Sunday 20 October 2013

[wanabidii] Watanzania waishio Uingereza kuzungumza na Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza, umetoa taarifa ya kuwakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata wasaa wa kwenda kuzungumza na Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Christopher Chiza na Wawakilishi kutoka SAGCOT katika Ofisi ya Ubalozi jijini London, siku ya Jumatano (tarehe 23 Octoba 2013) kuanzia saa Kumi na Moja jioni (17:00hrs).

Mheshimiwa Waziri anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kilimo, fursa zilizomo katika kilimo na ushirikishwaji wa Diaspora katika uwekezaji katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi. 

Aidha Mhe. Christopher Chiza anatarajiwa kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi watakaohudhuria mkutano huo.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment