Habari inasikitisha kweli hasa kwa watoto,
Lakini TAMWA sio kuandika tu hapa ,twambieni mmefanya nini kumsaidia huyu mama?! Maana mmeweka habari hii hapa kuleta mjadala ambao hautakuwa tija kwa waathirika.
--------------------------------------------
On Thu, 9/1/14, Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Mahakama Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya mali
To: "uwazi@hotmail.com" <uwazi@hotmail.com>, Haki.yako@gmail.com, "Henry Mdimu" <mdimuz@gmail.com>, "Jestina George" <jestinageorge@googlemail.com>, "johnbukuku@gmail.com" <johnbukuku@gmail.com>, "Josephat Lukaza" <josephat.lukaza@gmail.com>, "Othman Michuzi" <othmanmichuzi@gmail.com>, "Ahmad Michuzi" <amichuzi@gmail.com>, "GSengo ." <albertgsengo@yahoo.com>, "Subi Nukta" <subi@wavuti.com>, "Emmanuel Shilatu" <pbuyegu2@gmail.com>, "Sigfred Kimasa" <kingkif07@gmail.com>, "info@dewjiblog.com" <info@dewjiblog.com>, "Francis Dande" <dande15us@gmail.com>, "Grace Mkojera" <gmkojera@gmail.com>, "francis godwin" <francisgodwin2004@yahoo.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Maggid Mjengwa" <mjengwamaggid@gmail.com>
Date: Thursday, 9 January, 2014, 8:16
Mahakama
Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya
mali
Na Thehabari.com,
Nkasi
MAHAKAMA ya
Mwanzo Namanyere wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa imeingia
kwenye lawama kwa kitendo cha kuvunja ndoa
iliyokuwa na mgogoro bila kugawanya mali iliyochumwa kipindi
cha
wanandoa wakiishi kama mke na mume.
Bi. Maria
Tarafa (25) mkazi wa Kijiji cha Isale ambaye ni mmoja wa
wanandoa hao ametoa
malalamiko hayo hivi mjini hapa alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari
hizi, huku akiituhumu mahakama hiyo haijampa nafasi ya
kujitetea kama akiwa
kama mlalamikiwa.
Alisema
mumewe, Ndebile Kazuri (31) alikuwa akitaka kumtelekeza yeye
na watoto wao
wanne kwa muda mrefu kwa kutaka kuivunja ndoa yao halali
kinyemela, lakini
alikuwa akimshinda kila alipoitisha vikao vya wazazi na
viongozi wa vijiji na kata
akitaka kuivunja ndoa hiyo bila kutoa haki kwa mama na
watoto (huduma).
Alisema mume
huyo wameishi naye kama mtu na mke wake tangu mwaka 2003 na
kufanikiwa kupata
watoto wanne ambao walikuwa wakiishi eneo moja na baba yao
huku Kazuri naye akiishi
na mwanamke mwingine eneo hilo ambaye pia wamezaa
naye.
"…Licha ya
kuishi naye amekuwa akinipiga na kunifukuza niondoke kwake
na watoto wangu
nirudi kwetu, lakini mimi nimekataa mara zote na kumwambia
nitakuwa tayari
kuondoka baada ya kupata haki zangu na watoto kuhakikisha
wako katika malezi
mazuri," alisema Bi. Tarafa.
Alisema
mumewe aliamua kwenda baraza la kata na kuomba barua ili
aende mahakamani
kuiomba mahakama ivunje ndoa yake na mkewe aondoke na kurudi
kwa wazazi wake.
Kazuri alifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo, Namanyere
Wilaya ya Nkasi
Oktoba 28, 2013, kesi namba 26/2013 iliyosikilizwa na Hakimu
aliyetajwa kwa
jina la B. Stanley.
Alisema
mahakama ilimwita kwa mara ya kwanza na kumsomea maelezo ya
mdai (mumewe) ya
kuomba ndoa yao ivunjwe yeye alipinga na kutaka awasilishe
maelezo yake lakini
mahakama iligoma kwa madai ilichoitaji kwa mlalamikiwa ni
kujibu kama yupo
tayari au la na si kupata maelezo. "…Niliomba niliomba
nipewe nafasi ya
kuzungumza upande wangu lakini walikataa na kuniambia; mama
tumekuja kusikiliza
kesi ya talaka na si maelezo mengine, we sema kama upo
tayari au la…," alisema.
Aliongeza
kuwa Novemba 18, 2013 baada ya yeye kukiri kuwa yupo tayari
kuachana na mume
huyo iwapo atapata haki zake na watoto, mahakama ilivunja
ndoa hiyo na kuamuru
aondoke na watoto wawili bila kueleza namna watakavyo pata
huduma toka kwa baba
yao.
Alisema
mahakama iliamuru watoto wa miaka 7 na 9 watabaki kwa baba
yao nay eye kuondoka
na wawili wenye miaka miaka chini ya saba. Aliongeza kuwa
Mahakama iliamuru
apewe magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo tulilima pamoja
na bati 7.
"…Mume wangu
alidanganya kuwa hatuna mali pale mahakamani, mimi nikaeleza
ni uongo kwani
tuna ng'ombe zaidi ya 127, buzi 30, nyumba mbili pale
kijijini Isale pamoja na
hekari zaidi ya 70 za ardhi…hawakunisikiliza pale
mahakamani. Ukweli ni kwamba
tunamali hizo ambazo tulichuma tukiwa wote," alisema Bi.
Tarafa.
Mwandishi wa
habari hii amebahatika kupata nakala ya hukumu ya kesi hiyo,
ambayo kweli
haikuonesha namna watoto wanaobaki kwa mama watahudumiwaje
licha ya kuamuru
kuwa watabaki na mamayao.
Akizungumzia
sakata hilo, Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Wilaya, Ramadhan Rugemalira alisema mama huyo
anahaki ya kufungua
kesi ya madai kuomba mgawanyo wa mali na matunzo kwa watoto
endapo hakuridhika
na hukumu iliyotolewa kwa shauri hilo. "…Anachotakiwa
kuomba mahakamani kwa
sasa ni mgawanyo wa mali, kwamba katika kesi yao ambayo
mahakama ilivunja kuna
mali ambazo mahakama haikuzizungumzia kabisaa lakini na mimi
(mke) ninahaki na
mali hizo, unaona…ataleta ushahidi kama ng'ombe hao wapo
kama kuna ardí na
nini…hivyo huyo mwanaume ataitwa na kesi kusikilizwa,"
alisema Rugemalira.
Hata hivyo, Hakimu
Rugemalira alisema huenda mtoa hukumu wa mwanzo aliteleza
kwa kitendo cha
kutoainisha namna watoto wanaobaki kwa mama watalelewa vipi.
Alisema pamoja na
hayo bado mama huyo anahaki ya kufungua madai mengine kudai
haki hizo.
Tulipo zungumza na
Kazuri juu la mali ambazo mke anazilalamikia, yaani
ng'ombe 127, nyumba 2, mbuzi 30 na ardhi hekari 70
alisema mali hizo
alipewa na babayake wakati anaanza maisha hivyo bado ni mali
ya babayake ambaye
alidai yupo hadi sasa. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa
habari hizi
umebaini baba yake na Kazuri (yaani Kazuri Moshi) ni
marehemu alifariki tangu
Machi 2004 na mali zake kugawiwa kwa watoto wake.
Hata hivyo mtalaka wake
Kazuri anasema walipewa ng'ombe za urithi toka kwa baba
yake na Kazuri zikiwa
65 lakini wamezizalisha hadi kufikia idadi zilipo sasa
pamoja na mashamba na
nyumba lakini anashangaa mzazi mwenzake anamdhulumu kila
kitu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa
ushirikiano na TAMWA
___________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la
Thehabari.com
Mail address:-
mushi@thehabari.com/
jomushi79@yahoo.com/
info@thehabari.com
Mobile:- 0717
030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment