Sunday 20 October 2013

Re: [wanabidii] Tanzia: Julius Nyaisanga

Oh, jamani kumbe alikuwa bado mdogo kabisa. Bado tulikuwa tunahitaji huduma yake. R.I.P Julius, Uncle J.

2013/10/20 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Picture
Julius Nyaisanga
Meneja wa Aboud Media, Julius Nyaisanga alias "Super Tall" aka "Uncle J", ameaga dunia.

Taarifa zinasema marehemu Nyaisanga:-
  • Amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Mazimbu, Morogoro alikopelekwa jana mchana kwa matibabu.
  • Alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na kisukari. 
  • Ameaga dunia katika umri wa miaka 53.
  • Ameacha mjane na watoto watatu.

Hapa wavuti.com na Watanzania walio wengi tunamkumbuka marehemu Uncle J kwa umahiri wake wa utangazaji katika 
redio mbalimbali kama vile RTD (sasa TBC) hasa katika usomaji taarifa ya habari na utangazaji vipindi vya burudani na maarifa kama vile Starehe na BPKahawa ni Mali, DJ Show na Uncle J na Club Raha Leo Show.

Pamoja na kuwa kifo huleta huzuni kwa tunaobaki kwa kuwa hatutamwona wala kumsikia tena tuliyempenda, ni vyema pia kumuenzi kwa kazi zake nzuri. Hebu usikiliza moja ya rekodi zake kwenye pleya iliypoachikwa hapo chini ambapo alikuwa na kawaida ya kufunga kipindi kwa kibwagizo cha "fundi mitambo vituuuuuu ni mimi uncle J Nyaisanga. Adios!"

Pia aliwahi kufanya kazi hiyo  ya utangazaji katika vituo vya Radio One Stereo, na ITV. 

Apumzike pema marehemu Julius Nyaisanga!
Utawakumbuka watangazaji wafuatao kuwa moja ya timu bora, mahiri na maarufu kabisa ya watangazaji waliovutia watu kusikiliza redio: David Wakati, Sarah Dumba, Eda Sanga, Jacob Tesha, Ananilea Nkya, Sango Kipozi, Omar Jongo, Ahmed Jongo, Barnabas Mluge, Idrissa Sadallah, Benjamin Kikomongo "Ben Kiko", Bartholomeo Kombwa "Bart Kombwa", Danstan Tido Mhando, Masoud Masoud, Yusuph Omar Chunda, Bujaga Izengo Kadago, Abisai Steven, Angalieni Mpendu, Titus Philipo, Bakari Msulwa, Michael Katembo, Nazir Mayoka, Abdul Ngalawa, Mohammed Kisengo, Abdallah Mlawa, Hendrick Michael Libuda, Abdallah Idrissa Majura, Mikidadi Mahmoud, Rosemary Mkangara, Wilson Malosha, Damian Msangya, Nswima Ernest, Nathan Rwehabura, Betty Chalamila (Betty Mkwassa), Elisia Isabula, Aloysia Maneno, Albert Msemembo, Abdul Masoud, Chisunga Stephen, Siwatu Luanda, Tumbo Tamimu Risasi, Selemani Mkufya, Salim Mbonde, Christine Chokunegela, Kassim Mikongolo, Salama Mfamao, Zawadi Machibya, Juma Ngondae, Salim Seif Mkamba, Nelly Kedela, Dominic Chilambo, Sekioni Kitojo, Malima Ndelema, Khalid Ponera, Julius Nyaisanga, Ahmed Kipozi, Charles Hillary, Aboubakar Liongo, Paschal Mayala, Penzi Nyamungumi, Sued Mwinyi...

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment