Sunday 22 December 2013

Re: [wanabidii] Braza Airtel Money Majanga


Kaka Pole sana kwa mikasa ya Airtel Money. Hata mimi yalinipata nikiwa hapa hapa DAR. Kuna mtu alikuwa ananunua mazao sehemu za Matombo Morogoro. Sehemu hiyo mtandao unaopatikana ni maarufu Airtel. Nilijaribu kwenda kwa wakala, nikazunguka karibu Sinza na Mikocheni yote wakala wanasema hawana pesa. Ukiwauliza kwa nini wote hawana float wanasema wanapata hasara kwa vile comission ni ndogo. Ilinibidi niende CRDB kuweka pesa kwa namba ya Wakala wa Matombo, ndipo pesa hizo zikaenda. Ilinibidi kwa muda wa wiki nzima niwe nakwenda kufoleni benki kama vile na mimi ni Wakala.




Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

From: Suleiman Serera <sellyserera@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 23 Dec 2013 01:33:42 +0800
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Braza Airtel Money Majanga

Pole sana kaka. Vya bure kweli gharama!

On Dec 22, 2013 8:19 PM, "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com> wrote:
Braza, Airtel Money Majanga!
Hakatwi mtu hapa, Mungu atusamehe sana. Naangalia katika kibindo
changu nagundua kuna laki mbili na ushehe na kwa kuwa nilikuwa na
safari ya kuelekea Moshi natafuta njia iliyo salama ya kuhifadhi fedha
hizo.
Kama ilivyo desturi ya binadamu kuvutiwa na maigizo yanayoshamiri
katika vyombo vya habari na pia unyonge wa binadamu kuitikia mbiu za
migambo zinazolia kila mara, basi nilichukua kiasi hicho cha fedha na
kuziweka katika akaunti yangu ya Airtel Money aka Zain zamani,
kichwani nikiwa na tumaini kuwa fedha hizo nitaweza kuzitumia kama
nilivyopanga pale nitakapo taka fanya hivyo.
Nilianza safari yangu kama kawaida kwanza nilifika Dar es Salaam
salama salimini na kukamlisha lile lililonipeleka huko kisha kuelekea
Moshi, Kilimanjaro. Shekhe!nikiwa Moshi baada ya majuma mawili,
naangalia mfuko wangu naona hauna kitu, nimechacha ile mbaya
naukumbuka wimbo wa O.S.S maladhi yote ugua lakini kuchacha usiombee.
Ahmadi kibindoni! baada ya kitambo kidogo nikakumbuka kibindoni kwangu
nina fedha nimeweka .
Nikajongea jirani na kibanda cha Airtel Money nikifuata kwa umakini
kabisa taratibu za kutoa fedha bila ya kukosea maana taratibu zao
zinahitaji mtu ambaye akuogopa umande akiwa mdogo huku shule na kama
hukusoma lo umeumia mara naambiwa umekosea Pin! nikajaribu kila njia
nimekosea lo salahe! Namuuliza wakala hapa vipi? ananiambia hawa jamaa
wa Aitel Money braza majanga! wanasumbua sana mara nyingi tatizo hilo
linatokea , pole.
"Jana kaja mama hivyo hivyo , labda nenda pale jirani utakuta kagorofa
kadogo kuna ofisi yao , lakini sidhani kama watakusaidia, watakwambia
pini hainzi na 1 mara 2 mara namba zinazofanani hazifuatani ilimradi
pesa yako ikae muda mrefu kwao." Ananidokeza kijana ambaye ni wakala
wa kutoa fedha huku akiendelea kuwahudumia wateja mjini Moshi ambapo
anatoa huduma ya uwakala wa pesa kwa kampuni zaidi ya moja.
Nateremka kidogo mjini Moshi nakutana na msikiti na upande wa pili
pana gorofa dogo napanda ngazi zilizozooofu sana kwa woga wa kuanguka
nashikilia mbao za pembeni nafika ofisi ya Airtel Kilimanjaro naeleza
shida yangu kwa kijana mwembamba. Kwanza anaomba kitambulisho changu
kisha anasema utapigiwa simu ."Unajua hapa Moshi tupo sisi ofisi kuu
ipo Arusha kwa hiyo utapigiwa simu." anasema kwa upole
Anayesubiri lazima awe na matumaini kwa kile anachokingoja ilikuwa
jumamosi hiyo nikasubiri sikupata jawabu huku nikipiga simu ya huduma
kwa wateja, ahadi tele na majibu yasiyo na ukweli yalitolewa. Nafsini
nikisema jambo gani limenisababisha niweke pesa zangu kwenye simu
yangu ya Airtel.
Jumamosi , kimya, jumapili nayo kimya Jumatatu kimya! Mateso na
maumizu ya Airtel Money hayo. Nikawapigia simu jamaa zangu wakanitumia
pesa kupitia line yangu ya mtandao wa Tigo na kupata pesa angalau
zilinifikisha Dar es Salaam siku ya pili nikafika makao Makuu ya
Airtel niweze kutatuliwa tatizo langu.
Hapo awali nikiwa Moshi, nakutana na kijana mmoja ambaye ni miongoni
mwa wanafunzi wangu namuelezea tatizo lililonikuta nayeye ananiambia
kuwa Airtel Money wana matatizo ni vizuri kutumia mitandao mingine
vinginevyo utaaibika mwalimu.
Asubuhi yake ya tarehe 3 Disemba mwaka huu nafika makao makuu nakutana
na mama mrefu mwenye  mwili uliojengeka mwenye majibu ya haraka
yanayokatisha tamaaa Naelezea tatizo langu lakini msaada nakosa kabisa
, narudi mapokezi nakuomba kumuona Afisa Uhusiano au Legal Officer wao
nikiwa hapo kwa saa moja nzima bila jibu bila kujari safri yangu ndefu
kutoka Kilimanajro mpaka Dar es Salaam kufuatilia pesa yangu.
Gafla, anakuja kijana mwingine akivalia fulani nyekundu yenye
maandishi meupe akisema mzee una shida gani nikamuelekeza kwa muda
akakiomba kitambulisho changu na kunitatulia tatizo langu mara baada
ya kupokea mikwara ya mama mrefu ambaye alijitambulisha kuwa yeye
ndiye meneja, aha ha ha ha Meneja wa Mikwara Airtel wa eneo hilo, lo !
laki mbili zinanitoa jasho .
Nilitoa fedha zangu kwenye akaunti yangu zote na kesho yake kurudi
kwangu na pesa zangu mfukoni nikiwa nimeingia hasara ya madeni na
gharama za usafiri kutoka Moshi hadi Dar
Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idd majuma matatu baadaye nachukua fedha
kutoka katika akaunti  yangu ya Tigo kwa wakala anaweka katika Airtel
money laki tano na ushehe. Duu ile kuweka kiasi hicho cha fedha longo
longo zile zile mara umekosea pin , mara utafungiwa baada ya kujaribu
mara sita mara akaunti yako imefungiwa.
Leo hii ni siku ya tatu na niliyetaka kumtumia fedha bila ya kukatwa
nimemuweka njia panda hajapata fedha, uaminifu juu yake umepungua na
bado hakuna jibu la msaada nililopewa na kampuni hii ya simu. Huku
wakiwa na idara ya huduma kwa wateja ambayo binafsi mimi ninasema hii
ni huduma ya usumbufu kwa wateja.
Je, sasa niianze safari ya kuelekea Dar na kwa pesa zipi? Ama kweli
bure gharama. Kumbe mbiu zote za mgambo hazina ukweli.
Wasalaaam ndugu yenu Adeladius Makwega
+255688905109

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment