Sunday 15 December 2013

Re: [wanabidii] Taarifa ya Reginald A Mengi kuhusu yanayosemwa juu yake

Prof wa geology alitoa alichoita fact and figure, ningetegemea taarifa hii ingekuwa na fact kama hao washirika ni akina nani wanazalisha kiasi gani wanalipa kodi kiasi gani wanatumia mitambo gani au wanatumia vijana maarufu kama nyoka, mhandisi wa migodi mtanzania analipwa kati ya 3m na 15m kwa mwezi, yeye wakwake anawalipaje? Budget yake ya csr ikoje? Mengi anakipindi cha malumbano ya hoja kupitia itv amwite prof na team yake nae aandae team yake walumbane tujue ukweli.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Pauline Mengi <paulinemengi@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, December 15, 2013 7:02:23 AM GMT-0800
Subject: [wanabidii] Taarifa ya Reginald A Mengi kuhusu yanayosemwa juu yake

1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata
nafasi ya kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini
ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.

2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta
binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe.
Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye
kikao cha
kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa
Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:

"Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya
raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu."

4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa
kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.

5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu
kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa
takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.

6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi
mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata
kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.

7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya
kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya
kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye
Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic
Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania
katika rasilimali zao.

8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa
kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa
Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana
katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi
wetu.

Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment