Monday 14 October 2013

[wanabidii] Hakuna kiongozi Afrika anayestahili tuzo ya Mo Ibrahim 2013

Wakfu wa Mo Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari  mjini London, umesema kuwa baada ya kutafakari kwa makini, wamemkosa mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu wa 2013.

Huu umekuwa ni mwaka wa nne kwa bara la Afrika kukosa kiongozi  mstaafu anayestahili kutunukiwa tuzo ya Mo Ibrahim.

Tuzo ya Mo Ibrahim ilizinduliwa miaka saba iliopita. Kiongozi wa kwanza kupewa tuzo hiyo alikuwa ni Joachim Chisano, Rais 
mstaafu wa Msumbiji. Mwaka 1995, Festus Mogae aliyekuwa Rais wa Botswana 2008 alitunukiwa tuzo hiyo kabla ya kutunukiwa rais Pedro Pires wa Cape Verde mnamo mwaka 2011.

Tuzo ya Mo Ibrahim hutolewa kwa kiongozi aliyeteuliwa katika misingi ya kidemokrasia, ambaye amestaafu kwa kipindi cha miaka mitatu na ambaye uongozi wake  uliheshimu sheria na misingi ya utawala bora.

Tuzo hiyo huambatana na:-
  1. Kitita cha dola za Kimarekani milioni 5 kwa kipindi cha miaka kumi. 
  2. Dola za Kimarekani laki mbili kila mwaka hadi kiongozi aliyetuzwa atakapofariki. 
  3. Fedha kwa kipindi cha miaka kumi, kwa ajili ya kukamiisha mradi wowote unaoungwa mkono na mshindi wa tuzo hiyo.

Mo Ibrahim ni mfanyabiashara bilionea, raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan.


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/10/ni-mwaka-wa-nne-mfululizo-hakuna-kiongozi-afrika-anayestahili-tuzo-ya-mo-ibrahim.html#ixzz2hlTPgwzk

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment