Wednesday 23 October 2013

[wanabidii] Watanzania 3 watiwa mbaroni wakiwa njiani kwenda kujiunga na al-Shabaab

Jeshi la Ulinzi la Kenya liliwatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na al-Shabaab, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba).

Ali Ramadhan mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.

Polisi walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.

Kwa mujibu wa polisi, watatu hao walikuwa wanaelekea Kismayu kwenda kujiunga na "vita vitakatifu, walivyodai vinaongozwa na [al-Shabaab]".

http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/newsbriefs/2013/10/21/newsbrief-01

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment