Saturday 5 October 2013

[wanabidii] Mtu yeyote ana uhuru wa kujiunga na mfuko wa hiari wa Hifadhi ya Jamii aupendao

HIFADHI YA JAMII NI HAKI YAKO

1. UTANGULIZI

Hifadhi ya Jamii ni haki ya kila Mtanzania . Haki hii imeanishwa katika  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 11(1) na Sera ya Taifa ya  Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003.

2. HIFADHI YA JAMII KWA SEKTA ISIYO RASMI

Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Iinawafahamisha Wananchi wote kuwa hifadhi ya Jamii ni haki ya kila mtu na si kwa wale tu walio katika ajira rasmi. Kulingana na takwimu zilizotolewa mwaka 2012 idadi ya 
Watanzania ni milioni 44.9 ambao kati yao watu milioni 1.7 tu ndio waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ikiwa ni asilimia 6.5 tu ya Nguvu kazi yote ya watu milioni 23.7. 

Hivyo Mamlaka inasisitiza Wanachi wote wenye umri wa kufanyakazi, miaka (18-60) walio ajiriwa katika sekta iliyo rasmi au sekta isiyo rasmi (waliojiajiri) kama vile Wakulima, wafanyabiashara ndogondogo, wasusi, vinyozi, mamalishe, mafundi cherehani n.k kuwa wote wanahaki ya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika mpango wa lazima au mpango wa hiari, kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii ifuatayo:- PSPF (PSS), VSRS (GEPF), PPF (DAS), LAPF (LAPF DC Scheme) na NSSF.

3. UHURU WA MWANACHAMA KUJIUNGA NA MFUKO AUPENDAO

Kwa mujibu wa kufungu cha 30 cha Sheria ya Mamlaka, mfanyakazi ambaye ameajiriwa na hajawahi kujiunga na mfuko wowote wa Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa lazima ama wa pensheni anao uhuru wa kuchagua mfuko wowote kati ya mifuko tajwa hapo juu. 

Hii inamaana kwamba mfanyakazi anapaswa kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu katika mpango wa lazima, lakini ana haki ya kujiunga na mpango wa hiari zaidi ya mmoja.

4. MAELEKEZO YA MAMLAKA KWA WAAJIRI, MIFUKO, WANACHAMA NA VYOMBO MBALI MBALI VINAVYOHUSIKA NA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WANACHAMA WAPYA.

  1. Waajiri wote katika utumishi wa umma na sekta binafsi wanapaswa kuzingatia matakwa ya sheria kwa kuwapa fursa watumishi wapya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya lazima wanayoitaka. Uhuru wa mfanyakazi uheshimiwe. 

  2. Waajiri wote wa sekta ya umma na sekta binafsi wanapaswa kuipa Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii fursa sawa ya kuandikisha wafanyakazi wapya kuwa Wanachama wa Mifuko hiyo bila vikwazo vyovyote. 

  3. Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii izingatie matakwa ya Sheria ya Mamlaka wakati wa kuandikisha wanachama wapya.

Imetolewa na;

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Dar-Es-Salaam
Tanzania.

Tel:+255 222761683/8
Tovuti: www.ssra.go.tz

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment