Monday 16 December 2013

Re: [wanabidii] Taarifa ya Reginald A Mengi kuhusu yanayosemwa juu yake

Nimepata wepesi kuelewa kwa nini Mengi amelazimika kutoa maelezo haya.
Lakini nafikiri katumia muda wake bure kuyasema.
Ni dhahiri kuwa alichokisema Waziri Mhongo alikuwa hakielewi.
Ni katika kipindi hiki ambacho CCM na Bunge vimemkalia rais kooni kuhusu mawaziri mizigo.
Kwamba waziri hajamuelewa Mengi kuwa maneno ya mengi kuhusu watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi kuwa
Mengi anatetea maslahi ya watanzania kuliko yeye binafsi ni dalili nyingine ya umzigo wa waziri huyu kwa Rais na watanzania kwa ujumla. Hivi Waziri aliposema Mengi anatafuta maslahi yake binafsi aliamini kuwa watu wenye akili watamuamini????
Wote tumekuwa tukimsikia Mengi na kuyaona matendo yake. Kwa sehemu tunauona utajiri wake.
Ni mtu gani anaweza kufikiri kuwa Mengi anatetea maslahi yake katika kutamka mara kwa mara kuwa watanzania washirikishwe uchumi isipokuwa waziri mzigo???
Waziri wa namna hii anawezaje kuendelea kuwepo na tufikiri kuwa Taifa linaweza kunufaika na raslimali zake??
Shida kweli
 

From: Pauline Mengi <paulinemengi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, December 15, 2013 6:02 PM
Subject: [wanabidii] Taarifa ya Reginald A Mengi kuhusu yanayosemwa juu yake

1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee  kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.

2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha
kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba: 
 
 "Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu."
  
4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla. 

5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.

8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu. 

Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment