Friday 18 October 2013

Re: [wanabidii] Tahadhani kama wewe sio mwendaji wa Katikati ya Jiji (Posta) mara kwa mara

Mndeme;
Unachoongea ni sawa,kutafutwe njia nyingine zaidi za kuwafikishia taarifa wananchi badala ya vibao tu tena ambavyo ni vidogo au kuwasubiri wakosee walipishwe faini,huu sio ustaarubu mana information/communication is power always.
Kuna vyombo vingi vya habari k.m. magazeti,TVs,Radio n.k mbavyo vikitumika kwa muda kama mwezi mmoja watu wengi tutakuwa na taarifa nini kinachoendelea.
Uzuri wa Maafande ukikubali kosa na kuomba msamaha huwa ni waelewa sana.

 
Reuben



On Thursday, October 17, 2013 11:28 PM, Mathew Mndeme <mathewmndeme@gmail.com> wrote:
Kwa Waendesha Magari ....Chukua Taadhari unapokwenda Posta
Kwa sisi ambao tunafanya kazi  na kutekeleza wajibu wetu wa kila siku pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam, kwenda Posta ni kati ya maswala magumu na mtu unafanya hivyo tu unapolazimika sana. Hivyo ni jambo la kawaida kabisa kwenda Posta na kukuta mabadiliko makubwa kama vile barabara au jengo jipya kwa sababu tu hujafika muda mrefu.

Leo nilikwenda Posta na baada ya kumaliza yaliyonipeleka Posta nilikua na safari ya kwenda kununua nyanya, vitunguu, dagaa, bamia na ngogwe sokoni Kariakoo. Hivyo nilitokea barabara ya Ohio na kuingia Bibi Titi Muhamed. Mahesabu yangu ilikua niingie Barabara ya Morogoro na kisha nielekee Kariakoo kwa kupitia pale Fire. Kwa kua hapakua na foleni, nilikuja kwa kasi ya kawaida na nikaonesha  kiashiria cha kuingia Barabara ya Morogoro. Bila kujua kuwa hakuna tena uwezekano wa kutoka Barabara ya Bibi Titi na kuingia ya Morogoro, nilishangaa kuona wa nyuma yangu ananipigia honi kuwa napoteza muda. Nilipojaribu kukata kuingia Morogoro nikashtuka kuwa hakuna njia na nilipopita sio mahali halali pa kuingia. Wakati nashtuka na kurudi nyuma, ili ninyooke na Bibi Titi, ghafla nikaona askari wa usalama barabarani ananiita mbele yangu kua nisimame. Akaingia ndani ya gari na kunieleza makosa yangu. Kwa maelezo yake pale nilikua nimefanya makosa matatu kwa wakati mmoja: Kutumia barabara vibaya, kutokufuata sheria za barabarani, na kutaka kusababisha ajali kwa kupita kusikoruhusiwa. Nilitakiwa kulipa 90,000/= (30,000/= kwa kila kosa). Ilibidi nivute pumzi jinsi ya kujieleza hadi nikajikuta naanza kwa kujitambulisha jina, ninakotoka na ninapofanya kazi  kama vile najitambulisha kwenye mkutano kabla ya kuanza kutoa mhadhara au kuchangia mada...usicheze na kulipa faini ambazo hujazitegemea.

Kusema ukweli nilichoka na kwa uungwana na ukweli wa moyo nilimweleza yule askari kuwa sikukusudia kuvunja sheria ila ukweli ni kuwa sikua na taarifa kuwa barabara zile kubwa mbili haziingiliani tena. Nilimwambia kuwa sijapita hiyo barabara muda mrefu kidogo na mara ya mwisho nilipopita ujenzi wa RBT ulikua unaendela na njia hizo zilikua zinaingiliana. Nilijaribu kumwambia kuwa, kwa mtu yeyote anayeijua DSM ni ngumu kuwaza kuwa kuna hayo mabadiliko katika eneo kama lile. Sikujua kuwa nilikua najielezea uzembe wangu wa kutokutazama vibao vipya...kumbe kuna vibao viwili pale vyenye alama ya kutokukunja kulia na kukuelekeza usonge mbele. Alinikatalia na kunipeleka kulipa faini.

Nilishangaa kujua kuwa lile lilikua eneo mkakati la askari kwani wamejenga hadi kibanda pembeni kwa lengo la kukamata watu pale na kulikua na askari kama watano hivi. Kwa kuwa ndani mwangu sikua kabisa na mpango wa kuvunja sheria wala makusudi yoyoye niliona halali kulipa ile pesa. Hivyo niliamua kuongea nao wote kwa muda kama dakika tano kwanza kueleza ugumu wa kuelewa yale mabadiliko na pili kuomba msamaha maana ningekosa pesa za kununua tena bamia iwapo ningelipa faini. Ninamshukuru Mungu na ninawashukuru wao kuwa nilipokubali kosa la kutokujua mabadiliko ya njia na kuomba msamaha; walinielewa na wakaniruhusu kuondoka bila kulipa...ingawa hawakauniacha bure kwani walisema kutokulipa faini kumetokana na "upare wangu"...tukacheka wote.

Nikiwa pale  kwa zile dakika chache nilithibitisha kile nilichokua nawaeleza wale askari kuwa ni ngumu sana kwa mgeni wa mjini/njia ile kutokosea pale kwani ndani ya dakika kama tano nilishuhudia watu kadhaa wakikamatwa kwa kosa kama langu ambalo limetokana na yale mabadiliko kutokujulikana na ni ngumu sana kujua njia imefungwa kwani hata vibao vya alama za maelekezo ni vidogo.

Niwashauri wale wanaoendesha magari kuwa ukiwa unatokea Posta na barabara ya Bibi Titi hakuna ruhusa kuingia Barabara ya Morogoro. Kama una huo mpango, inakulazimu kunyooka hadi Mnazi Mmoja ndio utafute namna ya kugeuza urudi tena na Bibi Titi kuipata Morogoro au ukapitie barabara ya Lumumba kurudi Morogoro. Hakuna kuingia Morogoro kwa upande wa kuelekea Fire wala kuelekea Samora..Unapitiliza. Kwa maelezo ya wale watumishi wa umma (askari) niliowakuta pale walianiambia kuwa ile junction ni njia ya kupita mabasi ya RBT kwenda na kurudi katikati ya mji na sio kwa gari linguine lolote lile.

Pia nashauri badala ya kutumia hiyo nafasi kama mahali pa kuwatoza faini kubwa wakosaji wasio na hatia kama ambavyo ingekua kwangu, pawekwe vibao vikubwa zaidi na itafutwe namna nyingine ya kufanya yale mabadiliko ya njia zile kuu kujulikana na watu wengi zaidi.

Nimeona nikutaadharishe wewe usomaye ili usipate usumbufu na kulipa faini kubwa kwa kutokujua kama mimi ilivyonikubwa leo.


MM

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment