Friday 11 October 2013

Re: [wanabidii] Taarifa ya Naibu Waziri juu ya ruhusa ya kurejea kuchapishwa Mwananchi, Rai online

Hapa ndipo ninapoamini kuna matatizo makubwa kwenye Serikali yetu, ndani ya wiki mikanganyiko miwili inajitokeza wazi kwenye utendaji wa Serikali na hivyo kuzidi kuipunguzia haiba yake mbele ya umma. Mimi kwa binafsi yangu nabaki na mambo matatu nikijiuliza, moja kuna viongozi wasiofahamu sheria, madaraka na majukumu yao, mbili wapo viongozi wanaotumia madaraka yao kupindisha sheria kwa maslahi binafsi. Tatu wapo viongozi wanaofahamu wajibu wao na sheria za kuzisimamia lakini hawana nguvu ya maamuzi hawa wote wanafanya kazi chini ya mwamvuli mmoja hapo ndipo ninapoliona tatizo linalolikabili Taifa letu. Naomba kuuliza hivi idara ya habari maelezo iko chini ya wizara gani?

Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

>*JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
>*WIZARA YA HABARI, VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO*
>
>*TAARIFA KWA UMMA*
>
>Napenda kuufahamisha umma kwamba *mimi ndiye NILIYERUHUSU* Gazeti la
>Mwananchi kuendelea na utoaji wa taarifa/habari kwenye tovuti yake, pia
>Gazeti la Rai kutoka kila siku.
>
>Ninalazimika kutoa ufafanuzi kwa njia ya maandishi kutokana na kupigiwa
>simu nyingi na waandishi wa habari kuhusiana na tamko jipya la Mkurugenzi
>wa Habari – Maelezo, Ndg Assah Mwambene kuhoji uhalali wa Gazeti la
>Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai kutoka kila siku, badala ya mara
>moja kwa wiki (Alhamisi).
>
>Tarehe 4/10/2013 nilifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Mwananchi
>Communication Ltd (MCL) na New Habari
>Corporation (2006) Ltd kwa upande mmoja na msajili wa magazeti kwa upande
>mwingine.
>
>*Katika kikao hicho cha pamoja na viongozi wa Magazeti ya Mwananchi na
>Mtanzania maombi matatu yaliwasilishwa;*
>
>*1. * Ombi la kumuomba waziri apitie upya adhabu iliyotolewa kwa mageazeti
>hayo. Katika hili Majibu yangu niliwaambia kwamba mwenye mamlaka juu ya
>suala hilo ni waziri mwenye dhamana na masuala ya habari pekee.
>
>*2. * Ombi la Gazeti la Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai kutoka kila
>siku badala ya kutoka siku ya Alhamis.
>
>*2.1 * New Habari walieleza kuwa siku zilizopita waliwahi kuomba kwa
>maandishi (barua) kwamba gazeti la Rai litoke kila siku. Maelezo ya Naibu
>Msajili wa Magazeti katika kikao hicho yalikuwa kwamba, kulikuwa na tatizo
>la kiufundi katika kurejea maombi hayo na akakiri kuwa hakuna kinachozuia
>gazeti la Rai kutoka kila siku. Kutokana na maelezo hayo mimi niliridhia
>gazeti hilo sasa liruhusiwe kutoka kila siku.
>
>*2.2 * Kuhusu gazeti la Mwananchi kuwa online, Naibu Msajili alisema
>hakuna sheria yeyote inayoweza kuzuia gazeti hilo kuwa online ila aliwataka
>lisionekane gazeti zima kama lilivyo pia wabadili nembo (Master Head)
>kwamba waweke nembo ya MCL na siyo ya gazeti husika ambalo limefungiwa. Pia
>baada ya maelezo hayo niliridhia gazeti hilo liwe mtandaoni kwa kuzingatia
>angalizo lililotolewa na Naibu Msajili wa Magazeti.
>*
>3. *Hoja ya tatu ilikuwa ni ile ya Serikali kupitia Idara ya Habari -
>Maelezo kuwa na uhusiano mzuri na vyombo vya habari, ili kuepuka misuguano
>isiyo ya lazima.
>
>*3.1 * Pendekezo hili nililipokea na niliwasilisha kwa Mhe Waziri wa
>Habari kwa hatua zaidi, likiwamo suala la kupitia upya adhabu na ushauri wa
>kujenga uhisiano na vyombo vya habari.
>
>*3.2 * Masuala ya Gazeti la Mwananchi kuwa* online* na Rai kutoka
>kila siku, NILILITOLEA UAMUZI siku hiyo hiyo, na uamuzi ni kwamba
>niliwaruhusu baada ya kuridhika kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa sheria
>yoyote uliofanywa na waombaji.
>
>Nimeamua kuweka sawa jambo hili kutokana na taarifa ya Mkurugenzi wa
>Maelezo ambayo ninaamini kwamba kutolewa na kusambazwa kwake ni kukosekana
>kwa mawasiliano kati yake kwa uipande mmoja na Mhe. Waziri, Naibu waziri na
>Naibu Msajili wa Magazeti kwa upande mwingine.
>
>Hivyo aliyeruhusu Gazeti la Mwananchi kuwa online na Rai ni mimi na ndiyo
>maana kuanzia tarehe 5/10/2013 Gazeti la Rai lilianza kuchapwa kila siku na
>kusambazwa, na Gazeti la Mwananchi likaanza kuwa mtandaoni kwa kuzingatia
>maelekezo ya Naibu Msajili wa Magazeti.
>* ** *
>*Imetolewa na:*
>
>*Amos G. Makalla*
>*Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo*
>*11 Oktoba 2013*
>------------------------------
>
>
>Kwa kumbukumbu tu, jana, Oktoba 10, 2013 ilitoka taarifa kwa Waziri wa
>Wizara hiyo hiyo kupitia Idara ya Habari, ikikumbushia adhabu iliyotolewa
>ya kutokuchapishwa kwa magazeti hayo hata kwenye mitandao yao ya kijamii na
>kuonya kuhusu kutii sheria kama inavyoelelekezwa. Nukuu ya taaria hiyo ni
>hii ifuatayo:
>
>JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
>WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
>
>*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
>
>Idara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba
>Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
>Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na
>Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia
>kuanzia 27 Septemba, 2013.
>
>Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari
>maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka
>masharti ya adhabu walizopewa.
>
>Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza
>gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa
>Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku
>ya Alhamisi.
>
>Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo
>katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.
>Serikali inawataka wamiliki wa vyombo habari nchini kuwa na utamaduni wa
>kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali
>kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA,
>kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI.
>
>Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja
>kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa ilivyoanisha.
>
>Imetolewa na,
>*Idara ya Habari – MAELEZO
>10 Oktoba, 2013*
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment