Tuesday 17 December 2013

[wanabidii] Rais Kikwete amteua Omari J. Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013. Eng
Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.

 "Mwisho"

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

16 Desemba, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment