Saturday 5 October 2013

[wanabidii] CCM: Tuna imani na Tume ya Katiba

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea nchini kikieleza kuwa kinaiamini na kuiheshimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba ambaye ni mwenyekiti.

Kauli hiyo ya CCM imekuja kipindi ambacho Jaji Joseph Warioba akivishutumu vyama vya siasa kuingilia mchakato huo, huku akivionya kwamba  mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametoka kwa wananchi, siyo vyama vya siasa.

Ufafanuzi huo wa CCM unaonekana kama kutaka kuweka mambo sawa baada ya hivi karibuni vyombo vya habari kumnukuu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho, Abdallah Bulembo akisema siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusu mambo wanayoyataka yaingizwe ndani ya Katiba.

Katika majibu yake, Jaji Warioba alimtaka  Bulembo kuacha kupiga kelele dhidi yake kwa maelezo kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya, bali alitumwa na Serikali kwa niaba ya wananchi

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya CCM  Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema kuwa chama hicho tawala kinaiheshimu tume hiyo na kamwe hakiwezi kuiingilia.

Nape alisema tume hiyo iliteuliwa kwa ajili ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya, hivyo wanaiheshimu na wana imani nayo. "Tunaheshimu tume, tuna imani nayo na tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mchakato wa Katiba" alisema Nape.

Kauli ya Nape imekuja wakati ambao kuna msuguano kati ya CCM na Serikali yake kwa upande mmoja na vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment