Monday 16 December 2013

Re: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] Kwanini Hotuba Ya JK Kumuaga Mandela Ilikuwa Bora?

Hiki alichosema JK SA ndicho alichokisema kwa uhodari sana Mzee Kingunge Ngombale Mwiru juzi siku ya Jumamosi Nkrumah UDSM akianisha mahusiano ya ANC na TANU na Tanzania na SA, na mchango wetu katika kuikomboa SA na nchi zingine katika bara letu. Mengi tulikuwa hatuyajui na tumeyajua kupitia hotuba hizi mbili. Changamoto kwa wanahistoria wetu ni kwamba mambo haya hayajaandikwa, na ni tuna jukumu la kuyaandika ili yasipotee.

Kitila
 



From: Josephine Slaa <jaminiel@yahoo.com>
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Monday, December 16, 2013 11:50 AM
Subject: Re: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] Kwanini Hotuba Ya JK Kumuaga Mandela Ilikuwa Bora?

Tuache  unafiki,

Maggid,nani anayeharibu historia ya Tanzania Leo,Kama si wewe na viongozi wako wanaopotosha.

Ni vigumu Sana kusifia maandishi Kama matendo hayaenzi yaliyoandikwa.
Ni unafiki kuiambia Dunia kwa Maneno.wengi wa hao tunaowaona na kuwalenga duniani wanaijua vema historia yetu zaidi ya unavyoijua wewe.

Ni Mara ngapi maandishi mengi yakiwemo yakwako yamepotosha historia ya KWELI,ili mradi mnafanya kuwaridhisha watu Fulani kwa Faida binafsi.

Yatosha,dhamira Zetu zituhukumu,Tushuhudie historia kwa matendo.
Nimeandika haya baada ya kusoma makala ya Mwalimu mkuu.naomba  uipitie.

Historia hujegwa kwa gharama,vivyo hivyo huendelea kuenziwa kwa gharama.

Ningefurahi waandishi Kama wewe mngejikita katika Haki na ukweli,simamieni historia iliyojengwa kwa gharama yoyote pasipo unafiki wowote.

Mandela hakuwahi kuhubiri Amani,Bali alifanya matendo yaliyopelekea Amani kuwapo,na Hii ndiyo Sifa kubwa tunayomuenzi Nayo Leo.
Alitamani Uhuru,akaamini Uhuru wa KWELI utapatikana pale tu kutakapokuwa na Equal opportunities.

Na hicho ndicho Zuma alisisitiza kwenye hotuba yake.


Josephine S Mshumbusi
Director Igeheta.
Kawe Muzimuni,
Plot 559
Dar-es-Salaam
Tanzania.
+255789691998



On 16 Des 2013, at 8:53, Ansbert Ngurumo <ansbertn@yahoo.com> wrote:

Maggid,
Nakubaliana nawe.

Ansbert Ngurumo
Existential Philosopher, Musician, Journalist & Media Manager
Vox Media Centre & Free Media
Tanzania

On 16 Des 2013, at 8:26 asubuhi, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Ndugu zangu,

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela.

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'.

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia.

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru. Ni Thabo Mbeki. Baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa.

Usiku Mwema.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
Http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment