Thursday 24 October 2013

[wanabidii] UWAZI KATIKA MIKATABA JE TUTUMIE MFANO WA NCHI GANI?

MIKATABA IWE WAZI NA IJADILIWE NA WANANCHI!
WAZO ZURI. LAKINI JE TUTUMIE MFANO WA NCHI GANI?

Kwa muda sasa wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakihaha kuhakikisha mikataba inakuwa wazi na wengine wanataka ijadiliwe na Bunge, na wengine wanataka ijadiliwe na wananchi. Kuna ishu kama tatu zinapigiwa debe hapo. (1) Iwe wazi yaani wananchi waifahamu, waisome (2) Ijadiliwe na Bunge (3) Ijadiliwe na wananchi.

Katika sura ya haraka hili ni jambo zuri lakini kuna maswali matatu hivi ya kujiuliza (1) Usiri wa kibiashara ambao ni haki ya mfanyabiashara yoyote utazingatiwaje hapo? (1) Kujadiliwa na Bunge, je Bunge litakuwa na mambo mangapi ya Kufanya? maana tunajua kila wakati kunakuwa na mikataba mipya mingi katika ngazi tofauti nchini .. au mikataba ya kujadiliwa na bunge itakuwa ni ile mikubwa ya kitaifa pekee? Nahisi kama Bunge litakuwa ni Bunge la mikataba (3) kujadiliwa na wananchi ni ni dhahiri wananchi watatofautiana, je hatuoni kila wakati tutakuwa na kura za maoni za mikataaba?

Mwisho Niwape kazi wanaharakati na wanasiasa na watu wote wanaotaka Mikataba iwe wazi isomwe na ijadiliwe na wananchi.

Ni dhahiri Jambo hili wanaharakati wameliona linafanyika katika nchi Fulani. Na Kama Katika nchi fulani mikataba ipo hivyo ni dhahiri hata sisi wapo watu waliopata mikataba ya aina hiyo kutoka nchi tunazozipigia mfano. Sasa Naomba Wadau wanitafutie nchi ambazo Mikataba yake iko wazi kwa wananchi, na inajadiliwa na wananchi, nchi mikatab inajadiliwa na Bunge .. naomba na moja ya mikataba iliyojadiliwa na wananchi katika nchi wanazozipigia mfano.

Kwa maoni yangu mimi ni vizuri kutafuta njia itakayowabana watu tunaowaamini kuingia mikataba. 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment