Friday 18 October 2013

Re: [wanabidii] Utafiti: Wasio na elimu waongoza kumpenda Rais Jakaya Kikwete

Tusiwalaumu hawo Darasa la saba hebu tuangalie, hao wasomi wetu ndi
waliotufikisha hapa tulipo, wanaojiita wasomi ndio waliosaini mikataba
mibovu kama ITPL, MADINI,RICHMOND na kadhalika, wasomi hao hao ndio
waliotuletea EPA, Mmambo mengi na mabaya katka Tanzania yetu
yamehalibiwa na hao wanaojiita wasomi.

Nashangaa leo wakijitenga na kutuletea utafiti usio na kichwa wala
miguu eti wasiokwenda shule ndio wanampenda JK, Wakati wao ndio
walimfagilia kwa maslahi yao binafsi wengine wakathubutu mpaka kumuita
chaguo la mungu, sasa leo wanamgeuka na kuwatumia lawama darasa la
saba, mnasubiri 2015 mje kuwatumia hao hao mnaowatuhumu leo
Tuache chuki jamani tuwa wakweli na ukweli humuweka mtu Huru

On 10/18/13, Magora Hassan <magorah15@gmail.com> wrote:
> Kwa Tanzania nadhani elimu bado sio kigezo cha kumfanya mtu afanue
> maamuzi sahihi ktk kupiga kura.nausea hili kwa sababu hata wasomi wetu
> wanakuwa mstari wa mbele kuhamasisha kuwchaguwa watu wezi na wasio na
> maadili ya utumishi wa umma kwa kitu kidogo wanchopewa.nikiwa chuo
> nilishuhudia wanafunzi wengi bana wakitumiwa na wanasiasa kufanya kampeni
> uku wakijua Kuwa wahusika hawakuwa watu wema kwa kukabidhiwa dhamana ya
> kuongoza nchi yetu.ikiwa wasomi wanatumika kirahisi kiasi iki kwa maslahi
> ya wanasiasa,Je hao mnaosema ni daresa la saba itakuwaje ?
>
> Rgrds
> Magora
> On Oct 18, 2013 9:14 AM, "mngonge" <mngonge@gmail.com> wrote:
>
>> Utafiti huo ulitakiwa useme watanzania wengi wanampenda Kikwete kwa
>> sababu
>> watanzania walio wengi wana elimu ya darasa la saba au chini. Japo nina
>> wasiwasi na design, sample size na namna walivyopick respondents
>> (sampling
>> procedure) kama ni appropriate. Kwa hali tuliyonayo sasa hata hao wenye
>> darasa la saba na kushukachini wamekwishashtuka si rahisi kupata majibu
>> kama hayo. Rais ni kiongozi wa taifa zima hivyo utafiti unaohusu maoni ya
>> raia juu ya utendaji wake lazima uhusishe sample kubwa na iwe na
>> uwakilishi
>> mzuri kwa kila cluster/strata.
>>
>>
>> 2013/10/16 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>>
>>> Na Goodluck Eliona, Mwananchi
>>>
>>> Ripoti mpya ya utafiti imebaini kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wenye
>>> elimu ya darasa la saba na wale wasiosoma, ndiyo wanaokubaliana na
>>> utendaji
>>> kazi wa Rais Jakaya Kikwete.
>>>
>>> Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina la 'Namna Watanzania
>>> wanavyouangalia
>>> utendaji kazi wa Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'
>>> ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Asasi ya Afrobarometer,
>>> inaonyesha
>>> kuwa asilimia 77 ya waliokosa elimu ndiyo wanamuunga mkono Rais Kikwete.
>>>
>>> Afrobarometa ni Asasi ya Kimataifa inayojumuisha taasisi tatu za
>>> Institute for Democracy ya Afrika Kusini, Ghana Centre for Democratic
>>> Development ya Ghana na Political Science Department ya Chuo Kikuu cha
>>> Michigan cha Marekani.
>>>
>>> Mtafiti Msaidizi wa Afrobarometer, Stephen Mwombela akisoma ripoti hiyo
>>> mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema asilimia 72
>>> ya
>>> wale walioishia darasa la saba ndiyo wanamuunga mkono Rais.
>>>
>>> Wakati asilimia 23 ya watu wasiosoma ndiyo hawamkubali Rais na asilimia
>>> 28 ya wale walioishia darasa la saba, pia hawaridhishwi na utendaji wa
>>> kiongozi huyo.
>>>
>>> Mwombela, hata hivyo, alisema utafiti huo uliohusisha watu 2,400 wa
>>> Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wasomi wa
>>> kiwango cha sekondari na kuendelea wanaunga pia mkono utendaji wa Rais,
>>> lakini siyo kwa kiwango cha juu kama wale ambao hawajasoma.
>>>
>>> "Asilimia 60 ya waliosoma elimu ya sekondari na kuendelea wanaunga mkono
>>> utendaji wa Rais, lakini 40 hawakubaliani na utendaji wake," ilisema
>>> taarifa ya matokeo ya utafiti huo uliofanyika kati ya Mei hadi Juni
>>> mwaka
>>> jana.
>>>
>>> Matokeo ya utafiti huo yanatofautiana na yale ya mwaka 2008, ambayo
>>> yalionyesha kuwa wasomi walikuwa wanamuunga mkono Rais kwa asilimia 92.
>>>
>>> Pia katika matokeo ya utafiti huo wa mwaka 2008, ulionyesha kuwa
>>> wasiosoma walimuunga mkono kiongozi huyo kwa asilimia 92.
>>>
>>> Imani ya wananchi kwa Rais
>>>
>>> Ripoti hiyo ilisema pia imani ya wananchi kwa utendaji wa Rais imeshuka
>>> hadi kufikia asilimia 74 kwa mwaka jana, tofauti na asilimia 94 ya mwaka
>>> 2005 wakati aliposhika wadhifa huo.
>>>
>>> Pia utafiti huo uliodhaminiwa na Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa
>>> Umaskini (Repoa) umebainisha kuwa imani ya wananchi kwa Rais imeshuka
>>> kutoka asilimia 88 mwaka 2008 hadi asilimia 74, huku idadi ya watu
>>> wasiokubaliana kabisa na Rais ikiongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 2008
>>> hadi asilimia 26 mwaka 2012.
>>>
>>>
>>>
>>> Imani kwa Bunge
>>>
>>> Wananchi wengi pia wameonyesha kutokuwa na imani na mwenendo wa Bunge,
>>> kwa kulipa asilimia 76 mwaka 2012, idadi yao ikishuka kutoka asilimia 83
>>> ya
>>> mwaka 2008.
>>>
>>> Imani ya wananchi kwa Bunge imeshuka katika kipindi hiki ambalo liko
>>> chini ya Spika Anne Makinda, ambaye alichukua uongozi mwaka 2010 wakati
>>> mwaka ule wa 2008 lilikuwa chini ya Samuel Sitta imani ilikuwa juu.
>>> Taarifa
>>> hiyo pia inaeleza kuwa watu wanaoishi vijijini ndiyo wanaoridhishwa
>>> zaidi
>>> na Bunge kwa kupata asilimia 63, ikilinganishwa na wakazi wa mijini
>>> ambao
>>> ni asilimia 60.
>>>
>>> Pia imebainika kuwa wananchi wa Zanzibar wanaridhishwa zaidi na utendaji
>>> wa Bunge kwa asilimia 64, tofauti na wananchi wa Tanzania Bara ambao
>>> wanaridhishwa kwa asilimia 61.
>>>
>>> "Watu waliokuwa wanakubaliana na utendaji wa Bunge mwaka 2003 walikuwa
>>> asilimia 31, lakini mwaka 2012 idadi iliongezeka hadi asilimia 61,"
>>> alisema
>>> Mwombela wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti huo unaofanyika kwa mara
>>> ya
>>> tano nchini Tanzania.
>>>
>>> Hata hivyo, Mwombela alisema kuwa wananchi wengi bado wanafurahishwa na
>>> utendaji wa Mahakama, lakini idadi yao imepanda kutoka asilimia 73 kwa
>>> mwaka 2008 na kuwa asilimia 74 mwaka 2012.
>>>
>>> Akichangia baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa, Dk Abel Kinyondo, alisema
>>> kuwa matokeo ya utafiti huo hayajaonyesha kuporomoka kwa imani kwa Rais
>>> badala yake yameonyesha uhalisia.
>>>
>>> "Inawezekana imani kwa Rais haijashuka, badala yake imekaa katika hali
>>> yake, kwa sababu kitu gani alikifanya 2008 watu wakampenda sana, ambacho
>>> leo hii hajakifanya hadi wasimpende?" alihoji Kinyondo. Kinyondo
>>> alionekana
>>> kushangazwa na namna Rais alivyoweza kupata asilimia 71 wakati nchi
>>> inapita
>>> katika kipindi kigumu cha rushwa na ufisadi.
>>>
>>> Mwakilishi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor
>>> Kimesera alisema utafiti huo una kasoro kadhaa ikiwa ni pamoja na
>>> kumtaja
>>> Rais kuwa ndiye mwakilishi pekee wa Serikali wakati kuna viongozi
>>> wengine
>>> wengi. "Kwa upande wa Rais walitakiwa kuhoji viongozi wengi zaidi kwa
>>> sababu Rais siyo kiongozi pekee yake katika Serikali," alisema.
>>>
>>> Naye Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Dk Jonas Kipokola
>>> alisema kama utafiti huo ungefanyika Mei hadi Juni mwaka huu, huenda
>>> matokeo yangekuwa tofauti. "Siwezi kusema yangekuwaje, lakini
>>> yasingekuwa
>>> hivyo yalivyo," alisema Kipokola.
>>>
>>> --
>>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>> Disclaimer:
>>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and
>>> facts
>>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that
>>> you
>>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>>> Guidelines.
>>> ---
>>> You received this message because you are subscribed to the Google
>>> Groups
>>> "Wanabidii" group.
>>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send
>>> an
>>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment