Tuesday 22 October 2013

RE: [wanabidii] Stori za uongo zinazowafanya watu kuichukia nchi yao

Ni bahati mbaya sana, tena sana, kwa mtu kuiponda nchi yake bila umakini wowote bali ushabiki na kutokujua. Hakuna mgeni atayeisifia nchi yako bure bure tu. Tunaweza kukusoana tukiwa ndani chumbani lakini kujiadhiri mbele ya wageni ni tatizo kubwa; ni kuwapa silaha maadui zetu.

Matinyi.


From my Android phone on T-Mobile. The first nationwide 4G network.



-------- Original message --------
From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Date: 10/22/2013 6:38 PM (GMT+03:00)
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Stori za uongo zinazowafanya watu kuichukia nchi yao


TUACHE KUJINYANYAPAA KWA KULETA STORI ZA UONGO!
NANI KAKWAMBIA WAKATI WA UHURU 1961 TULIKUWA SAWA NA MALAYSIA! TUNAFANYA WATU WAICHUKIE BURE NCHI YAO KWA KUWAPA USHAHIDI WA UONGO JUU YA MATAIFA MENGINE!

Naamini wengi wenu mmeshasikia watu wakiIfananisha NCHI YETU na Malasyia, China, Japan, Korea nk kuwa tulikuwa nao sawa wakati wa uhuru, wengine wana sema wakati tunapata uhuru nchi hizo zilikuwa masikini sana sawa na sisi na sasa wametupita sana. Hizi ni fikra za kujinyanyapaa na zinazowapotezea watu dira ya uzalendo kwa Taifa lao.

Malaysia wakati inapata uhuru wake Mwaka 1957 tayari walishakuwa wanavyuo Vikuu Viwili ambavyo ni University of Malaya kilichoanza mwaka 1949 na MARA University of Teknology kilichoanzishwa mwaka 1956 na vyuo vingine vya elimu za juu kadhaa. Sisi tunapata Uhuru 1961 tulikuwa 0, na mwaka huo ndio juhudi zikaanza kwa wanafunzi 14 kwa kuazima jingo la TANU. Hivi tulikuwa sawa kweli?

ChinamMpaka mwaka 1961 wakati tunapata Uhuru washakuwa mamia ya vyuo vikuu, kwa uchache mno baadhi ni Fudan University -1905, Shanghai Jiao Tong University-1896, Peking University-1898, Tsinghua University-1911, Renmin University of China-1937, Beijing Normal University-1902. Hivi kwa staili hii tulikuwa sawa na China miaka tunapata Uhuru wetu? China Hiyo hiyo kati ya mwaka 1940 na 1950 walikuwa wamefanikiwa kutengeneza ndege Moja ya Kivita wenyewe. Sisi tullikuwa wapi kipindi hicho? hivi ni watu wa kujilinganisha nao hawa?

Japani ndio kabisa wala sio ya kujilinganisha nayo kwani hadi mwaka 1961 ilishakuwa na vyuo vikuu lukukika baadhi ya hivyo kwa uchache sana ni Tokyo Denki University 1949, Akita University 1949, Hirosaki University 1949, Ehime University 1949. Japan mwezi wa 12, 1941 lakeke lilivamia Marekani kule Hawaii na kufanya mashambulizi mazito ya anga katika kambi ya kijeshi na kuua makomandoo 2,402, kuangamiza ndege za kijeshi za Marekani 188, kufanya uharibifu mkubwa kwa ndege 159, kuzamisha meli 4 za kivita na kuharibu zingine na madhara mengine mengi. Japani Tangu miaka ya 1930s imekuwa ikitengeneza Ndege kwa mamia. Hivi kweli tuna sababu ya kujilinganisha na Japan?

Tuache stori za uongo zinazowafanya watu kuichukia nchi yao na kupunguza uzalendo wao kwa Taifa letu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment