Friday 18 October 2013

Re: [wanabidii] Zitto anapigwa vita ndani ya CHADEMA na Mitandao ya Urais ndani ya CCM

Hadi sasa suala hili, ndani ya CHADEMA limetolewa kauli na watu wawili, Ofisa Mwandamizi wa Habari na Katibu wa Baraza la Wadhamini, Antony Komu. Hakuna mahali popote ambapo Ndugu Zitto ameshambuliwa binafsi na chama juu ya majukumu yake hayo kama Mwenyekiti wa PAC. Labda mleta hoja atuoneshe huo ushahidi alionao.

CHADEMA wamesema wazi kuwa wako tayari kutoa ushirikiano, kama ambavyo siku zote wamepigania, sheria hiyo itekelezwe, si katika ruzuku pekee, bali katika fedha zote ambazo vyama vinapata, kwa ujumla ni mapato na matumizi.

On Friday, October 18, 2013 10:19 AM, Reginald Miruko <rsmiruko@gmail.com> wrote:
Na huu unafiki mwingine, Chadema mpya ndo mtu gani?
On Oct 18, 2013 6:06 PM, "CHADEMA Mpya" <chademampya2014@gmail.com> wrote:
Tangu Zitto atoe agizo la vyama vya siasa kukaguliwa kwa niaba ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kumezuka malumbano mbalimbali dhidi ya Zitto (Personal Attack) badala ya Kamati kwa ujumla toka kwa watu mbalimbali lakini zaidi sana toka CHADEMA na CCM.
Kwa mtazamo wangu ndani ya CCM na CHADEMA wanaomshambulia Zitto wanafanya makusudi na kwa malengo ya kisiasa. Wanataka watu waone agizo lile ni la Zitto na sio la Kamati ya Bunge na kwamba Zitto ana agenda binafsi jambo ambalo sio kweli na ni Propaganda tu.
Ndani ya CHADEMA kuna watu wanataka kumfitinisha Zitto na WanaCHADEMA kwa malengo binafsi lakini hasa hasa ni ya Uchaguzi ndani ya Chama chao. Wanataka WanaCHADEMA waamini kuwa Zitto anataka kuzuia ruzuku ili wapate shida na washindwe kufanya kazi za Chama na wale wa Makao Makuu wakose mishahara yao ya kila mwezi. Wanajua na wanaamini kwa kufanya hivyo watu wao ndani ya Chama watamchukia Zitto na ukija uchaguzi Zitto hatapata Uenyekiti (Maana anautaka na yuko very serious wakati huu kuliko wakati mwingine wowote). Lakini Zitto alishasema hadharani kuwa yeye hana wasiwasi na hesabu za CHADEMA maana ziko safi anataka kuwabana CCM.
Ndani ya CCM kuna mitandao ya Urais ambayo kila uchao inahangaika kuingiza fitina ndani ya CHADEMA ili viongozi wagombane Chama kisambaratike ili wao wapite kwa urahisi. Wanajua hata kama watapitishwa na CCM wakati CHADEMA ikiwa bado ni imara hawatafanikiwa kuingia Ikulu. Inasemekana mitandao hiyo ya Urais ndani ya CCM ndio ambayo pia imekuwa ikilipua mabomu kwenye mikutano ya CHADEMA kwa kuloby Ma OCD na Ma RPC ili watu wafe kwenye mikutano ya CHADEMA watu waiogope CHADEMA kabla ya 2015. Kwa hiyo Mitandao hii ya CCM inachokifanya ni kuchochea fitina na Migogoro ndani ya CHADEMA kwa kumgombanisha Zitto na Viongozi wenzake na WanaCHADEMA pia kwa njia ya Propaganda ila kwa sababu CHADEMA nako Zitto ana maadui basi wanaungana na hawa wa CCM kumshambulia Zitto. Zitto stand on Issues and Truth Time will solve everything.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment