Monday 7 October 2013

[wanabidii] Taarifa ya TATOA ya kusimamisha kusafirisha mizigo nchi nzima

Chama cha wamiliki wa malori Tanzania (TATOA), leo Oktoba 5, 2013 kinatangaza kusimamisha kusafirisha mizigo nchi nzima kutokana na Wizara ya Ujenzi kuondoa nafuu ya kutolipa tozo ya uzito wa magari uliozidi asilimia tano (5% tolerance) ya uzito unaokubaliwa kisheria.

Tozo ya nafuu kwa uzito uliozidi asilimia tano (5% tolerance) ilitolewa na serikali mwaka 2006 baada ya kamati iliyoundwa na serikali pamoja na TATOA kubainisha kuwa mizani mingi nchini hazina uzani sawa, hali iliyopelekea kutofautiana kwa vipimo kwa mzigo mmoja.

Jambo la pili lililopelekea kuwekwa kwa tozo ya nafuu kwa mzigo uliozidi asilimia tano ya uzito ulikubaliwa ilikuwa ni ubovu wa barabara nchini pamoja na matuta (bumps) mengi ambayo yalikuwa yanapelekea mizigo kuyumba, wakati mizani hazifanyiwi uwianishi (calibration) wa mara kwa mara.

Sababu za Serikali kwamba tozo hili ya unafuu inapelekea uharibufu wa 

barabara na ongezeko la uzidishaji mizigo, hazina ukweli wowote, kwa kuwa tatizo la uzidishaji mizigo lilikuwa kubwa zaidi awali, kabla ya tozo ya unafuu haijawekwa, lakini pia TATOA, kama mdau mkubwa kwenye ujenzi wa barabara zetu katu hangependa kuona zinaharibika.

TATOA inaamini kuwa zoezi hili limefanywa kwa makusudi kuidhoofisha sekta, hasa kutokana na ukweli kwamba zoezi hili halikushirikisha wadau yaani TATOA, na pia juhudi za TATOA kufanya majadiliano na waziri husika zimepuuzwa.

Lakini zaidi ni kuwa ondoleo la tozo hili limekuja wakati ambapo serikali haijatekeleza malalamiko mengi kutoka kwa TATOA, hali ambayo inaonyesha dharau ya wazi kwa sekta ambayo ni ya pili kwa kuchangia pato la taifa.

Kwa muda mrefu sasa, TATOA imekuwa ikilalalamikia maswala ya ongezeko kubwa la bima, ukosefu wa sehemu za kupaki magari, tozo la barabara, uwepo wa geti moja tu kwenye mpaka wa Tunduma hali ambayo imepelekea msongamano na ucheleweshaji wa mizigo uliokithiri na sasa tozo ya asilimia tano (5% tolerance).
  
TATOA inaamini kwamba mambo haya yanazungumzika, na kusimamisha usafirishaji sio suluhisho la matatizo, lakini ukaidi wa wizara na waziri husika ndio vimepelekea hali hii.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment