Sunday 22 December 2013

Re: [wanabidii] Braza Airtel Money Majanga

Makwega,
 
Pole yaliyokupata. Nimefurahia kusoma habari yako ambayo inavutia kusoma kutokana na vikolombwezo vya lugha. Kama riwaya fulani vile!
Kweli bure ghali sana!


On Sunday, 22 December 2013, 18:17, Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com> wrote:
Wee kwanini unarudia kosa?


On 22/12/2013, Suleiman Serera <sellyserera@gmail.com> wrote:
> Pole sana kaka. Vya bure kweli gharama!
> On Dec 22, 2013 8:19 PM, "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com>
> wrote:
>
>> Braza, Airtel Money Majanga!
>> Hakatwi mtu hapa, Mungu atusamehe sana. Naangalia katika kibindo
>> changu nagundua kuna laki mbili na ushehe na kwa kuwa nilikuwa na
>> safari ya kuelekea Moshi natafuta njia iliyo salama ya kuhifadhi fedha
>> hizo.
>> Kama ilivyo desturi ya binadamu kuvutiwa na maigizo yanayoshamiri
>> katika vyombo vya habari na pia unyonge wa binadamu kuitikia mbiu za
>> migambo zinazolia kila mara, basi nilichukua kiasi hicho cha fedha na
>> kuziweka katika akaunti yangu ya Airtel Money aka Zain zamani,
>> kichwani nikiwa na tumaini kuwa fedha hizo nitaweza kuzitumia kama
>> nilivyopanga pale nitakapo taka fanya hivyo.
>> Nilianza safari yangu kama kawaida kwanza nilifika Dar es Salaam
>> salama salimini na kukamlisha lile lililonipeleka huko kisha kuelekea
>> Moshi, Kilimanjaro. Shekhe!nikiwa Moshi baada ya majuma mawili,
>> naangalia mfuko wangu naona hauna kitu, nimechacha ile mbaya
>> naukumbuka wimbo wa O.S.S maladhi yote ugua lakini kuchacha usiombee.
>> Ahmadi kibindoni! baada ya kitambo kidogo nikakumbuka kibindoni kwangu
>> nina fedha nimeweka .
>> Nikajongea jirani na kibanda cha Airtel Money nikifuata kwa umakini
>> kabisa taratibu za kutoa fedha bila ya kukosea maana taratibu zao
>> zinahitaji mtu ambaye akuogopa umande akiwa mdogo huku shule na kama
>> hukusoma lo umeumia mara naambiwa umekosea Pin! nikajaribu kila njia
>> nimekosea lo salahe! Namuuliza wakala hapa vipi? ananiambia hawa jamaa
>> wa Aitel Money braza majanga! wanasumbua sana mara nyingi tatizo hilo
>> linatokea , pole.
>> "Jana kaja mama hivyo hivyo , labda nenda pale jirani utakuta kagorofa
>> kadogo kuna ofisi yao , lakini sidhani kama watakusaidia, watakwambia
>> pini hainzi na 1 mara 2 mara namba zinazofanani hazifuatani ilimradi
>> pesa yako ikae muda mrefu kwao." Ananidokeza kijana ambaye ni wakala
>> wa kutoa fedha huku akiendelea kuwahudumia wateja mjini Moshi ambapo
>> anatoa huduma ya uwakala wa pesa kwa kampuni zaidi ya moja.
>> Nateremka kidogo mjini Moshi nakutana na msikiti na upande wa pili
>> pana gorofa dogo napanda ngazi zilizozooofu sana kwa woga wa kuanguka
>> nashikilia mbao za pembeni nafika ofisi ya Airtel Kilimanjaro naeleza
>> shida yangu kwa kijana mwembamba. Kwanza anaomba kitambulisho changu
>> kisha anasema utapigiwa simu ."Unajua hapa Moshi tupo sisi ofisi kuu
>> ipo Arusha kwa hiyo utapigiwa simu." anasema kwa upole
>> Anayesubiri lazima awe na matumaini kwa kile anachokingoja ilikuwa
>> jumamosi hiyo nikasubiri sikupata jawabu huku nikipiga simu ya huduma
>> kwa wateja, ahadi tele na majibu yasiyo na ukweli yalitolewa. Nafsini
>> nikisema jambo gani limenisababisha niweke pesa zangu kwenye simu
>> yangu ya Airtel.
>> Jumamosi , kimya, jumapili nayo kimya Jumatatu kimya! Mateso na
>> maumizu ya Airtel Money hayo. Nikawapigia simu jamaa zangu wakanitumia
>> pesa kupitia line yangu ya mtandao wa Tigo na kupata pesa angalau
>> zilinifikisha Dar es Salaam siku ya pili nikafika makao Makuu ya
>> Airtel niweze kutatuliwa tatizo langu.
>> Hapo awali nikiwa Moshi, nakutana na kijana mmoja ambaye ni miongoni
>> mwa wanafunzi wangu namuelezea tatizo lililonikuta nayeye ananiambia
>> kuwa Airtel Money wana matatizo ni vizuri kutumia mitandao mingine
>> vinginevyo utaaibika mwalimu.
>> Asubuhi yake ya tarehe 3 Disemba mwaka huu nafika makao makuu nakutana
>> na mama mrefu mwenye  mwili uliojengeka mwenye majibu ya haraka
>> yanayokatisha tamaaa Naelezea tatizo langu lakini msaada nakosa kabisa
>> , narudi mapokezi nakuomba kumuona Afisa Uhusiano au Legal Officer wao
>> nikiwa hapo kwa saa moja nzima bila jibu bila kujari safri yangu ndefu
>> kutoka Kilimanajro mpaka Dar es Salaam kufuatilia pesa yangu.
>> Gafla, anakuja kijana mwingine akivalia fulani nyekundu yenye
>> maandishi meupe akisema mzee una shida gani nikamuelekeza kwa muda
>> akakiomba kitambulisho changu na kunitatulia tatizo langu mara baada
>> ya kupokea mikwara ya mama mrefu ambaye alijitambulisha kuwa yeye
>> ndiye meneja, aha ha ha ha Meneja wa Mikwara Airtel wa eneo hilo, lo !
>> laki mbili zinanitoa jasho .
>> Nilitoa fedha zangu kwenye akaunti yangu zote na kesho yake kurudi
>> kwangu na pesa zangu mfukoni nikiwa nimeingia hasara ya madeni na
>> gharama za usafiri kutoka Moshi hadi Dar
>> Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idd majuma matatu baadaye nachukua fedha
>> kutoka katika akaunti  yangu ya Tigo kwa wakala anaweka katika Airtel
>> money laki tano na ushehe. Duu ile kuweka kiasi hicho cha fedha longo
>> longo zile zile mara umekosea pin , mara utafungiwa baada ya kujaribu
>> mara sita mara akaunti yako imefungiwa.
>> Leo hii ni siku ya tatu na niliyetaka kumtumia fedha bila ya kukatwa
>> nimemuweka njia panda hajapata fedha, uaminifu juu yake umepungua na
>> bado hakuna jibu la msaada nililopewa na kampuni hii ya simu. Huku
>> wakiwa na idara ya huduma kwa wateja ambayo binafsi mimi ninasema hii
>> ni huduma ya usumbufu kwa wateja.
>> Je, sasa niianze safari ya kuelekea Dar na kwa pesa zipi? Ama kweli
>> bure gharama. Kumbe mbiu zote za mgambo hazina ukweli.
>> Wasalaaam ndugu yenu Adeladius Makwega
>> +255688905109
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>


--

______________________________________________
Real Change for Real Development,

Lemburis Kivuyo
+255654650100 - Website: www. <http://www.infocomcenter.com/>kivuyo.com,
Unlimited Webhosting at TZS. 10,000/-/Month - www.webstar5.net

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment