wanabidii] Re: URAIS 2015-MATATIZO YA BERNARD K. MEMBE

Haya mwenzetu  unamtaka nani umnadi basi lakini muda wa kampeni bado

On Jul 31, 2014 12:16 PM, "'Godfrey Ngupula' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Nimeleta topic hii ili kwa pamoja pia tujadili matatizo ya mtu mwingine anayetajwa sana kuwa anaweza kuibuka kidedea katika kinyanganyiro cha urais CCM. Kwa mtazamo wangu Membe kwa haya yafuatayo sioni kama anafaa kuwa raisi wa Tz:

(a) Kwanza haaminiki: Ili mtu aweze kuaminika na jamii kubwa ya watazania ni lazima ajulikane undani wake na ikibidi madhaifu yake na strengths zake.Lakini Membe anaonekana yupo yupo tu na huku kwa nguvu zote akijitahidi kujificha asili yake, na hiki watu makini hatuwezi kumuamini haswa kwa dhamana ya nafasi kubwa kama uraisi. Binafsi siamini hata kidogo kama Membe anaweza kukemea chochote na kufanya chochote kwa maslahi ya nchi na haswa kitu kinachohusu kuwa na maamuzi magumu na yenye tija.

(b) Sio safi. Watu wengi wanadhani Membe ni mtu safi. Lakini, ukweli ni kuwa Membe si safi hata kidogo. Ni huyuhuyu ndiye aliyesema Tanzania inaweza kupokea hela kutoka kokote na kwa masharti yeyote hata kama anayetupatia fedha hizo ni shetani. Uraisi ni suala la values na misimamo. Kama mcha Mungu wa kweli ni lazima kuna mambo fulani mtu utakuwa nayo au basi kukupa hofu kiasi fulani. Sipendezwi na mtu ambaye anaweza fanya chochote ali mradi tu, afanikiwe katika mambo yake.Kwa lugha nyingine Raisi ajae hapaswi kuwa msani msanii kama Membe.

(c) Hana maamuzi magumu: Nchi kwa jinsi ilivyo na inavyoenda kwa sasa inatakiwa mtu mwenye uwezo wa kuleta displine katika system. Eti Tanzania nayo ina ugaidi wa ndani, huu ni udhaifu wa kimfumo kutokana viongozi wakuu kufumbia macho  baadhi ya mambo kwa maslahi binafsi. Kwa tunakotaka kwenda Membe ni dhaifu sana  na hawezi kukemea chochote na haswa akijua kundi fulani litampa kura,basi kundi hilo laweza fanya chochote na asifanye kitu. Hebu angalieni watu wanaompigia debe Membe, RidhiOne, Kigangwala,nk, wote ni wasanii sanii tu ambao bado hawajatoshea katika kusimika misngi ya kiinchi labda huko baadae.

(d) Hana historia.  Kiukweli kabisa mpaka hapa tulipo nchi imepitia mambo mengi. Binafsi huwa sipendi mtu kuibukia kona fulani na kutangaza nia ya kuutaka uraisi kwa kisingizio unakerwa na kero za watanzania,lkn hata wakati mmoja hujawahi kuwa suluhisho la kero hizo na ni kiongozi. Membe hapo alipo ni kudra tu za familia ya JK na ndio hao wanataka kuendelea kutuongoza tena kwa mgongo wa Membe,nafikiri watanzania tunayo haki ya kuchagua mwingine tunayedhani ana uwezo wa kutusaidia.  na mengine mengiiiiiiii...NGUPULA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Read More :- "Re: [wanabidii] Re: URAIS 2015-MATATIZO YA BERNARD K. MEMBE"

[wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?

NA MOBHARE MATINYI

Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo wa Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini - si kwa kuwa mimi ni mkurya! La hasha!
Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya karibuni wamekuwawakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si mjadala wake.

NANI ALIWAINGIZA JESHINI
1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia, Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata amakuwahamasisha vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea, akiwemo Marehemu babu yangu mzaa mama na baba yangu mkubwa, walikataa kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe zao. Hawawalipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wakuingia jeshini ukaanzia hapo na kuendelea.

2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo. Mfano,Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa - kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholi na ikibidi sana Wakakwa (kabila la Idi Amin). Nchini Kenya walisemakwamba kwa askari bora uchukue Wakamba. Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na Wahehe. Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu. Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila kiongozi wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere hawakuzifuata.

MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA
3. Nini matokeo ya mpangilio huu wa Waingereza? Kule Uganda karibu wanajeshi wote wakati Amin anaichukua nchi (walikuwa 8,000 hivi), walikuwa Walango, Waacholi na Wakakwa lakini kwa kuhofia kupinduliwa akaanza kuwauaWaacholi na Walango na kuwajaza Wakakwa na baadaye akawaweka mpaka Wazaire na Wanubi wa Sudankusini na kaskazini mwa Uganda. Kule Kenya hadi kesho, majeshi ya Kenya yamejaa Wakamba na kwa mnaofuatilia mtamkumbuka Jenerali Muringe. Kwa kuwa Wakikuyu wamekuwa wakishika dola, Wakamba waliminywa kwenye vyeo vya chini lakini wamejaa majeshini Kenya kupita kiasi, hasa kutokana na umaskini wa nchi yao ya Ukambani ambayo ni kame pia.

NYERERE KUUNDA JWTZ 1964
4. Kwa Tanganyika Wakurya walijaa jeshini mno wakati tunapata uhuru kiasi kwambaNyerere akasema hili ni tatizo.Alipovunja Kings African Rifles na kuunda JWTZ baada ya maasi ya 1964, Nyerere aliamua kuweka sera kimya kimya kwamba jeshi hili litakuwa na watu wa makabila yote. Ilikuwa kazi ngumu kwake kwa kuwa waliokuwa wanakuja kujiandikisha kwa wingi walikuwa ni Wakurya zaidi kutokana na utamaduni wa kawaida wa Wakurya wa kupenda kupigana, vita, ukakamavu, umwamba, n.k. Wakurya, kama Wakamba, Waacholi, Walango, na Wakakwa waliitwa na Waingereza "Marshal Tribes" -yaani makabila ya wapiganaji. Hata hivyo, Nyerere alifanikiwa kuwapunguza mno lakini bado alibakia nao wengi kutokana na utamaduni, historia na ukweli wa mambo,kwamba ukitaka askari mzuri chukua anayependa vita, siyo mtu mwoga. Kama si Nyerere, jeshi lingekuwa wakurya watupu, siyo wakurya wengi, bali wao wenyewe kwa hata 90%.

WAKURYA NA NYERERE
5. Wakurya hawakuwa na urafiki wowote na Nyerere kama watu wanavyodhani kutokana na fikra za Kiafrika kwamba kila kitu kina nguvu za siri nyuma yake, iwe baraka za Mungu, rushwa, udini, mapenzi, ukabila, uchawi, fitna, mkosi, n.k. Mwafrika haamini kwamba kitu kinaweza kutokea kwa sababu zake chenyewe bali mpaka kuwe na mtu mwingine anayekifanya kitokee. Kati ya watu waliotaka kumpindua Nyererekwenye miaka ya 1960 mwishoni, kwa mnaofuatilia, walikuwepo akina Chacha (nahifadhi jina lake kamili), na kutokana na tabia ya Wakurya kumtukana Nyerere alipokwenda ziarani Tarime, aliamua kuacha kufanya ziara huko. Si hivyo tu, Nyerere alikwepa hata kuwapa nafasi za juu Wakurya na mkurya pekee aliyewahi kushika uwaziri katika miaka 25 ya Nyerere ni Bhoke Munanka ambaye walikorofishana hata hivyo (waziri pekee aliyemwambia kwamba huu ujamaa wako utaumiza watu na hakuna anayeutaka). Kamamjuavyo, Munanka alikuwa mfanyabiashara mkubwa katikati ya ujamaa.

6. Aidha, Rais Nyerere hakuwahi kumteua mkurya kuwa mkuu wa majeshi wala msaidizi wala chochote cha juu ingawa ukiongea na watuwanakwambia mambo mengine kabisa. Mkuu wa kwanza wa JWTZ alikuwa Sarakikya kutoka Meru; akaja Twalipo kutoka Songea; akajaMusuguli kutoka Bunda (si mkurya). Rais Mwinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kumteua mkurya kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Kyaro, na baadaye Mkapa akamteua Jenerali Waitara. Hata kwenyeVita ya Uganda, Nyerere hakumpa mkurya kuongoza vita ile ingawa kwenye makamanda wa chini Wakurya walijazana kama utitiri, achilia mbali askari wa kawaida. Ni Mwita Marwa pekee ndiye aliyekuwa kwenye makamanda wa kuongoza brigedia, lakini wengine wote walibanwa pembeni........Nyerere hakutaka taabu baadaye.

WAKURYA KUPENDA VITA/JESHI
7. Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia, tulipovamiwa na Amin Oktoba 31, 1978, na baadaye Nyerere kutangaza vita, serikali ilitoa mwito kwa wananchi kujiunga na mgambo/jeshi kwa hiari. Nafasi zilikuwa 2,000 kwa kilamkoa. Wakurya walilaani kitendo hicho cha kuweka ukomo wa idadi na wakatuma wajumbe kwenda kulalamika kwa Nyerere kwamba idadi ya 2,000 ni ndogo mno kwa mkoa wa mashujaa. Nyerere akasema hawezi kuondoa ukomo huo. Wakatuma tena ujumbe wa pili, na Nyerere akashauriwa na makamanda wake kwamba kwa kuwa mikoa mingine imeshindwa hata kufikisha 500 tu, basi ni heri Wakurya waachiwe waje tu. Nyerere akasema kwamba basi anaruhusu nafasi 4,000 kwa mkoa wa Mara. Hii imeandikwa kwenye vitabu na waandishi wasiokuwa Watanzania.

8. Wazee wa mkoa wa Mara walikerwa mno na uamuzi waNyerere wa kuweka ukomo mwingine wa 4,000 na wakaamua kwamba dawa ni rahisi sana, kwamba vijana wao waende kwenye mikoa ambayo ilikuwa imeshindwa kufikisha idadi ya 2,000 ya awali. Huu si utani. Kaka yangu alikwenda Morogoro. Baba yangu mkubwa alikwenda Moshi na ndugu yangu mwingine alikwenda Usukumani na wote wakaenda vitani na wakarejea kwa ushindi na furaha. Wote wapo hai hadi leo na kaka yangu huyu aliingia Magereza baadaye. Kwa kifupi, Nyerere aliwabana Wakurya wasiendevitani kwa wingi kama walivyotaka. Mjomba wangu Nyaronyo Kicheere alipata medani ya vita pia kwa kujitolea kwenda vitani akitokea JKT - yumo humu ukumbini muulizeni.

KWA NINI WAKIMBILIE JESHINI
9. Mimi binafsi, wakati ninamaliza kidato cha sita na huku nikiwa nimefaulu, uamuzi wangu ulikuwa kwenda JWTZ kwanza na mambo mengine yafuate baadaye. Kama si wazee wangu kunikatalia, leo hii ningekuwa kwenye magwanda. Naomba Kivuyo na LKK mniambie, mimi niliyezaliwa mjini, nikakulia Dar es Salaam, simjui Nyerere wala hanijui, ninahusika vipi na Nyerere wakati aliacha urais nikiwa sijafika miaka 18? Nyerere ametoka kwenye urais mwaka 1985 lakini miaka 27 baadaye bado Wakurya wamejaa jeshini ingawa wananyanyaswa kutokana na maneno ya kipuuzi kama haya, je, Nyerere anahusika vipi na kuwepo kwao? Mkurya wa miaka 20 leo, aliyeko jeshini, anahusika vipi na Nyerere? Kwa ufupi ni hivi ........... Wakurya tunalipenda jeshi, basi! Nenda hata Kenya utawakuta jeshini, mpaka hapa Marekani wamo jeshini. Je, Nyerere aliitawala Kenya na Marekani?

10. Pili, kutokana na maendeleo kuwa nyuma sana mkoani Mara, sehemu pekee ya ajira ilikuwa jeshini kwa miaka mingi hadi walipoanza kuchimba dhahabu kwa wingi kule Nyamongo, na kuuza ng'ombe kwa magendo nchini Kenya. Wilaya ya Tarime, wakati ule wa Nyerere, ilikuwa kama sehemu ya Kenya kwani magharibi ilizibwa na Ziwa Viktoria, kusini na mbuga ya Serengeti, na kuja Mwanza kulikuwa na mto usiokuwa nadaraja (Mwinyi alilijenga baadaye), kule mashariki na kaskazini ilikuwa nchi ya Kenya. Nyerere hakutaka hatakufanya ziara tu, achilia mbalikujenga walau shule moja. Hivyo, jeshi likawa kama kimbilio la ajira lakini hii ikiwa ni baada ya kuangalia kwanza hulka na silka ya Wakurya kwenye masuala ya kupigana/jeshi/ushujaa, n.k.

Ndugu zanguni Kivuyo na LKK, siwalaumu kwa kudhani hivyo kwa kuwa haya maneno yako hivyo lakini kama nilivyosema, ndivyo Waafrika tulivyo. Ushahidi uliopo ni kwamba Nyerere hakuelewana na Wakurya hata mara moja na aliwabana wasiingie jeshini lakini akafika mahali akashindwa. Ushahidi ni wa kutosha na mkitaka nitawapa kwenye barua pepe zenu binafsi kwa kuwa hapa si vema kuyataja majina ya watu bila vibali vyao.

Wakurya tuna vitu vitano tunavyovipenda sana: Kupigana, familia, ng'ombe, ukweli na utaifa. Ni fahari kubwa kwa mkurya kuingia jeshini, fahari kubwa mno; wanangu madume wote wawili, mmoja miaka 9 na mwingine 6, wako hapa Marekani lakini wanapenda kuvaa nguo za jeshi na kucheza na matoi ya vifaru, ndege za jeshi, n.k.
Jeshi liko damuni kwa Wakurya!

CHANZO: MOBHARE MATINYI, na MHADHIRI MWANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?"

[wanabidii] Shushushu (Afisa Usalama wa Taifa) ni mtu wa aina gani,anafanya nini?

Kuna ukweli mmoja usiofichika wala kupingika kwamba watu wengi sana wanapenda kazi ya ushushushu, yaani Uafisa Usalama wa Taifa.Hiyo sio kwa Tanzania pekee bali sehemu nyingi duniani. Ukiingia mtandaoni utakutana na watu wengi wanaozungumzia taaluma ya intelijensia au/na wahusika katika hali ya kutamani kuifahamu taaluma hiyo nyeti  au kuwa mhusika.

Leo nitaanza mlolongo (series) wa makala kuhusu taaluma hiyo adimu. Hata hivyo ni vema nikatahadharisha mapema kwamba nitakachoandika ni kile tu kinachoruhusiwa kuandikwa hadharani. Kimsingi,taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri,na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo,kuna maelezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.

Kwa tafsiri rahisi, ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri (clandestine methods). Japo kwa kiswahili ushushushu ni intelijensia, kiundani kuna tofauti kati ya ushushushu unaofanyika ndani ya nchi na unaofanyika nje ya nchi.Kwa hapa Uingereza, Idara ya ushushushu inayoshughulika na masuala ya ndani inajulikana kama MI5 na inayohusiska na ushushus nje ya nchi ni MI6.Kwa huko nyumbani, tofauti hizo zipo ndani ya muundo wa taasisi husika, kwa maana kwamba kuna taasisi moja tu lakini ndani yake kuna mgawanyo wa kimajukumu ya ndani na ya nje.

Kadhalika, japo mashushushu wamekuwa wakifahamika pia kama spies, ukweli ni kwamba spy ni shushushu anayefanya kazi nje ya nchi yake,kitu kinachojulikana kiusalama kama ujasusi au espionage kwa Kiingireza.

Japo mataifa mbalimbali yana miundo tofauti ya Idara zao za Usalama wa Taifa,lengo na kazi kuu ni ukusanyaji wa taarifa hizo.Kwa minajili ya makala hizi, nitazungumzia zaidi mazingira ya huko nyumbani Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni idara ya serikali iliyo chini  ya Ofisi ya Rais,ambayo ina jukumu la kukusanya na kuchambua taarifa za usalama na kuziwasilisha 'mahala kunakohusika' katika namna ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo ataona inafaa.

Kimsingi, mkuu'halisi' wa Idara hiyo ni Rais mwenyewe,ambaye kwa lugha ya kiusalama anafahamika kama 'sponsor.' Wakuu wa Idara za usalama popote pale duniani hufahamika kama spymaster.

Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage),uzandiki (subversion),uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism). Lakini jukumu la Idara hiyo si kukusanya taarifa hizo na kuzichambua tu bali pia kuzuwia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa taifa.

Ni kwa vile utendaji wa kazi wa Idara yoyote ile ya Usalama wa Taifa unaegemea katika usiri mkubwa ndio maana kwa 'mtaani' kuna hisia tofauti kuhusu umuhimu wa taasisi hiyo. Ukweli ni kwamba laiti umma ungefahamu nini kinafanywa (au kinapaswa kufanywa) na Idara hiyo basi kwa hakika ingethaminiwa zaidi ya kuogopwa tu. Ni muhimu hapa nisisitize kuwa ninazungumzia 'hali mwafaka' yaani kwa Kiingereza ideal situation. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wananchi wakiishutumu Idara yetu ya Usalama wa Taifa kuwa imeleemea mno kwenye siasa hasa kuibeba CCM,imezembea mno kiasi cha kuruhusu ufisadi kushamiri, na imekuwa ikilaumiwa pia kutokana na matukio mbalimbali yanayotishia usalama wa Taifa kama vile ugaidi.

Wanaotoa lawama hizo wapo sahihi kwa kiasi flani,kwani  kushamiri kwa maovu katika jamii sambamba na mwendelezo wa matukio yanayotishia usalama wa taifa ni viashiria kuwa Idara ya Usalama ya nchi husika ina mapungufu kiutendaji.

Hata hivyo,ni muhimu kutambua kanuni moja muhimu ya ufanisi au kushindwa kimajukumu kwa Idara ya Usalama wa Taifa popote pale.Ni kwamba wakati Idara husika inapaswa kuwa macho katika kila sekunde kuzuwia matendo ya kidhalimu, wanaopanga kufanya matendo hayo wanahitaji mara moja tu kufanikisha azma yao.Mfano halisi ni kwenye matukio ya ugaidi. Wakati gaidi anahitaji fursa moja tu kufanikisha tukio la kigaidi, Idara ya Usalama inahitaji kila fursa- kila sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwezi,mwaka-kuhakikisha gaidi hafanikiwi.

Kadhalika, wakati inaweza kuwa rahisi kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa inaposhindwa kuzuwia tukio flani, kwa mfano shambulio la kigaidi nchini Kenya, kiuhalisi suala zima la ukusanyaji wa taarifa za kiusalama ni gumu mno. Hebu pata picha: unaletewa tetesi kuwa kuna mtu anataka kulipua bomu kanisa au msikiti. Mara nyingi tetesi hizo huwa hazibainishi jinsia ya mtu huyo,wajihi wake,ni mwenyeji au mgeni na vitu vingine muhimu vya kuweza kumtambua japo kwa ugumu. 

Kutokana na ugumu wa zoezi la kukusanya taarifa za kiusalama,ndio maana wahusika-mashushushu/maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa-wanapaswa kuwa watu wenye akili isiyo ya kawaida, au angalau wenye uwezo mkubwa wa kutumia akili.Neno lenyewe intelijensia linahusiana na matumizi ya akili.Lakini si akili tu, bali pia maafisa usalama wa taifa hupaswa kujifunza na kuendeleza hisia ya sita (6th sense). Mwanadamu wa kawaida ana hisia 5: HARUFU  kwa kutumia pua; LADHA kwa kutumiamdomo/ulimi, KUGUSWA (touch) kwa kutumia ngozi, KUONA kwa kutumia macho, KUSIKIA kwa kutumia masikio. Lakini kwa mashushushu wanapaswa kuwa na hisia ya ziada ya kutambua kitu zaidi ya kutumia hisia hizo 5 kuu. Si kazi rahisi hata kidogo.

Basi kwa leo niishie hapa.Nitaendelea na mfululizo wa makala hizi angalau kila wiki. Usikose kutembea blogu hii kupata habari na makala zaidi kuhusu taaluma hii nyeti ya ushushushu kwa kubonyeza hapo juu ya blogu kwenye seksheni ya INTELIJENSIA 

http://www.chahali.com/2014/07/shushushu-afisa-usalama-wa-taifa-ni-mtu.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] Shushushu (Afisa Usalama wa Taifa) ni mtu wa aina gani,anafanya nini?"

[wanabidii] KORTI YAAMURU MATANDIKO WA MSD ALETWE MAHAKAMA

KORTI YAAMURU MATANDIKO WA MSD ALETWE MAHAKAMA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imeamuru mshitakiwa wa kwanza ambaye alikuwa ni Mkuuu Mkurugenzi wa Operesheni Kanda ya Kaskazini wa Bohari Kuu ya Madawa(MSD), Slyvester Matandiko katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni tatu aletewe mahakamani au hospitalini ili asomewe mashitaka yanayomkabili.

Amri hiyo ilitolewa Jana na Hakimu Mkazi Hellen Liwa ambaye Alisema amekuba liana na ombi la Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(PCCB), Leornad Swai ambalo lilikuwa Linaomba Mahakama hiyo itoe amri ya upande wa jamhuri uende kumsomea Mashitaka Matindiko kwasababu tangu Kesi inayowakabiliwa jumla ya washitakiwa wa tano , mapema mwaka huu, ni washitakiwa wanne tu ndiyo waliosomewa mashitaka na mshitakiwa mmoja (Matandiko) bado hajasomewa mashitaka kwakile kinachdaiwa na upande wa utetezi Kuwa mshitakiwa Huyo ni mgonjwa na hawezi kufika mahakamani.

Ombi hilo liliwasilishwa jana na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.

Swai alidai kuwa washtakiwa wengine wameshasomewa mashitaka bila Matandiko kuwapo mahakamani kwa madai kuwa ni mgonjwa, hivyo kutokana na sababu hiyo, upande wa Jamhuri unaomba Mahakama kuhamia nyumbani kwa mshtakiwa huyo.

hakim Liwa Alisema anaiarisha Kesi hiyo hai Septemba 4 Mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kwamba Agosti 19 Mwaka huu, mshitakiwa Huyo asomewe Mashitaka.

Mbali na Matandiko ambaye ni Mkurugenzi wa Oparesheni Kanda ya Kaskazini wa MSD, wengine ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, ambaye pia ni Meneja wa Viwango, Sadiki Materu, Wasajili kutoka Bodi ya Maabara za Afya ni Zainabu Mfaume na Joseph Nchimbi.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wote kwa pamoja, wanakabiliwa na mashtaka saba, ya kutumia madaraka vibaya, na hivyo kuisababishia hasara serikali ya dola za Marekani 2,093,500, kwa kuruhusu uingizaji wa vitendanishi feki vya HIV nchini, na kuingizwa Bohari Kuu ya Dawa.

Wakati huo huo Kesi ya matumizi Mabaya a madaraka inayomkabili Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taneso, William Mhando imetajwa Jana na imearishwa hadi Agosti 26 Mwaka huu, Kwaajili ya kaunza kusikilizwa.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Agosti Mosi Mwaka 2014

Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] KORTI YAAMURU MATANDIKO WA MSD ALETWE MAHAKAMA"

[wanabidii] WAWILI KORTINI KWA UGAIDI DAR

WAWILI KORTINI KWA UGAIDI DAR
Na Happiness Katabazi
WIMBI la Kuwafikisha washukiwa wa makosa ya ugaidi mahakamani limezidi kushika kasi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi Jana kuwafikisha watu Wengine Wawili kwa makosa mawili ya ugaidi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi, Mawakili waandamizi wa serikali Bernad Kongora, George Baraso na Peter Njike walidai Kesi hiyo ugaidi Na.31 ya Mwaka 2014 na kwamba washitakiwa Hao ni Kassim Salum Nassoro na Said Shehe Sharifu.

Wakili Njike alidai kosa la kwanza ni la kula Njama Kutenda kosa la ugaidi kinyume na Kifungu cha 27(c) Cha Sheria ya Kuzia Ugaidi ya Mwaka 2002 na kwamba washitakiwa hao Katika tarehe tofauti Kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , walikuwa Njama Kutenda kosa kimyume Cha Sheria hiyo kwa kuwaajili watu ili washiriki kufanya matendo ya ugaidi.

Wakili Njike Alilitaja kosa la pili Kuwa kuwaajili watu ili washiriki kufanya vitendo Vya ugaidi kinyume na Kifungu Cha 21(b) Cha Sheria ya Kuzia Ugaidi ya Mwaka 2002. Kuwa washitakiwa wote Katika tarehe tofauti Kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , kwa makusudi wakikubali kumwajili Sadick Absaloum na Farah Omary ili washiriki Kutendavitendo ugaidi na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.

Kwa upande wake Hakimu Moshi aliwataka washitakiwa wasijibu chochote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo na kwamba ni Mahakama Kuu ndiyo yenye Mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo na akaairisha hadi Agosti 6 Mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa ambapo upande wa jamhuri Ulidai siku hiyo utawasilisha ombi Lao.

Julai 17 Mwaka huu, itakumbukwa DPP, aliwafikisha watu 17 mahakamani hapo KWA makosa ya ugaidi..

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la IJumaa, Agosti Mosi Mwaka 2014.

Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] WAWILI KORTINI KWA UGAIDI DAR"

[wanabidii] Hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa Tarehe 31 mwezi Julai, 2014

tangulizi

Ndugu wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kuzungumza na taifa juu ya masuala muhimu yanayohusu nchi yetu. Mwezi wa Saba tunaoumaliza leo ulikuwa na matukio mengi baadhi yakiwa makubwa na kushtusha na mengine yalikuwa matukio ya kawaida. 

Mashambulio ya Mabomu
Ndugu Wananchi; 
Tarehe 3 Julai, 2014 na tarehe 07 Julai, 2014 kulitokea mashambulizi ya mabomu nyumbani kwa Sheikh Sudi Ally Sudi na katika mgahawa wa Vama kwa mfuatano huo. Kabla ya hapo, kulikuwa na matukio mengine matatu: Kanisa la Olasiti tarehe 5 Mei, 2012, Mkutano wa Kampeni wa CHADEMA tarehe 15 Juni, 2013 na Baa ya Arusha Night Park tarehe 13 Aprili, 2014. Hali kadhalika, tarehe 13 Juni, 2014 kulitokea shambulizi la mabomu katika eneo la Darajani, Zanzibar.

Kila lilipotokea shambulizi uchunguzi ulifanyika na watuhumiwa kukamatwa. Lakini, watuhumiwa waliokamatwa safari hii wanaelekea kutoa sura nzuri zaidi ya mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivi vya kikatili pale Arusha na kwingineko nchini. Watu 38 wameishafikishwa Mahakamani, wengine 8 watafikishwa Mahakamani kesho na uchunguzi na msako unaendelea kote nchini kuwapata watuhumiwa wengine. 

Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri iliyotufikisha hapa tulipo sasa. Tunawaomba waongeze bidii, maarifa na ushirikiano mpaka wote waliohusika wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Aidha, natoa pongezi na shukrani maalum kwa wananchi wema waliotoa taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa. Napenda kutumia nafasi hii kuwasihi wananchi wenye taarifa kuhusu wanaotafutwa au ye yote anayejihusisha na vitendo hivi viovu watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama ili hatua zipasazo zichukuliwe.

Kutupwa Viungo vya Binadamu

Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Julai, 2014, katika Bonde la Mto Mpiji lililopo eneo la Bunju Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, viligunduliwa viungo vya binadamu na baadhi ya vitendea kazi vya madaktari vikiwemo aprons na gloves. Viungo hivyo vilivyokutwa vimekakamaa na kuhifadhiwa katika mifuko myeusi 85, vilikuwa vimetupwa jana yake tarehe 21 Julai, 2014. Tukio hilo lilileta taharuki na hofu kubwa katika Jiji la Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.

Uchunguzi uliofanywa uligundua kuwa viungo hivyo vilikuwa vinatumika kufundishia wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Tiba kilichoko Mbezi Beach maarufu kwa jina la IMTU. Ni utaratibu wa kawaida kwa vyuo vikuu vya udaktari nchini na kote duniani kutumia miili ya wanadamu waliofariki kufundishia. Hata hivyo, pale viungo hivyo vinapokuwa havihitajiki tena kwa shughuli hiyo, zipo taratibu zake za kuvisitiri ambazo hazikufuatwa. Bahati nzuri mamlaka husika zimeona kasoro hiyo na hatua zimeanza 

kuchukulikuwa. Tuziachie mamlaka hizo kuchukua hatua zipasazo kwa mujibu wa madaraka yao na kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazotawala shughuli za namna hiyo. Ni matumaini yangu kuwa yaliyofanywa na IMTU hayatafanywa tena na Chuo hicho wala chuo kingine cho chote hapa nchini. 

Ziara Yangu Mikoani

Ndugu Wananchi;
Katika mwezi huu wa Julai, nimefanya ziara katika ya mikoa ya Tanga na Ruvuma. Nimefurahishwa sana na hatua kubwa ya maendeleo waliyopiga wananchi wa mikoa hiyo. Pamoja na mchango wa Serikali, ari na mwamko mkubwa wa kujiletea maendeleo walionao viongozi na wananchi wa mikoa hiyo vimechangia sana katika kuongeza kasi ya maendeleo na mafanikio yanayoendelea kupatikana. Katika ziara hizo, nilizindua miradi iliyokamilika na kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile ya barabara, umeme,maji, afya, elimu, majengo ya Serikali, nyumba na kadhalika. 

Nimepata faraja kubwa kupata taarifa kuwa ahadi zangu nyingi na zile zilizomo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi zimekamilika na zingine ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Ndoto ya miaka mingi, kabla na baada ya Uhuru, ya wananchi wa Mikoa ya Kusini ya kutaka Mikoa yao ifunguke na kuunganishwa na mikoa mingine kwa barabara za lami sasa kuna uhakika wa kukamilika. Barabara ya kutoka Mbinga, Songea hadi Namtumbo iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Marekani imekamilika na tuliizindua. Tuliweka mawe ya msingi ya kujenga barabara ya lami kutoka Namtumbo, Tunduru, Mangaka hadi Mtambaswala kwenye Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Japan. Barabara ya kutoka Mangaka hadi Masasi iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan imekamilika na tuliizindua. Katika barabara ya kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay kimebaki kipande cha kilometa 66 kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay ambacho hakikuwa na mpango wo wote wa kuwekewa lami kwa sasa. Bahati nzuri, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Bibi Tonia Kandiero alitangaza pale Namtumbo kuwa Benki yake itafadhili ujenzi wa barabara hiyo. Mambo sasa yamekamilika.

Kule Masasi mkoani Mtwara na Nachingwea mkoani Lindi tulizindua kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Mbwinji unaomaliza tatizo kubwa la maji kwa miji hiyo kwa miaka mingi ijayo.

Nyumba za Bei Nafuu

Ndugu Wananchi; 
Nikiwa wilayani Mkinga na katika Manispaa ya Songea nilizindua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirila la Nyumba la Taifa (NHC). Nyumba hizo za vyumba viwili na vitatu zinauzwa kwa bei ya shilingi milioni 31 hadi 42. Wenzetu wa NHC walinieleza utayari wa kujenga nyumba zaidi endapo watapatiwa maeneo na Halmashauri za Wilaya na Miji. Walinilalamikia kuwa hawapati ushirikiano wa kutosha kutoka mamlaka husika. Nilipokuwa Mkinga na Songea niliagiza Halmashauri hizo na nyinginezo nchini kutenga maeneo kwa ajili ya NHC na Mifuko ya Hifadhi za Jamii yote ili waweze kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla. 

Hii ni fursa ya aina yake kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kuweza kujipatia nyumba kwa urahisi. Halmashauri zisiwe kikwazo wakati ardhi imejaa tele na kila wakati wanapima viwanja vipya. Jambo lingine zuri waliloniambia viongozi wa NHC ni kwamba zipo Benki ambazo wanashirikiana nazo kutoa mikopo kwa watu wanaonunua nyumba zao. Ni matarajio yangu kwamba uongozi wa Halmashauri zote nchini utaitikia maelekezo yangu na kwamba utatenga maeneo kwa ajili ya mashirika yetu hayo.

Matibabu kwa Wazee

Ndugu Wananchi;
Nilipokuwa wilaya ya Kilindi nilifurahishwa sana na utaratibu wa kuwapatia wazee huduma ya matibabu. Kama mjuavyo Sera ya Afya inataka wazee na watoto wa chini ya miaka mitano watibiwe bure katika hospitali za Serikali. Bahati mbaya vitambulisho wanavyopata wazee vimekuwa havithaminiwi ya kutosha. Kwa sababu hiyo, nafuu wanayostahili kupata imekuwa haipatikani kwa urahisi na wengine huikosa kabisa. 

Katika Wilaya ya Kilindi, Halmashauri ya wilaya imeamua kuwakatia wazee hao Bima ya Afya inayotolewa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na hivyo kuondoa kabisa migogoro inayohusiana na vitambulisho vya wazee vilivyokuwepo kabla. Kwa kuzingatia malalamiko ya mara kwa mara ninayoyapata kutoka kwa wazee kuhusu matibabu, nashauri Halmashauri zote nchini ziige mfano wa Wilaya ya Kilindi. Kama Kilindi wameweza kwa nini wengine washindwe. 

Ndugu Wananchi;
Katika mikoa hii miwili nilipokea taarifa za kutia moyo kuhusu juhudi za wananchi na Serikali katika kupanua fursa za elimu. Vijana wengi wenye umri wa kujiunga na shule za msingi wanafanya hivyo na wale wote wanaofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata fursa ya kwenda sekondari. Hatuna tena tatizo la fursa. Pamoja na mafanikio hayo mazuri, taarifa za wanafunzi wengi kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari, zimenishtua na kunisikitisha sana. 

Katika Mkoa wa Tanga kwa mfano, kati ya wanafunzi 50,921 walioanza darasa la kwanza mwaka 2007 , ni wanafunzi 41,017 tu ndiyo waliofanya mtihani mwaka 2013. Hivyo basi, wanafunzi 9,904 ambao ni sawa na asilimia 19.4 hawakumaliza elimu ya msingi. Kwa upande wa sekondari, katika mkoa wa Ruvuma, kwa mfano, kati ya wanafunzi 18,892 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2010 ni wanafunzi 9,968 sawa na asilimia 52.76 ndiyo waliofanya mtihani wa kidato cha nne. Hivyo basi, wanafunzi 8,924 sawa na asilimia 47.2 hawakumaliza elimu ya sekondari. Taarifa za namna hii nilizipata pia katika ziara zangu ya Mikoa ya Kagera, Geita na Simiyu. Nina kila sababu ya kuamini kuwa hali ni hiyo hiyo kwa Mikoa mingine mingi nchini. Kwa kweli kiwango hiki cha wanafunzi wanaoshindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari ni kikubwa mno. Kinanisikitisha sana, hakikubaliki na hakiwezi kuachwa kiendelee. 

Ndugu Wananchi;
Kwa maoni yangu wazazi, walimu na viongozi wanao wajibu maalumu wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanahudhuria masomo shuleni tangu wanapoanza mpaka wanapomaliza masomo yao. Huu ni wajibu wa lazima na siyo hiari. Ni wajibu wa kisheria. Kwa hiyo, nimeagiza kwamba, wazazi, walimu, Maafisa Elimu wa Wilaya wa Msingi na Sekondari na Kamati husika katika Halmashauri zote nchini ziwajibike ipasavyo kuhakikisha kuwa utoro mashuleni unakomeshwa. Ajenda ya mahudhurio shuleni iwe ni ya kudumu katika vikao vyote vya Halmashauri. 

Kuanzia sasa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ni lazima watoe taarifa za mahudhurio ya wanafunzi kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kila miezi mitatu. Maafisa Elimu wa Wilaya nao watalazimika kutoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri mwezi mmoja baada ya kupokea taarifa hizo. Halmashauri hazina budi kuchukua hatua stahiki za kijamii na kisheria kuhakikisha kuwa watoro wanarudi shuleni. Wazazi wa watoto hao au mtu ye yote atakayebainika kuhusika na utoro huo abanwe ipasavyo. 

Sheria ya Elimu ya 1978 ipo, itumieni kwa ukamilifu kulitatua tatizo hili. Haipendezi kusubiri mpaka miaka saba kwa wanafunzi wa shule ya msingi au miaka minne kwa wanafunzi wa sekondari ipite ndipo taarifa za utoro kwa wanafunzi zitolewe au zijulikane. Lazima ufuatiliaji wa mahudhurio uwe wa mara kwa mara ili hatua za kuzuia ziweze kuchukuliwa mapema. Ninawataka viongozi wa TAMISEMI, Mikoa na Wilaya kuchukua hatua stahiki kudhibiti tatizo hili la utoro na watoto wengi kutokumaliza masomo. Litarudisha nyuma maendeleo ya taifa. 

Umeme Vijijini

Ndugu Wananchi; 
Nilipokuwa mkoani Ruvuma nimezindua ujenzi wa miradi mingi ya umeme vijijini. Kwa mujibu wa miradi hiyo vijiji 309 vitapatiwa umeme kati ya vijiji 509 vya Mkoa huo vinavyohitaji umeme. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo na viongozi wenzake, viongozi na wafanyakazi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo ya kufikisha umeme vijijini. Kwa kweli ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu suala la umeme vijijini kupewa msukumo mkubwa kiasi hiki, kwani kinachofanyika Ruvuma kipo nchi nzima. Nawaomba wananchi wanaofikishiwa umeme wautumie. Hata gharama za kuunganisha umeme zimepunguzwa makusudi, ili watu wengi waweze kumudu kuingiza umeme majumbani na kwenye shughuli za kichumi na huduma.

Mchakato wa Katiba Mpya

Ndugu Wananchi;
Kama tujuavyo, Bunge Maalum la Katiba lililoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014 kupisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi kushughulikia bajeti za Serikali husika, litakutana tena tarehe 5 Agosti, 2014 kuendelea na kazi yake ya kutunga Katiba Mpya. Kwa vile Bunge Maalumu la Katiba halikuweza kumaliza kazi yake ndani ya siku 70 zilizotengwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nimeliongezea Bunge hilo siku 60 kwa ajili ya kukamilisha kazi yake. Nimefanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Sheria hiyo hiyo. 

Hatua Iliyofikiwa Kabla ya Kuahirishwa kwa Bunge

Ndugu Wananchi; 
Itakumbukwa pia kuwa, tarehe 16 Aprili, 2014, baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni na kutoka nje. Wakati wanatoka Bungeni, kazi kubwa ilikuwa imefanyika. Tayari Kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa muungano. Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili. Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonyesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana. 

Baada ya hapo, taarifa ya kila Kamati iliwasilishwa kwenye Bunge zima. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, maoni ya wachache nayo yaliwasilishwa. Kazi iliyokuwa inafuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ni kwa Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa. Baada ya Wajumbe kujadili taarifa hiyo itafuatia kupiga kura ili kuamua kuhusu Sura hizo mbili. Kama yalivyo masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi utafanywa kwa theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano wetu. 

Sababu za Baadhi ya Wajumbe Kususia Bunge Maalumu la Katiba

Ndugu Wananchi;
Sote tumewasikia Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba waliosusia vikao vya Bunge hilo wakielezea sababu zilizowafanya watoke Bungeni. Walitoa matamko kwenye vyombo vya habari na pia katika mikutano ya hadhara waliyoiitisha na kuhutubia sehemu mbalimbali nchini. Sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepo wa kisiasa unavyokwenda.

Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili. Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yo yote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili cho chote. Pili, wametoa sharti la wao kurudi Bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilo kukubaliwa, wamesisitiza kutorudi Bungeni. 

Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba

Ndugu Wananchi;
Mimi nimehusika katika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo. Kwa kweli sikumbuki wakati wo wote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba. 

Mimi siyo Mwanasheria na hivyo nakiri kwamba naweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana ya baadhi ya maneno ya kisheria. Hata hivyo, sikumbuki kuwepo kwa kifungu cho chote katika Sheria kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka hayo. Tangu tulipoyasikia maneno hayo yakisemwa nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba anisaidie. Badala yake naambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria haiakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba ni kubariki Rasimu na siyo kufanya vinginevyo. Nimeambiwa kuwa sheria inasemaTume itaanda Rasimu ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba litatunga Katiba iliyopendekezwa. 

Ndugu Wananchi;
Tarehe 30 Desemba, 2010, nilipozungumzia dhamira yangu ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya nilieleza wazi nia ya kuwepo kwa uwakilishi mpana wa Watanzania katika mchakato huo. Ndiyo maana katika Sheria tukaweka ngazi nnekatika mchakato wa kutunga Katiba. Ngazi ya kwanza ikiwa ya wananchi kutoa maoni yao juu ya kila wanachotaka kijumuishwe katika Katiba ya nchi yao. Ngazi ya pili, ni ya wananchi kupitia wawakilishi wao katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotayarishwa na Tume. 

Ngazi ya tatu inajumuisha wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Sehemu zetu mbili za Muungano, yaani Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi, wakichanganyika na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania kutoka pande zote mbili za Muungano. Hawa ndio wanaounda Bunge Maalumu la Katiba, lenye jukumu la kutunga Katiba inayopendekezwa.

Mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za Mabaraza ya Kutunga Sheria ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa. Ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu lisingetumiwa neno la kutunga Katiba. Hali kadhalika, lisingewepo sharti la kupiga kura na msisitizo wa kupata theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano. Aidha, kama ingekuwa jukumu la Bunge Maalumu ni kubariki tu Rasimu lisingepewa siku 70 za kazi na Rais kupewa mamlaka ya kuongeza siku zaidi kadri aonavyo yeye inafaa.

Ngazi ya nne na ya mwisho, tuliweka kura ya maoni ya wananchi kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba. Kama ingekuwa Rasimu ya Tume haiwezi kubadilishwa hata nukta kwa nini basi tuweke kura ya maoni ya kuwahusisha wananchi wote? 

Ndugu Wananchi;
Tulizibuni ngazi hizi nne kwa dhana kwamba kile ambacho hakikuonekana au hakikuwekwa sawa katika ngazi moja kitaonekana na kurekebishwa katika ngazi inayofuata katika ngazi zile tatu za mwanzo. Na, iwapo Katiba iliyotungwa haitawaridhisha wananchi wanayo haki ya kuikataa. Kwa kufanya hivyo, wananchi ndiyo waliopewa turufu ya mwisho. 

Ndugu wananchi;
Kwa kweli, napata shida kuelewa mkanganyiko unatoka wapi na hasa wale wanaoongoza kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu kuwa ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tena hatua kwa hatua. Nashangazwa zaidi ninapoona wale wale waliotunga Kanuni za Bunge Maalumu ndiyo wanaoongoza kuhoji uhalali wa kile walichokitunga.

Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: "Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti". Mwisho wa kunukuu. 

Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha. Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.

Ndugu Wananchi, 
Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura. 

Kinachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume

Ndugu Wananchi; 
Yapo madai yanayotolewa na kuenezwa na Wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndiyo maana basi wanaweka sharti la kujadiliwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni. Madai haya nayo yananipa taabu kuyaelewa. Ndugu zetu hawa walishiriki siku zote 19 za Kamati 12 zilipokutana kujadili Sura yaKwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Halikadhalika. walikuwepo na kushiriki kwa ukamilifu wakati taarifa za Kamati, tangu ya Kwanza mpaka ya 12,zilipowasilishwa kwenye Bunge zima. Aidha, na wao walishiriki kutoa maoni ya wachache kwa dakika 20 na kutoa ufafanuzi kwa muda wa dakika 30 kwa kila Kamati. Haya maneno ya sasa kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine kabisa ambayo wanadai eti ni ya CCM yanatoka wapi.

Mimi nadhani kuwa huenda katika Kamati kumefanyika marekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo, wawe wakweli kuhusu jambo hilo kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa. Matokeo yake ni kuwafanya wafuasi wao na wapenzi wao na hata watu wengine waamini kuwa kinachojadiliwa siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine tena ni ya CCM. Jambo hilo si kweli na wenyewe wanajua kwamba si kweli ila sijui kwa nini wameamua kupotosha ukweli.

Ndugu Wananchi;
Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao? Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo. 

Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano. Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano. Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.

Nililolisema mwanzoni kabisa mwa mchakato na nalirudia tena leo kwamba, ili tuweze kufanikiwa kupata Katiba Mpya ambayo sote tunaitaka, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa ni jambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana. Ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo sasa katika mchakato wa Katiba.

Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake. Hali kadhalika nampongeza sana Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Mheshimiwa Samwel Sitta, kwa kuitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Bahati mbaya ni kwamba Wajumbe wa vyama vilivyosusia Bunge Maalumu hawakushiriki. Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Sitta hatokata tamaa kuendeleza juhudi za mashauriano na kwamba katika vikao vijavyo na wenzetu hawa watashiriki. 

Ndugu Wananchi;
Hivi karibuni kumekuwepo pia madai yanayoelekeza lawama kwangu. Kwanza nalaumiwa eti kuwa mambo yalikuwa yanaenda vizuri mpaka pale nilipotoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Maalumu ndipo yalipoharibika. Pili nalaumiwa kwamba nawezaje kuikana Rasimu ya Katiba ambayo na mimi ni mmoja wa watu waliotia sahihi katika Rasimu hiyo.

Niruhusuni nianze na hili la pili. Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya yameitafsiri isivyo sahihi yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuandika Rasimu ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepewa kazi tatu kufanya. Kwanza, kupokea Rasimu hiyo na Taarifa ya Tume kutoka kwa Mwenyekiti jambo ambalo lilifanywa tarehe 30 Desemba, 2013. Pili, amepewa kazi ya kuitangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume kwa watu wote kuiona na kuisoma ndani ya siku 30. Alipewa sharti la kuitangaza katika Gazeti la Serikali na vyombo vingine vya habari. Hili nalo lilifanywa hivyo tarehe 22 Januari, 2014.

Ndugu Wananchi;
Katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie sahihi yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume. Sahihi zilizomo ndani ya Rasimu na Taarifa ya Tume ni za Wajumbe wa Tume, kamwe sahihi ya Rais haimo hivyo hawezi kulaumiwa kuwa anaikana sahihi yake. Yeye ametimiza wajibu wake wa kutangaza, akaiweka hadharini kwa umma wa Watanzania kuiona na kusoma Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume vilivyotayarishwa na kutiwa sahihi na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi ya tatu ni kuitisha Bunge Maalumu ambayo nayo imekamilika tangu tarehe 18 Februari, 2014. 

Ndugu Wananchi,
Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwa mara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu. Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato. Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume. Ukweli ni kwamba Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza nilipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi. Napenda watu wasijenge dhana kuwa nilipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yangu. Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo. Sikuiingilia kwa namna yo yote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo. Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu. 

Ndugu Wananchi;
Kuhusu madai kwamba mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo hazina ukweli wo wote. Ni madai yasiyokuwa na msingi. Kwani mimi hasa siku ile nilifanya lipi la ajabu. Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume. Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamoto za miundo ya Serikali mbili na Serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume. Nimetumia takwimu zile zile za Tume. Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume. 

Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo. 

Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu. Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya. Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani. Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao. Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa. Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu. Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali. Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame. Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.

Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania. Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa. Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato. Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?. 

Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita. 

Hitimisho

Ndugu Wananchi;
Mwisho, ni maoni yangu ya dhati kuwa mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba hauna sababu ya kuendelea kuwepo. Naamini hayo yote ambayo Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wanayalalamikia yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge Maalumu la Katiba iliyotengenezwa na Wajumbe wote na wao wakiwemo. Nawasihi waitumie. Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa Chama cha Mapinduzi wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye. Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa. Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa. Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele. 

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] Hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa Tarehe 31 mwezi Julai, 2014"

[wanabidii] HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA TAIFA - 31 JULAI 2014(KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA).

Mchakato wa Katiba Mpya

Ndugu Wananchi;

Kama tujuavyo, Bunge Maalum la Katiba lililoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014 kupisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi kushughulikia bajeti za Serikali husika, litakutana tena tarehe 5 Agosti, 2014 kuendelea na kazi yake ya kutunga Katiba Mpya. Kwa vile Bunge Maalumu la Katiba halikuweza kumaliza kazi yake ndani ya siku 70 zilizotengwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nimeliongezea Bunge hilo siku 60 kwa ajili ya kukamilisha kazi yake. Nimefanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Sheria hiyo hiyo. 

Hatua Iliyofikiwa Kabla ya Kuahirishwa kwa Bunge

Ndugu Wananchi; 

Itakumbukwa pia kuwa, tarehe 16 Aprili, 2014, baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni na kutoka nje. Wakati wanatoka Bungeni, kazi kubwa ilikuwa imefanyika. Tayari Kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa muungano. Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili. Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonyesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana. 

Baada ya hapo, taarifa ya kila Kamati iliwasilishwa kwenye Bunge zima. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, maoni ya wachache nayo yaliwasilishwa. Kazi iliyokuwa inafuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ni kwa Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa. Baada ya Wajumbe kujadili taarifa hiyo itafuatia kupiga kura ili kuamua kuhusu Sura hizo mbili. Kama yalivyo masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi utafanywa kwa theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano wetu. 

Sababu za Baadhi ya Wajumbe Kususia Bunge Maalumu la Katiba

Ndugu Wananchi;

Sote tumewasikia Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba waliosusia vikao vya Bunge hilo wakielezea sababu zilizowafanya watoke Bungeni. Walitoa matamko kwenye vyombo vya habari na pia katika mikutano ya hadhara waliyoiitisha na kuhutubia sehemu mbalimbali nchini. Sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepo wa kisiasa unavyokwenda.

Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili. Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yo yote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili cho chote. Pili, wametoa sharti la wao kurudi Bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilo kukubaliwa, wamesisitiza kutorudi Bungeni. 

Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba

Ndugu Wananchi;

Mimi nimehusika katika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo. Kwa kweli sikumbuki wakati wo wote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba. 

Mimi siyo Mwanasheria na hivyo nakiri kwamba naweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana ya baadhi ya maneno ya kisheria. Hata hivyo, sikumbuki kuwepo kwa kifungu cho chote katika Sheria kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka hayo. Tangu tulipoyasikia maneno hayo yakisemwa nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba anisaidie. Badala yake naambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria haiakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba ni kubariki Rasimu na siyo kufanya vinginevyo. Nimeambiwa kuwa sheria inasemaTume itaanda Rasimu ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba litatunga Katiba iliyopendekezwa. 

Ndugu Wananchi;

Tarehe 30 Desemba, 2010, nilipozungumzia dhamira yangu ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya nilieleza wazi nia ya kuwepo kwa uwakilishi mpana wa Watanzania katika mchakato huo. Ndiyo maana katika Sheria tukaweka ngazi nne katika mchakato wa kutunga Katiba. Ngazi ya kwanza ikiwa ya wananchi kutoa maoni yao juu ya kila wanachotaka kijumuishwe katika Katiba ya nchi yao. Ngazi ya pili, ni ya wananchi kupitia wawakilishi wao katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotayarishwa na Tume. 

Ngazi ya tatu inajumuisha wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Sehemu zetu mbili za Muungano, yaani Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi, wakichanganyika na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania kutoka pande zote mbili za Muungano. Hawa ndio wanaounda Bunge Maalumu la Katiba, lenye jukumu la kutunga Katiba inayopendekezwa.

Mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za Mabaraza ya Kutunga Sheria ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa. Ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu lisingetumiwa neno la kutunga Katiba. Hali kadhalika, lisingewepo sharti la kupiga kura na msisitizo wa kupata theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano. Aidha, kama ingekuwa jukumu la Bunge Maalumu ni kubariki tu Rasimu lisingepewa siku 70 za kazi na Rais kupewa mamlaka ya kuongeza siku zaidi kadri aonavyo yeye inafaa.

Ngazi ya nne na ya mwisho, tuliweka kura ya maoni ya wananchi kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba. Kama ingekuwa Rasimu ya Tume haiwezi kubadilishwa hata nukta kwa nini basi tuweke kura ya maoni ya kuwahusisha wananchi wote? 

Ndugu Wananchi;

Tulizibuni ngazi hizi nne kwa dhana kwamba kile ambacho hakikuonekana au hakikuwekwa sawa katika ngazi moja kitaonekana na kurekebishwa katika ngazi inayofuata katika ngazi zile tatu za mwanzo. Na, iwapo Katiba iliyotungwa haitawaridhisha wananchi wanayo haki ya kuikataa. Kwa kufanya hivyo, wananchi ndiyo waliopewa turufu ya mwisho. 

Ndugu wananchi;

Kwa kweli, napata shida kuelewa mkanganyiko unatoka wapi na hasa wale wanaoongoza kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu kuwa ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tena hatua kwa hatua. Nashangazwa zaidi ninapoona wale wale waliotunga Kanuni za Bunge Maalumu ndiyo wanaoongoza kuhoji uhalali wa kile walichokitunga.

Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: "Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti". Mwisho wa kunukuu. 

Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha. Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.

Ndugu Wananchi, 

Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura. 

Kinachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume

Ndugu Wananchi; 

Yapo madai yanayotolewa na kuenezwa na Wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndiyo maana basi wanaweka sharti la kujadiliwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni. Madai haya nayo yananipa taabu kuyaelewa. Ndugu zetu hawa walishiriki siku zote 19 za Kamati 12 zilipokutana kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Halikadhalika. walikuwepo na kushiriki kwa ukamilifu wakati taarifa za Kamati, tangu ya Kwanza mpaka ya 12, zilipowasilishwa kwenye Bunge zima. Aidha, na wao walishiriki kutoa maoni ya wachache kwa dakika 20 na kutoa ufafanuzi kwa muda wa dakika 30 kwa kila Kamati. Haya maneno ya sasa kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine kabisa ambayo wanadai eti ni ya CCM yanatoka wapi. 

Mimi nadhani kuwa huenda katika Kamati kumefanyika marekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo, wawe wakweli kuhusu jambo hilo kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa. Matokeo yake ni kuwafanya wafuasi wao na wapenzi wao na hata watu wengine waamini kuwa kinachojadiliwa siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine tena ni ya CCM. Jambo hilo si kweli na wenyewe wanajua kwamba si kweli ila sijui kwa nini wameamua kupotosha ukweli.

Ndugu Wananchi;

Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao? Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo. 

Ndugu Wananchi;

Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano. Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano. Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.

Nililolisema mwanzoni kabisa mwa mchakato na nalirudia tena leo kwamba, ili tuweze kufanikiwa kupata Katiba Mpya ambayo sote tunaitaka, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa ni jambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana. Ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo sasa katika mchakato wa Katiba.

Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake. Hali kadhalika nampongeza sana Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Mheshimiwa Samwel Sitta, kwa kuitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Bahati mbaya ni kwamba Wajumbe wa vyama vilivyosusia Bunge Maalumu hawakushiriki. Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Sitta hatokata tamaa kuendeleza juhudi za mashauriano na kwamba katika vikao vijavyo na wenzetu hawa watashiriki. 

Ndugu Wananchi;

Hivi karibuni kumekuwepo pia madai yanayoelekeza lawama kwangu. Kwanza nalaumiwa eti kuwa mambo yalikuwa yanaenda vizuri mpaka pale nilipotoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Maalumu ndipo yalipoharibika. Pili nalaumiwa kwamba nawezaje kuikana Rasimu ya Katiba ambayo na mimi ni mmoja wa watu waliotia sahihi katika Rasimu hiyo.

Niruhusuni nianze na hili la pili. Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya yameitafsiri isivyo sahihi yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuandika Rasimu ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepewa kazi tatu kufanya. Kwanza, kupokea Rasimu hiyo na Taarifa ya Tume kutoka kwa Mwenyekiti jambo ambalo lilifanywa tarehe 30 Desemba, 2013. Pili, amepewa kazi ya kuitangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume kwa watu wote kuiona na kuisoma ndani ya siku 30. Alipewa sharti la kuitangaza katika Gazeti la Serikali na vyombo vingine vya habari. Hili nalo lilifanywa hivyo tarehe 22 Januari, 2014.

Ndugu Wananchi;

Katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie sahihi yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume. Sahihi zilizomo ndani ya Rasimu na Taarifa ya Tume ni za Wajumbe wa Tume, kamwe sahihi ya Rais haimo hivyo hawezi kulaumiwa kuwa anaikana sahihi yake. Yeye ametimiza wajibu wake wa kutangaza, akaiweka hadharini kwa umma wa Watanzania kuiona na kusoma Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume vilivyotayarishwa na kutiwa sahihi na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi ya tatu ni kuitisha Bunge Maalumu ambayo nayo imekamilika tangu tarehe 18 Februari, 2014. 

Ndugu Wananchi,

Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwa mara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu. Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato. Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume. Ukweli ni kwamba Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza nilipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi. Napenda watu wasijenge dhana kuwa nilipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yangu. Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo. Sikuiingilia kwa namna yo yote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo. Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu. 

Ndugu Wananchi;

Kuhusu madai kwamba mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo hazina ukweli wo wote. Ni madai yasiyokuwa na msingi. Kwani mimi hasa siku ile nilifanya lipi la ajabu. Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume. Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamoto za miundo ya Serikali mbili na Serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume. Nimetumia takwimu zile zile za Tume. Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume. 

Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo. 

Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu. Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya. Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani. Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao. Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa. Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu. Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali. Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame. Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.

Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania. Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa. Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato. Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?. 

Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita. 

Hitimisho

Ndugu Wananchi;

Mwisho, ni maoni yangu ya dhati kuwa mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba hauna sababu ya kuendelea kuwepo. Naamini hayo yote ambayo Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wanayalalamikia yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge Maalumu la Katiba iliyotengenezwa na Wajumbe wote na wao wakiwemo. Nawasihi waitumie. Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa Chama cha Mapinduzi wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye. Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa. Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa. Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele. 

Mungu Ibariki Afrika!

Mungu Ibariki Tanzania!

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA TAIFA - 31 JULAI 2014(KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA)."

[wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,
DAR ES SALAAM, ALHAMISI, 31 JULAI 2014 SAA 5.00 ASUBUHI.

Ndugu waandishi wa habari,

Kama mnavyofahamu Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba (BMK) wanaotetea kuheshimiwa kwa maoni ya Wananchi katika mchakato wa kuandika Katiba maarufu kwa jina la UKAWA- Umoja wa Katiba ya Wananchi walitoka nje ya Bunge hilo tarehe 16 April 2014.

Sababu ya msingi iliyotutoa kwenye BMK ni mkakati uliokuwa ukitekelezwa na Wajumbe wa BMK wa CCM kupuuza maoni ya wananchi yaliyokusanywa na kuratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu mwenyekiti Jaji Agostino Ramadhani. Rasimu ya Katiba inapendekeza Muundo wa Muungano wa Shirikisho yenye Serikali Tatu. Kama waraka wa CCM unavyoeleza "Muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi." CCM wameukataa Muundo wa Muungano uliopendekezwa na Tume, na badala yake wanataka Muundo wa Serikali mbili ambao haujafanyiwa utafiti, haujapendekezwa na wananchi walio wengi, uliojaa na matattizo lukuki yasiyotatulika tangu enzi za uhuru na ambao haujapendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba. Kwa sababu aina ya muundo wa muungano ndiyo moyo wa rasimu ya katiba(kwa tafsiri ya CCM), ukiunyonga Moyo wa Rasimu hautakuwa na Rasimu ya Katiba inayotokana na maoni ya wananchi. UKAWA tunatetea maoni ya Wananchi yaheshimiwe na tumetoa wito kila mara kuwa hii ndiyo njia bora ya kutufanya turidhiane.

Ikumbukwe kuwa bunge la katiba halikuanzisha mchakato wa katiba, linakamilisha moja ya hatua muhimu za kupata katiba, tayari hatua mbili muhimu zimeshafanyika, maoni ya wananchi yametolewa na tume imetumia maoni hayo pamoja na rejea zingine na historia mbalimbali na imetuletea rasimu ya katiba inayotokana na mambo hayo. Bunge Maalum la Katiba halina uwezo na kibali cha kuvunja misingi mikuu ya maoni ya wananchi na kazi ya tume, kuvunja misingi mikuu "moyo wa rasimu" ni sawa na kuanzisha mchakato mwingine wa katiba na ni sawa na kuwa juu ya maoni na matakwa ya wananchi – UKAWA tumekataa kuwa sehemu ya uchakachuaji huu wa hali ya juu.

Ndugu waandishi wa habari,

Tunapenda ifahamike kuwa, UKAWA pia tulikwazwa na lugha za ubaguzi, uchochezi, matusi na kejeli zilizokuwa zikiporomoshwa na baadhi ya Wajumbe wa CCM ndani na nje ya BMK. Michango mingi ya Wajumbe wa CCM wa Bunge Maalum ilikuwa ya kumkejeli na kumdhalilisha Jaji Joseph Sinde Warioba na kauli za kibaguzi dhidi ya Waarabu, Wapemba na Wahindi.

Lugha za kibaguzi na kichochezi pia zilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi alipokuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika ibada ya kumsimika Askofu wa Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma. Mhe. Lukuvi aliwataka wananchi waliohudhuria ibada hiyo kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi. Katika hotuba yake katika kanisa la Methodist Mhe. Lukuvi aliendelea kuwachochea waumini aliposema kuwa "Serikali tatu zikipita ni wazi kuwa hata makanisa yatafungwa kwani nchi haiwezi kuwa na amani tena."

Lukuvi alisema Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu. Serikali haikuchukua hatua yeyote kukanusha na kumuwajibisha Mhe. Lukuvi.

Hivi karibuni kumekuwa na miito mbalimbali ambayo imetolewa kututaka sisi tulioko katika Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA), kurejea bungeni. Katika Baraza la IDD ambako Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi wito wa UKAWA kurudi bungeni ulisisitizwa.

Watu wengi wametoa kauli na hasa baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini nchini, kututaka turejee bungeni ili kuendelea na mchakato wa kuandika katiba mpya. Tunasema, tumewasikia na tunaheshimu kauli zao.

Tunatambua kuwa viongozi wa kidini ni watu wenye heshima na nafasi ya pekee katika jamii yetu. Ni watu waliopewa wajibu wa kutuongoza tukiwa hapa duniani na hata tukiondoka duniani. Kwa hiyo, napenda kuwahakikishieni kabisa kuwa UKAWA inaheshimu sana miito na ushauri wao.

Ndugu waandishi wa habari,

Pamoja na heshima hiyo, tunapenda pia waelewe haya yafuatayo:

Kwanza, UKAWA uliondoka bungeni, pamoja na mengine, kupinga njama za kuhujumu mchakato wa Katiba Mpya. Tulipinga kudharauliwa maoni ya wananchi kama yalivyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Tumepinga Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupuuza maoni ya wananchi na kutaka kuingiza maoni yake, kinyume cha kanuni na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Pili, tuliondoka bungeni kupinga lugha ya ubaguzi, uchochezi, matusi na kejeli. Baadhi ya kauli hizi tulizikabili ndani ya bunge na kuonya wenzetu kuacha lugha hizo na badala yake watumie jukwaa hilo kusaidia upatikanaji wa katiba mpya. Hatukusikilizwa.

Ninyi ni mashahidi jinsi wajumbe wa CCM walivyoporomosha matusi makubwa na tuhuma nzito dhidi ya Tume ya Jaji Warioba. Baadhi ya wajumbe waliwaita wajumbe wa tume hii Eti, "wasaliti wa Baba wa Taifa; wazee wanaosubiri kufa; na watu wasiokuwa na uzalendo bali wana ajenda binafsi."

Tatu, tuliondoka bungeni baada ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kushindwa kuwadhibiti wajumbe wanaotumia lugha ya ubaguzi, uchochezi, matusi na kejeli na kuendesha vikao vya bunge hilo kwa upendeleo. Mwenyekiti ameliendesha Bunge hilo kibabe. Ameshiriki kubadili ratiba na mtiririko wa matukio bungeni. Mwenyekiti wa Bunge la Katiba alivunja kanuni kwa kumtanguliza Mwenyekiti wa Tume kuwasilisha Rasimu kabla Bunge kusikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi. Amebadili Kanuni za Bunge la Katiba na sasa ametishia kufanya hivyo tena.

Nne, tuliondoka bungeni baada ya kuona waziri mmoja mwandamizi wa serikali ya Rais Kikwete, William Lukuvi, akiingia kanisani na kufanya uchochezi. Alidai Zanzibar inataka serikali tatu ili iwe huru kuanzisha Serikali ya Kiislamu na kuwarejesha Waraabu visiwani humo. Waziri huyu alikuwa amekwenda Kanisani kumwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Hadi tunaondoka na mpaka sasa, hakuna mamlaka yoyote iliyo juu ya Lukuvi ambayo imechukua hatua angalau hata ya kuomba radhi. Waziri Mkuu alikuwa na fursa adhimu kama mgeni rasmi katika Baraza la Idd kuomba radhi lakini hakufanya hivyo.

Tunawashukuru sana viongozi wa dini waliotoa matamko kulitaka Bunge Maalum la Katiba liheshimu maoni ya wananchi.

Ndugu waandishi wa habari,

Pamoja na kuwaheshimu viongozi wote wa dini, tumesikitishwa na matamshi ya baadhi yao kama yale yaliyotolewa katika Baraza la Idd kututaka UKAWA turejee bungeni, huku wakinyamazia matendo yaliyofanyika. Waziri Mkuu aliyekuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd ndiye aliyewakilishwa na Waziri Lukuvi alipotoa alipotoa kauli za kibaguzi na kichochezi katika kanisa la Methodist mjini Dodoma.

Leo ni zaidi ya miezi miwili tangu Bunge hili liahirishwe. Hatujamsikia kiongozi yoyote wa kidini (wale) wanaotutaka turudi bungeni, wakikemea au kutoa wito kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutumia haki, hekima na usawa, katika kuendesha mijadala bungeni.

Hatujasikia viongozi wa dini wanaotaka UKAWA warudi Bungeni wakitoa wito kwa wabunge wa chama tawala kurejea kwenye ajenda kuu na kuacha kashfa dhidi ya Tume. Kimya chao katika suala hili, kimechangia kukiongezea chama tawala kibri na dharau dhidi ya wananchi.

Vilevile, hatujawasikia viongozi wa madhehebu ya kidini wakimkemea Lukuvi wala Waziri Mkuu Pinda kuhusu kilichotokea kanisani Dodoma.

Badala yake, tumeendelea kuona viongozi wa dini wakikutana na viongozi wa serikali na chama tawala, bila jitihada za viongozi hao kukutana na UKAWA. Miito ya viongozi hawa inaelekezwa upande mmoja ikifumbia macho upande wa pili.

Sisi tunaamini viongozi wetu wa kiroho wanao uwezo wa kuangalia pande zote mbili na kutoa miito yenye ukweli, usawa na haki. Tunawasishi kabla ya kututaka kurejea bungeni, wangetumia busara hiyohiyo kutusikiliza na sisi kama ambavyo wanawafuata viongozi wa CCM, ofisi ndogo ya Lumumba na Ikulu jijini Dar es Salaam, kuwasikiliza.

Msimamo wa UKAWA uko wazi, tunataka maoni ya wananchi yaheshimiwe na Bunge Maalum la Katiba.

Mungu Ibariki Tanzania!

Imetolewa na;

-----------------------------------
Freeman Alkael Mbowe(MB),
Mwenyekiti - CHADEMA

---------------------------------------
Ibrahim Haruna Lipumba(MBMK)
Mwenyekiti – CUF – Chama Cha Wananchi,

--------------------------------------
James Francis Mbatia(MB)
Mwenyekiti – NCCR MAGEUZI.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "[wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI."