Saturday 19 October 2013

re:[wanabidii] MALALAMIKO JUU YA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, October 19, 2013 4:28:58 AM GMT-0700
Subject: [wanabidii] MALALAMIKO JUU YA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE

*MALALAMIKO JUU YA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBUKU YA MWALIMU NYERERE*
*
1. SHERIA YA UANZISHWAJI CHUO*

Mh. Waziri Mkuu, sheria iliyopo ya uanzishwaji wa chuo inamapungufu kadhaa,
ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho. Mapungufu hayo ni:

i. Sheria haitaji sifa za mkuu wa chuo aweje
ii. Sheria haitaji sifa za Makamu Mkuu wa Chuo
iii. Sheria haitaji sifa za Msajili wa Chuo
iv. Pia sheria inapigana na taratibu za NACTE ambazo zinataja uwepo wa
Rector, Deputy Rector Academic, Deputy Rector
Adminstration.
v. Sheria Haitaji ukomo wa Msajili (registrar) imeiachia Bodi na Mkuu wa
chuo suala la kuamua muda wa Msajili.
vi. Sheria inamtaja msajili kama Katibu wa kamati ya taaluma wakati yeye
hahusiki na mambo ya taaluma.
vii. Kazi za kamati zifuatazo Human Resource Development and Disciplinary
Committee, Finance and Planning Committee and Students' na Disciplinary
Appeals Committee hazitajwi na sheria, tofauti na kazi za kamati ya taaluma
ambapo kazi zake zimetajwa.

Mh. Rais tunakuomba sheria hii ya uanzishwaji wa chuo ipitiwe upya ili
kukidhi matakwa ya sasa na kuleta ufanisi wa kazi kwa ujumla. (P.T)
*
2. UWAKILISHI WA WAFANYAKAZI KATIKA BODI YA CHUO*

Pamoja na sheria kusema kuwa kutakuwa na uwakilishi wa Wafanyakazi (The
Mwalimu Nyerere Memorial Academy Act, 2005 Ibara 6:1 (D Na G) katika bodi
ya chuo, Mkuu wa chuo amekuwa akimdanganya Waziri kwa kumpatia mapendekezo
ya majina ya wanataaluma na wafanyakazi kwa ujumla, ambao sio wawakilishi
halali.

Suala

Mhe. Rais tokea mwaka 2006 Bodi ya Chuo hakina wawakilishi wa wafanyakazi
bali wawakilishi hao huteuliwa kutokana na matakwa ya Menejimenti, hivyo
kufanya mawazo ya wafanyakazi kutowasilishwa kwenye bodi.

*3. VIKAO VYA WAFANYAKAZI*

Mh. RaisTokea Mwenyekiti wa Bodi ateuliwe kwa muda wa miaka 8 sasa hajawahi
kufanya kikao na wafanyakazi. Suala hili limesababishwa na Menejimenti
ambayo kwa hakika imekuwa ikimficha Mh. Balozi ili kwa kumdanganya kuwa
mambo yanaenda. Hii imesababisha Mkuu wa Chuo kufanya vikao vichache vyenye
kututisha wafanyakazi na hivyo kushindwa kutoa mawazo yetu.

*4. MALENGO YA CHUO*

Mhe. Waziri Mkuu Kutokana na sheria ya chuo, Chuo kina malengo kumi na moja
(11) kama ifuatavyo:
a) To provide facilities for study and training in social sciences,
leadership and continuing education;
b) To conduct training programmes in the disciplines specified in paragraph
(a);
c) to engage in research and development in the disciplines specified in
paragraph (a) and to evaluate the results achieved by the Academy training
programmes;
d) To provide consultancy services to the public and private sectors in
specified fields as prescribed in this Act;
e) To sponsor, arrange, facilitate and provide facilities for conferences,
symposia, meetings, seminars and workshop, for discussion of matters
relating to social sciences, leadership and continuing education;
f) To conduct examinations and grant awards of the Academy as approved by
the National Council for Technical Education;
g) To arrange for publication and general dissemination of materials
produced in connection with the work and activities of the Academy;
h) To engage in income generating activities for effective financing and
promotion of entrepreneurship;
i) To establish and foster close association with the Universities and
other institutions of higher education and promote international
cooperation with similar institutions;
j) To do all such acts and transactions as are in the opinion of the
Governing Board expedient or necessary for the proper and efficient
discharge of the functions of the Academy;
k) To perform such other functions as the Minister or the Governing Board
may assign to the Academy, or as are incidental or conducive to the
exercise by the Academy of all or any of the preceding functions.

Mh. Rais,
kati ya malengo hayo juu ni lengo malengo a, f na J kidogo yameweza
kufanyiwa kazi. Lakini malengo mengine yote hajawahi kufanyiwa kazi tokea
chuo kianzishwe mwaka 2005. Mh. Raisnaomba ufanyie uhakiki haya tuandikayo
juu ya malengo. Chuo kimebaki kuwa kama sekondari, hakuna tafiti
zinazofanyika wala ushauri wa kitaalamu unaoendelea.

*5. MISHAHARA YA WAFANYAKAZI*

Mh. Raistunapenda kutoa masikitiko yetu juu ya mishahara ya wafanyakazi.
Kumekuwa na tatizo kubwa la ongezeko la mishahara ya wafanyazi wa kada
zote, wafanyakazi wamekuwa hawapandishwi madaraja kulingana na stahili yao.
Mshahara unapandishwa ni ule wa ongezeko la litolewalo na serikali, lakini
annual increment kwa wafanyakazi haipo kabisa. Hili limepelekea wafanyakazi
wanaoajiriwa siku za karibuni kulingana mishahara na wafanyakazi wa zamani.

Mhe. Makamo wa Rais suala hili linafanyika makusudi kabisa ili kuwakomoa
wafanyakazi, hatuwezi amini kuwa utawala hawajui juu ya suala hili. Hivyo
tunaomba ulifanyie kazi pia.

*6. AJIRA ZENYE UTATA*

Mh. RaisKumekuwa na ajira zenye utata kwa wahadhiri watatu (3), utata huu
umefanywa na msajili sio kwa bahati mbaya, bali kwa maslahi binasfi.
a. Ajira ya Ndugu Ernest Luambano: Mh Waziri Mkuu Ndugu Luambano aliajiriwa
na chuo mwaka 2004 akiwa na miaka hamsini (50) akiwa kama afisa tawala.
Ajira yake ilikuwa ni ya mkataba wa miaka 4, hivyo muda wa mkataba wake
ulikuwa uishe mwaka 2008. Lakini mwaka 2006 kwa kushirikiana na mkuu wa
chuo walirudisha umri wa Luambano nyuma yaani akaonekana amezaliwa mwaka
1959, basi kuandika tarehe. Baada ya kurudisha umri nyuma wameficha mafaili
ya ajira yake ya mwanzo ya mkataba na kufanya au kuingiza mwaka 1959 kama
mwaka wake wa kuzaliwa, hivyo kuonekana kwamba aliajiriwa akiwa na miaka 44
au 45.

Suala hili ni kinyume na taratibu za ajira katika ofisi za umma kama
inavyoelekezwa na standing order ya mwa 2009;
D.33 Appointment on Contracts:
(1) A candidate appointed to a pensionable post in the public service on
non-pensionable terms, or to a non-pensionable post, shall be required to
enter into a contract (on gratuity terms) specifying the terms of his
employment as provided for in Appendix D/V. Contracts on gratuity terms,
which shall be the normal form of engagement in such cases, provide for the
payment by Government of a gratuity at a prescribed rate on satisfactory
completion of the contract.
(2) Under special circumstances, certain persons may be engaged in the
public service to serve on contract terms. These shall include:
(a) a non-citizen who is engaged for some projects or on expatriate
requirements;
(b) a citizen from outside the public service who is engaged to the Service
under expatriate or consultancy requirements;
(c) a retired public servant who has been re-engaged in the Service; and
(d) a citizen who is first appointed to the Public Service after he has
attained the age of 45 years.
(3) Where it is in the opinion of the appointing authority that a public
servant be re-engaged on further terms of contract, the appointing
authority shall notify the Permanent Secretary (Establishments) who shall
forward to the Chief Secretary with recommendations.

D.34 Completion and Renewal of Contracts:
(1) The Chief Executive Officer shall inform the public servant three
months before the expiry of the contract, whether or not he wishes to
re-engage him for further period of service. Similarly the public servant
serving on contract shall notify his Chief Executive at least three months
before the engagement is due to expire whether or not he wishes to be re –
engaged, for a further period of service.
(2) Approval of the Appropriate Appointing Authority to be sought: On
receipt of the notification referred to in paragraph (1), the Chief
Executive Officer shall forward his recommendation regarding the
re-engagement of the public servant concerned to the appropriate authority
for approval.
(3) The Chief Executive Officer shall not initiate or seek the approval of
the re-engagement of a public servant in contract unless:-
(a) There are special resources and arrangements of training of counter
parts and successors in such post; and
(b) There is a special provision in the contract obliging the employee in
contract to impart his knowledge to the counterparts and successors.
(4) Re-engagement of a contract employee without consideration of the
requirements under paragraph (3) shall only be made by an approval of the
Chief Secretary.

D.39 Age of admission to a Pensionable Establishment:
Appointments to the pensionable establishment shall be restricted to
persons of and below the age of 45 years who would be in a position to
complete the fifteen years' service required to qualify for the grant of a
pension on reaching the compulsory age of retirement. There shall be
special circumstances which may justify variations in the application of
the general principle, and such cases shall be submitted for consideration
of the Permanent Secretary (Establishments).

Katika suala hili, bodi ya chuo ilidanganywa na Mkuu wa chuo kwa makusudi
ili bwana Luambano apate ajira ya kudumu. Hivyo Mh. Dr. Salim hajui lolote
juu ya hili kwani alidanganywa.

Tunakumba Mh, ufanyie kazi hili suala kwa haraka, kwani Msajili amekuwa
tatizo katika taasisi, ajira zote zinazofuata hapa nchini yeye ndiye
mhusika mkuu wa kuzitengeneza. Kwasababu na yeye amegushi. Wafanyakazi
hatutakubali kuendelea kufanya kazi na mtu ambaye amegushi umri, lakini pia
akikabiliwa na tuhuma lukuki za ufisadi.

Hivi sasa Mkuu wa chuo na Msajili wanahaha kuficha ukweli wa mambo kwa
kutengeneza na taarifa mbalimbali na kupoteza ushahidi juu ya hili, lakini
ni tumaini letu kuwa serikali ina mkono mrefu itaufikia ukweli pasipo
kumuonea mtu.

b. Ajira ya Mhagama: Huyu alikuwa mwajiriwa wa chuo kabla ya kujiuzuru
mwaka 2012. Ilikuwa ikifahamika tokea alipoajiriwa kuwa ana vyeti visivyo
halali. Lakini chuo kiliendelea kumulinda pasipo kufanyia kazi. Baadae chuo
kilimpeleka kusoma shahda ya uzamili chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Baada ya kumaliza, chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimnyima cheti, japo
Msajili alimpandisha mshahara pasipokuwa na vyeti na kumlipa mshahara wa
kiwango cha Uzamili. Suala hili liliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya
habari na mitandao ya jamii. Walipoona kuwa Mhagama anasakamwa Msajili
alimshauri ajiuzulu, wakati wa kujiuzulu alilipwa hela ya likizo. Pamoja na
sheria kuwa wazi, juu ya mfanyakazi anayeacha kazi ndani ya masaa 24,
kutakiwa kulipa mshahara wa mwezi mmoja kwa mwajiri bw Mhagama hakufanya
hivyo.

Suala hili lilichunguzwa na Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, jambo la kushanga taasisi hii ilikisafisha chuo kwamba
hakukuwa na shida. Mambo la kujiuliza hapa:
i. Mhagama aliajiriwa lini Mwalimu Nyerere?
ii. Menejimenti ya Mwalimu Nyerere alijua lini suala hili la Mhagama kufoji
vyeti?
iii. Baada ya kugundua Menejimenti ya Mwalimu Nyerere ilifanya nini?

Tukijibu maswali haya unagundua kuwa hata Ofisi ya Rais Sekreatieti ya
Maadili ya Viongozi wa haikufanya kazi yake ipasavyo. Haiwezekani suala
hili ligundulike miaka miwili nyuma, pasipo kuchukuliwa hatua (ushahidi
upo). Hata baada ya kulitambua hili hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

c. Ajira ya Bi Sara Mwakyusa: Muhadhiri huyu alipewa mkataba wa mwaka mmoja
ilikufundisha Tawi la Zanzibar. Menejimenti ilitambua kuwa huyu mhadhiri ni
muajiriwa wa manispaa ya Ilala shule ya Sekondari Azania, iliamua kuumpa
mkataba wa ajira ya mwaka mmoja, huku menejimenti ikijua ni kosa kisheria.

d. Ajira ya Bwana Rodgiers Kiowi, mwaka 2010 chuo kilimuajiri ndugu Kiowi
kama mhadhiri Msaidizi, wakati kikijua kuwa ni muajiriwa wa Taasisi ya
Teknolojia ya Dar es Salaam. Tunasema chuo kilijua kuwa ni mwajiriwa wa DIT
kwa ushahidi wa kimazingira.

i. Tokea aingie hajawahi kuingizwa kwenye payroll ya hazina na sasa ni muda
wa miaka mitatu. Kwanini ichukue muda mrefu kiasi hicho wakati Hazina na
MNMA ni viko karibu kama ni suala la ufuatiliaji.
ii. Pili, suala hili menejimenti ilifahamishwa na afisa mitihani
aliyejiuzulu, lakini haikuchukua hatua badala yake alihudhuria kikao cha
kamati ya taaluma.
iii. Mpaka sasa hajafunguliwa mashtaka ya kuiibia serikali.
Kwa ushahidi huu hakika Menejimenti ya chuo inajua suala hili, ndio maana
msajili amekuwa akitoa ushauri wa kiupotoshaji kwa mkuu wa chuo, ili bw
Kiowi asichukuliwe hatua.

Mh. Rais,
tunaomba uchunguze ajira hizi tata ambazo kwa hakika zimetafuna pesa za
walipa kodi. Mfano Kiowi amekuwa analipwa mshahara na marupurupu yote kwa
mapato ya ndani na sio hazina kwa muda wote.
*
7. UJENZI WA CHUO ZANZIBAR
*
Mh. Waziri Mkuu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Mkuu wa Chuo
amefanikiwa kufanikisha kujenga Chuo Zanzibar, hili ni takwa la kisheria.
Lakini ujenzi huu kwa mujibu wa kamati ya huduma za jamii za Bunge
hakukudhi baadhi ya mambo. Licha ya Naibu Waziri wa Elimu kutoa agizo juu
ya kutofunguliwa kwa jingo hilo, menejimenti ya chuo ilimdanganya Mh. Salim
(Mkiti), likafunguliwa. Ufunguzi huo haukuhudhuriwa na kiongozi yeyote wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. Hii ni kutokana msigano uliokuwepe
kati ya menejimenti, Naibu Waziri wa Elimu na Kamati ya kudumu ya huduma za
jamii ya bunge.

Mh. Raiskwa kuwa suala la ujenzi ni linaonekana, tunaomba utume watu wako
wakaangalie ujenzi ule kama umekidhi matakwa ya ujenzi.

*8. UKARABATI WA NYUMBA YA MTU KUWA HOSTEL YA WANAFUNZI ZANZIBAR*

Mh. Waziri Mkuu, kuna suala ambalo linatia shaka, ambalo ni ukarabati wa
nyumba ya mtu kuwa hostel ya wanafunzi Zanzibar. Hii ilikuwa ni njia ya
kufanya ufisadi kwani haukufuata taratibu za kimanunuzi. Bahati mbaya,
kamati ya huduma za jamii ya bunge ilifichwa juu ya ukweli huu. Yafuatayo
hayakufanyika:
i. Menejimenti haikutanganza tenda ya kutafuta hosteli.
ii. Haikutangaza tenda ya zaidi ya shilingi 700 kwa ajili ya kukarabati
jengo hilo.
iii. Pesa zaidi ya shilingi 700 zingeliweza kuanzisha ujenzi wa hosteli ya
chuo, kuliko kinachofanyika sasa hivi kwa kulipa dola 20,000 kwa mwaka
kwenye jingo hilo.

Mh. Rais, huu ni ufisadi mkubwa unaoendelea hapa, kwani hata bodi ya tenda
haijui jambo lolote juu ya ujenzi huu

*9. UJENZI WA HOSTELI YA KIGAMBONI*

Mh. Raissasa hivi chuo kinaendeleza ujenzi wa hosteli hapa Kigamboni,
Ujenzi huo uko kwenye awamu ya pili. Jambo la kushangaza katika awamu hii
ya pili hakuna tenda iliyotangazwa hii ni kinyume na taratibu. Mkandarasi
anayefanya kazi hii ni Yule Yule aliyejenga Zanzibar, aliyekarabati hosteli
ya wanafunzi Zanzibar.
Ujenzi wa awamu ya pili haujulikani sehemu yoyote zaidi ya Mkuu wa chuo na
Msajili, bodi ya Tenda haikushirikishwa kwa jambo lolote.

*10. MADENI YA NDANI*

Mh. RaisMadeni ya ndani ya yamezidi kuwa makubwa, wafanyakazi sasa wanadai
posho mbalimbali kama posho za nyumba na posho za nauli. Tokea mwezi wa
Saba posho hizi zimesitishwa pasipokuwa taarifa yoyote. Hakuna taarifa
yoyote iliyotolewa sababu ya kustisha posho hizi, japo tunasikia tutalipwa
mwezi wa kumi kwasababu sasa chuo hakina pesa.

Mh. RaisWahadhiri hupata posho kwa ajiri ya kusimamia mitihani,
kusahishisha mitihani, Kusimamia tafiti za wanafunzi na vikao mbalimbali,
mpaka sasa wahadhiri nao hawajalipwa. Japo la kushangaza hakuna sababu
yoyote iliyotolewa. Sasa wahadhiri wanapanga kugoma kwa sababu ya posho zao.

Mh. Waziri Mkuu, wafanyakazi hawawezi kuzungumza jambo lolote, kwasababu
mkuu wa chuo amekuwa akitumia vitisho kwa wafanyakazi kwamba yeye yuko
karibu na Rais, hivyo hakuna mtu anayeweza kumfanya lolote.

*11. VITISHO DHIDI YA WAFANYAKAZI (KUACHA KAZI) UBABE*

Mh. Waziri Mkuu, kumekuwa na vitisho vya mara kwa mara kwa wafanyakati
ambao huonekana wanakwenda kinyume na matakwa maovu ya menejimenti. Tokea
mwaka 2005 wafanyakazi wengi sana wameacha kazi kwasababu ya kunyanyaswa na
menejimenti ya chuo.

Mh. Raishili suala limekuwa likifichwa kwa mwenyekiti wa Bodi, akidanganywa
kuwa wafanyakazi hao wameacha kazi kwasababu zao binafsi, wakati sio kweli.
Mh. Raishili limesababisha mara kwa mara upungufu wa wafanyakazi hapa
chuoni.

*12. MANUNUZI*

Mh. RaisSuala la manunuzi limekuwa tatizo kubwa hapa kwetu, msajili wa chuo
amekuwa ndiye muhusika mkuu katika manunuzi ya chuo, suala hili limekubikwa
misingi ya rushwa. Msajili ndiye afisa manunuzi ya chuo, watu waliopo
katika kaitengo cha manunuzi wao ni alama tu, hawafanyi kazi zao. Japo
wamekuwa wakishiriki kumfanikishia msajili mambo yake ili yaonekane
yamefata taratibu.

Suala hili lilipelekwa PCCB, PCCB nao wamepewa rushwa na msajili, masjili
amekuwa na mawasiliano makubwa na afisa mmoja wa PCCB makao makuu. Afisa
huyo amekuwa akitoa siri za wapeleka taarifa, pia amekuwa akisaidia kuficha
maovu ya MNMA. Kwa uhakika zaidi juu ya suala hili naomba uchunguze
mawasiliano (simu) ya Msajili wa Chuo na maafisa wa PCCB waliokuwa
wanashughulikia masuala ya MNMA.

Pia Taasisi ya PPRA baadhi ya maafisa wake wanatumika kuficha ukweli juu ya
tuhuma zinazopelekwa huko. Pia uchunguzi ufanyike juu ya mawasiliano (simu)
ya siri kati ya afisa mmoja wa PPRA na Msajili wa chuo.
*
13. MCHAKATO WA KUMPATA MWENYEKITI WA BODI NA MKUU WA CHUO*

Mh. RaisMkuu wa chuo amemuandikia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi barua za tarehe 19 na 24 Julai aweze kumuomba Waziri wa Elimu,
akuombe umuungezee muda Dr. Salim Ahmed Salim. Hili tunakubaliana nalo
kabisa, sio kwamba Dr. Salim katenda makubwa, hapana ni kwasababu tunaimani
menejimenti haikumtumia ipasavyo. Tunaimani menejimenti mpya ikiwekwa na
Dr. Salim akaendelea kuwa Mwenyekiti, chuo chetu kitabadilika sana, kuliko
kilivyosasa.
Mh. Raisitakumbukwa kwamba Mkuu wa chuo wa muda wake wa miaka miwili
uliyomuongezea unakwisha mwezi wa 12 2013. Jambo la kushanganza mpaka sasa
hakuna mchakato wowote ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumpata mkuu wa chuo
mpya. Jambo hili linafanyika makusudi ili Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo aje
akaimu ukuu wa Chuo. Kukaimu kwake kutakuwa kunatoa nafasi kwa msajili wa
chuo kuwa Mkuu wa Chuo kwa "remote".

Katika suala hili, ni muendelezo wa Mkuu wa chuo kutotaka kufanya kazi na
watu wenye sifa na uwezo. Mfano Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo amekaimu nafasi
hiyo kwa muda wa mwaka mmoja na miezi miwili sasa. Mkuu wa chuo na amekataa
kuomba utumishi ili chuo kiajiri mtu mwenye sifa yaani mwenye Shahada ya
Uzamivu. Kwa kuwa Mkuu wa chuo na Msajili wanapenda watu wasiokuwa na uwezo
na ambao wanawasikiliza wao basi mchakato wa Naibu mkuu wa chuo
haukufanyiwa kazi.
Mh. Raistunakuomba kwa dhati, uingilie mchakato huu, ili malendo yao ya
kukaa na kaimu mkuu wa chuo asiye na sifa yasiweze kufikiwa.
*
14. WANATAALUMA KUTOKUWA NA SIFA*

Chuo chetu kinakabiliwa na tatizo kuwa katika taaluma, wanataaluma
waliowengi hawana sifa ya kufundisha. Ajira zao zina utata mkubwa sana, hii
imesababisha wahadhiri wengi kutojiamini kwa kuwa hawana sifa za kufundisha
elimu ya juu. Taratibu za walimu wa elimu ya juu wanatakiwa wawe na ufaulu
angalau wa GPA ya 3.5 lakini wahadhiri wengi wako chini ya hapo.

Pia tatizo hili linatokea katika masomo ya ufundishaji, (specialization)
mfano Mhadhiri aliyesoma shahaha ya "Political Science and Public
Administration" (PSPA) na ufaulu wake ukawa ni 3.2 GPA, shahada ya Uzamili
akasoma "Development Studies". Kwa MNMA Mwalimu huyu anaweza kufundisha
"Public Policy" kwa wanafunzi wa shahada. Mwalimu huyu ufaulu wake katika
somo hili ulikuwa alama "C" wakati akisoma shahada ya kwanza, na shahada ya
pili hakusoma somo hili. Hivyo unakuta Mwalimu wa huyo hajui
anachokifundisha licha ya wanafunzi kulalamika.

Mfano hapo juu ni baadhi tu, ya wahadhiri waliopo hapa, wengi hawana sifa
kama vyuo vingine. Ndio maana hata chuo chetu hakisikiki kutokana na aina
ya walimu tulionao.

*15. SERA YA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI (STAFF DEVELOPMENT POLICY)*

Maendeleo ya wafanyakazi ni motisha kwa wafanyakazi wenyewe, tokea mwaka
2005 chuo kianzishwe hakuna sera ya maendeleo ya wafanyakazi. Sera hii ni
muhimu sana kwa maendeleo ya taasisi. Kutokuwepo kwa sera hii wafanyakazi
wamekuwa hawapelekwi shule, hivyo kufanya wafanyakazi wengi kuanza kusoma
kwa kuibia.

Pia wapo wafanyakazi waliokataliwa kwenda kusoma kwa madai kuwa utendaji
kazi wao hauridhishi.

Tokea mwaka 2005 mpaka leo, mfanyakazi mmoja tu ndiye aliyeweza kuhitimu
shahada ya Uzamivu, tena kwa juhudi binafsi, kwani chuo kilikuwa kinamlipia
ada tu.

Miaka nane wa uwepo wa Mkuu wa chuo huyu ni mfanyakazi mmoja tu ambaye
amepata PHD, japo hata yeye upandishwaji wake daraja umekuwa na shida kubwa.

*16. MSAJILI WA KUWA MHADHIRI MWANDAMIZI (LECTURER)*

Upandaji wa madaraja katika elimu ya juu upo wazi, Msajili wa chuo
ameajiriwa na chuo kama afisa Tawala, baadae akapewa nafasi ya msajili.
Msajili hana uzoefu wowote katika kufundisha na hajawahi andiko lolote
kabla na hata akiwa mwajiriwa wa MNMA. Jambo la ajabu msajili sasa
ametunikiwa cheo cha mhadhiri mwandamizi (Lecturer), pasi kuwa na sifa.
Menejimenti imeidanganya bodi ya chuo, kwa kuumpa mshahara ambao sio
stahili yake.

*17. KAMATI YA UBORA YA CHUO*

Ofisi hii imekuwa ni picha tu, wakuu wa idara hii wamekuwa wakilipwa posho
za ukuu wa idara pasipokuwa na kazi yoyote. Tokea 2005 chuo kianzishwe
kamati hii haijawahi kukaa kikao hata kimoja wakati ubora ndio suala muhimu
katika mustakabali wa taasisi yetu.

*18. MITIHANI KUTOSAHIHISHWA*

Mwaka wa masomo 2011/2012 katika tawi la Zanzibar, ilibainika kuwa mitihani
na majaribio ya somo la "Bookkeeping" haikusahihishwa, hivyo matokeo
yalipikwa. Hii ilisababisha matatizo makubwa kwa wanafunzi kwani wengi
walifeli somo hilo. Matokeo yaliyowekwa yalikuwa yamepikwa hivyo kuondoa
uhalisia. Mwalimu wa somo husika hakuchukuliwa zozote.
Menejimenti ya chuo kwa kushirikiana, mkuu wa tawi Zanzibar na afisa
mitihani, wa chuo walificha ukweli huku wakiwaacha wanafunzi wakipoteza
haki zao. Suala hili lichunguzwe kwani limewasababishia wanafunzi kuapta
alama zisizo kuwa zao.

*19. UDAHILI WA WANAFUNZI*

Udahili wa wanafunzi umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka, udahili huu
umesababisha kushuka kwa mapato ya chuo. Kutoka wanafunzi 2235 mwaka
2010/2011 hadi wanafunzi 1742 mwaka 2012/2013.

Pia ofisi ya udahili imekuwa ikijihusisha na rushwa kwa kushirikiana na
ofisi ya mitihani. Katika mwaka wa masomo 2012/2013 wanafunzi wa ngazi ya
shahada 24 walikuwa hawana sifa. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi
ya ofisi hiyo. Ili kuficha uovu kwenye ofisi ya udahili, mpaka sasa mafaili
ya wanafunzi wote hayana kumbukumbu zao, hili linafanyika ili ionekane kuwa
wanafunzi wote hawana kumbukumbu kama walioingia pasipokuwa na sifa.

Mh. Raiskuna maswala mbalimbali ya ukiukaji wa taratibu za mitihani,
ukiukwaji huo umefanywa na Naibu Mkuu wa chuo, jambo la kushanga hakuna
hatua zozote zilizochukuliwa. Afisa mitihani huyu naye achunguzwe kwani
amekuwa akishirikiana na afisa udahili kufanya ufisadi. Pia ana tuhumiwa
kutengeneza vyeti feki na kuwapa wanafunzi waliofeli.

*20. OFISI YA UHASIBU
*
Ofisi ya uhasibu inakiuka taratibu nyingi za kifedha kwa kisingizio cha
raslimali watu. Mh. Tunaomba ufanyie uchunguzi ofisi hii kwa kina utaona
uozo uliopo. Kwasasa chuo kimemuongezea muda mhasibu mkuu aliyemaliza muda
wake, hili lilifanyika ili muhasibu huyo aweze kuwafichia maovu. Pia
kampuni inayofanya ukaguzi wa ndani imetiwa ndani ya mifuko ya wakubwa
hawa. Suala la pre auditing halifanyiki kwa makusudi kabisa

*21. PESA ZA PENSHENI*

Mh, Pesa za Pensheni za michango ya wafanyakazi za mwezi wa Agosti (8) 2013
zimeliwa. Pesa hizi ni pesa halali za wafanyakazi, kutokana na ukata mkubwa
uliokikumba chuo kwasababu ya ufisadi pesa hizo zimetumika kwa ajili ya
vikao vya wakubwa. Serikali ilileta michango hiyo ya wafanyakazi.

*22. AJIRA MPYA*

Tunaishukuru Tume ya ajira kwa kuingilia kati mchakato wa ajira ambao chuo
tayari kilikuwa kimefanya bulanda tayari, kwa kutaka kuajiri watu wasio na
sifa. Baadhi ya wakuu wa idara ambao walipewa uwezo wa kushort list
walikuwa wamekwisha pokea rushwa ya pesa wengine waliomba rushwa ya ngono,
ushahidi upo. Ukitaka kupata ushahidi huo chukueni namba za simu za wakuu
wa idara angalieni pesa zilizoingia kwa Tigo na M-pesa. Japo wapo waliopewa
cash.

Mh. Raistunakuomba upitie madai yetu haya, jambo haya ni baadhi tu ya
malalamiko ya wafanyakazi wa MNMA. Tuma watu wako waje wajionee uozo
uliokidhiri na kupindukia. Kuna malalamiko ya mfanyakazi mmoja mmoja, pia
ya vyama vya wafanyakazi.

Pia utakumbukua ulipokuja kututembelea chuo chetu, ulituambia kuwa tuko
kimya sana, ukimya wetu ni matatizo yaliyokidhiri hapa kwetu. Pia viongozi
wetu hawafanyi jitihada zozote za kusikikia kwa kuogopa tutaonekana, na
viongozi wataweza kujua matatizo yaliyopo. Njia hii Mkuu wa chuo ameitumia
sana ili kufanikisha adhima zake mbaya za kifisadi.

Natumaini ombi letu litafanyiwa kazi.

Sisi wafanyakazi
MNMA
Nakala kwa:
Ofisi ya Rais Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment