Thursday 10 October 2013

[wanabidii] MGOGORO WA WASAFIRISHAJI SERIKALI ILAUMIWE

Nimekuwa najiuliza maswali mengi tangu mgogoro wa serikali na wsafirishaji uanze. Serikali inabidi ilaumiwe kwa kuwaachia wasafirishaji watumie malori makubwa kusafirisha mizigo. Kwanini wasiboreshe na kutengeneza miundo mbinu ya reli ikawa ndio njia kuu ya usafirishaji badala ya kuachia secta muhimu kama hii kwa uchumi wa nchi kuendeshwa na watu binafsi? Madhara yake ndio hayo sasa wasafirishaji wanakuwa na kiburi kwababu wanajua wao ndio wameshikilia uchumi. Nadhani muda umefika sasa serikali ufufue reli ya kati kubeba mizigo na kukarabati ile ya dar - Tanga hadi Arusha ili bidhaa nyingi zisafirishwe kwa njia ya reli na hii itaondoa ukiritimba wa wasafirishaji na pia itakuwa na unafuu kwa wanaosafirsha mizigo yao na mwisho nafuu kwa mtumiaji wa mwisho.
Mh. Magufuli wacha malumbano na wasafirishaji kwa sasa wameshika mpini wewe umeshika makali yatakukata, la muhimu fufua reli zifanye kazi ndio ubora wa kazi yako utaonekana. 

0 comments:

Post a Comment