Tuesday 22 October 2013

[wanabidii] Tanzania Annual Young Professionals Awards 2014

Press Release

 

Proactive Employment Solutions Limited

Off Tel +255 222 617 938

E-mail:  taypa@pes.co.tz

 

Tanzania Annual Young Professionals Awards

 

Proactive Employment Solutions LTD ni kampuni inayojishughulisha na masuala ya ajira na rasilimali watu kama uchaguzi,ubadilishaji na upatikanaji wa ajira,mafunzo na Maendeleo ya wafanyakazi pamoja na maandalizi ya mishahara na mafao.Leo hii PES inayo furaha kutambulisha tuzo zinazolenga kuwatunuku waajiriwa katika sekta zote za umma na binafsi ambao jitihada zao za pekee zimeleta manufaa kwa jamii zinazo wazunguka na Maendeleo ya kitaifa kwa ujumla. Tuzo hizi zinajulikana kwa jina la Tanzania Annual Young Professionals Awards (TAYPA)

 

Lengo la TAYPA ni kuwatambua na kuidhinisha viongozi vijana ambao ni mifano ya kuigwa katika soko la ndani la ajira na kuwazawadia kwa kuwa mifano bora ya kufuatwa na wengine

 

Jukwaa hili litatoa chanzo na motisha kwa ajili ya wanataalamu vijana kufanya kazi kwa bidii katika kufanikisha malengo ya kazi ya muda mfupi na muda mrefu, madhumuni na maendeleo yao.

 

Tuzo ni katika makundi matatu

 

1:Tuzo ya SAGE - Mshiriki awe amechangia katika Maendeleo ya wengine kwa kushauri na/au kwa kuwaelimisha watu ambao wameonyesha mafanikio

 

2:Tuzo ya TRAIL BLAZER - Mshiriki awe amepata matokeo mazuri kwa kounyesha uongozi wa pekee katika mazingira magumu

 

3:Tuzo ya CAPTAIN OF INDUSTRY - Mshiriki awe amewasilisha miradi yenye mafanikio kwa kuonyesha uwezo wa uongozi wa kipekee katika mazingira magumu

 

Kuteua Mshiriki katika tuzo za TAYPA mwajiri au mfanyakazi mwenza lazima awasilishe fomu za uteuzi kwa mratibu wa TAYPA kwa njia ya barua pepe  taypa@pes.co.tz kuanzia Oktoba 7, 2013 hadi Novemba 15, 2013. Fomu hizo zitapatikana katika  www.pes.co.tz

 

Kuanzia Novemba 18, 2013 mpaka Novemba 29 kamati ya uteuzi itakutana na kuchagua washiriki watatu bora kutoka kila kundi ambao watapigiwa kura na umma kwa njia ya SMS

 

Sherehe ya tuzo hizi itafanyika tarehe 21 February 2014, Dar es Salaam.

 

 

Tunawaalika na kuwahimiza waajiri na wafanyakazi wote kuwasilisha uteuzi wao kwa ajili ya kupigiwa kura.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment