Wednesday 9 October 2013

Re: [wanabidii] Tamko la waandishi wa Habari tanzania kusitisha kuandika habari za wizara ya habari

wanahabari kwanza kabisa mngepigania maslahi duni mnayolipwa na
wamiliki wa vyombo vya habari kiasi amabacho wengi wamekuwa wanaishi
kwa mshiko kama wenyewe wanavyouita,

maslahi madogo kwa wanahabari yamesababisha ubabaishaji katika tansia
nzima ya habari na maisha magumu kwa wanahabari, kuna vyombo vya
habari vimekuwa vikaa kwa zaidi miezi mitatu bila ya kuwalipa
wanahabari wao amabo ndio mtaji mkubwa kwao.

kwa correspondent ndio imekuwa balaa kabisa story zinalipwa mpaka kwa
sh.1500 kwa story moja na zinakaa mpaka miezi 3 kupata hiyo pesa ya
story, kitendo ambacho linachangia maisha magumu kwa wanahabari.

Unakuta wahandishi wanafanya kazi mpaka miaka minne katika chombo cha
habari na kuitwa correspondent bila ajira wala mkataba wowote mbaya
zaidi hawana michango hata katika mifuko ya hifadhi ya jamii

Malipo kiduchu na kazi ngumu kwa wanahabari wetu kimesababisha wale
wenye elimu ya kama degree kuachana na kazi hiyo na kutafuta kazi
nyingine.

cha ajabu jumiiya mbali mbali za wanahabari kama press club zimekuwa
hazidai haki za wana habari matokeo yake wamekuwa wakitumika kwa
wanasiasa.

Wakati wamiliki wa vyombo vya habari wakipinga sheria ya habari
iliyofungia magazeti, nawaasa wanahabari nao waamke kwa kuwa na umoja
na kudai maslahi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari.



On 10/9/13, lingson adam <lingsadam@yahoo.co.uk> wrote:
> Wakuu hii ni jino kwa jino: Nifungie nikufungie?
>
> Lakini je wakivurunda mathalani kula rushwa, kufanya jaribio la uhaini hawa
> kina Fenella na Assa, halafu habari zao zisiandikwe, si itakuwa faida kwao?
>
>
>
> Suppose hawapendi publicity hawa jamaa (Fenella na Assa) si watakuwa
> wamepewa zawadi ya kutoandikwa hawa?
>
>
> Je habari zinazolenga kuwajenga wakiwapa watoa habari wengine hili shinikizo
> litawagusa kwa namna yoyote?
>
> Mwisho, hivi tunapoandika habari ni zawadi kwa watoa habari? Uandishi wetu
> hapa vipi wakulu?
>
>
> Ninachofurahia ni kwamba wanahabari wamechukua hatua! Iwe butu au na makali,
> lakini hatua imechukuliwa. Natumaini moto huu hautazimika.
>
>
>
>
> ________________________________
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Wednesday, October 9, 2013 5:33 PM
> Subject: [wanabidii] Tamko la waandishi wa Habari tanzania kusitisha
> kuandika habari za wizara ya habari
>
>
>
> AMKO LA WADAU WA HABARI WALIOKUTANA KUJADILI MUENDELEZO
> WA SERIKALI WA KUFUNGIA VYOMBO VYA HABARI, KATIKA HOTELI YA SERENA, JIJINI
> DAR ES SALAAM
> TAREHE 9 OKTOBA, 2013.
>
> Wadau wa habari waliokutana jijini Dar es Salaam leo, tarehe 9 Oktoba 2013,
> wamesikitishwa na hatua ya serikali ya kutosikiliza kilio cha wamiliki wa
> vyombo vya habari, wahariri, waandishi, taasisi za vyombo vya habari,
> wasambazaji wa magazeti na watu wengine wa kawaida, juu ya kuyaondolea
> adhabu magazeti matatu yaliyofungiwa na serikali ya MwanaHALISI, MTANZANIA
> na MWANANCHI.
>
> Aidha, wadau wamesikitishwa na hatua ya serikali ya kupuuza kilio chao cha
> kuomba kusitishwa kwa sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976; na
> kudhoofisha mchakato wa kuibadilisha sheria hiyo iliyotajwa na Tume ya Jaji
> Francis Nyalali mwaka 1992 kuwa ipo kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano
> wa Tanzania.
>
> Vilevile, tumesikitishwa na hatua ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
> Michezo, Mheshimiwa Dk. Fenella Mukangara na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
> (Maelezo), Assah Mwambene ya kudharau na kufanya uamuzi wa kuyafungia
> magazeti hayo bila kuyasikiliza na kupotosha umma juu ya jambo hilo.
> Kwa msingi huo, wadau wameazimia yafuatayo:
>
> 1. Kusitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha, shughuli zozote
> zitakazowahusisha au kuratibiwa na Mheshimiwa Fenella Mukangara na Assah
> Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja
> kuanzia leo.
>
> 2. Wadau wa habari tutaendelea kupinga sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa
> kupigia kelele kufutwa kwa sheria hiyo na kuongeza nguvu ya kisheria
> mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers
> Ltd, mwaka 2009 inayopinga sheria hiyo.
>
> 3. Tunaowamba wananchi wote watuelewe kwa kuchukua hatua hii.
>
> Uamuzi huu umefikiwa leo na wadau wahabari, kutoka taasisi zifuatazo:
> 1. Chama cha Wamiliki wa vyombo vya Habari (MOAT).
> 2. Jukwaa la Wahariri (TEF).
> 3. MISA Tan
> 4. Baraza la Habari Tanzania (MCT).
> 5. Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)
> 6. Dar City Press Club (DCPC)
> 7. Tanzani Human Rights Defenders (THRDC)
> Mwisho.
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment