Thursday 24 October 2013

[wanabidii] DAWASCO KUZIMA MTAMBO WA MAJI SIKU YA JUMAMOSI

Ofisi ya Uhuriano ya Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) Makao Makuu, imetoa taarifa likiwatangazia wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kuwa, mtambo wao wa kuzaliwa maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 12 siku ya Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2013 kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja usiku.

Taarifa hiyo imesema sababu ya kuuzima mtambo huo ni ili kuruhusu mkandarasi kufanya kazi ya kuunganisha bomba linalotumika la maji ghafi (raw water) na bomba jipya karibu na mabirika (clarifiers) ndani ya mitambo.
DAWASCO imetaya maeneo yatakayokosa maji kwa sababu zilizotajwa hapo juu kuwa ni pamoja na Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach,a Kawe, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Buguruni, Chang'ombe na Keko.

Wananchi wameshauriwa kuhifadhi maji kwa ajili ya kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

Kwa taarifa hiyo, DAWASCO imewaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment